Hospital ya muhimbili yamsababishia kansa mama huyu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospital ya muhimbili yamsababishia kansa mama huyu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kurunzi, Feb 27, 2011.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kisa hiki kimenikatisha tamaa na huduma za pale muhimbili kisa hiki cha mama mmoja amekufa kwa kansa ya jino.

  Ilikuwa hivi mama huyu alikuwa na mauumivu ya jino na lilikuwa limetoboka alipoenda pale muhimbili dak. Wa meno akamcheki na aliamua kuliweka jino risasi na kumruhusu huyo mama aende, baada ya muda wa kama miakaaka miwili hivi mama huyu akaanza kupata maumivu makali ya hilo jino hali iliyomlazimu kurudi tena muhimbili na baada ya kumchek dk. Alimpadawa za kutuliza maumivu tuna na kuöndoka na kadri siku ziliposonga maumivu yalizidi kuwa makali hali iliyomlazimu kusaka huduma sehemu nyingine ndipo aliponda kwa dk.mmoja Mhindi pale kariakoo dk. Alipomchek aligumdua risasi aliyowekewa pale muhimbili iliwekwa vibaya na kuingia kwenye fizi, kuona hivyo dk. Alimpigia simu huyo dk. Wa muhimbili na kumulezea kwani walikuwa wanafahamiana ndipo dk. Huyo wa muhimbili alipotanabahrha itakuwa ni dk. Mwanafunzi alimueka huyo mama rirasi.

  Ilibidi huyo mama kuöndolewa híyo sisari na kufanyiwa vipò zaidi na ndipo ilipogundulika amepata kansa ya jino iliyosababishwa na risasi aliyowekewa pale muhimbili.
  Baada ya mama huyo kupata majibu hayo alipatamshituko na badaye kufikiwa na mauti 'Leo tunamzika pale kimara lous.
   
 2. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wataalam wa tiba tuwe makini ktk utendaji wetu wa kazi kuondoa/matatizo kama haya jamani.Ni vema kumsikiliza mgonjwa vizuri,kujali na kufanyia kazi kwa ustadi mkubwa kila complain anayoi present.Kama mama huyu angesikilizwa na kuchunguzwa vizuri mapema yasingefikia huku.POLENI SANA WAFIWA...R.I.P
   
 3. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli huduma za afya ni mbovu pamoja na kwamba watoa huduma wa afya wanafanya kazi katika mazingira magumu lakini kuna mambo madogo wanashindwa kuyafanya mpaka yana hatari maisha ya wagonjwa.
  Hata wale wa fast track bado wanalipua.
   
 4. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2012
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,593
  Likes Received: 25,516
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu wangu alizibwa jino na wazungu more than 15 years ago hapohapo Muhimbili na aliambiwa halitamsumbua kwa zaidi ya miaka 20 , mpaka sasa hakuna hata dalili kwamba litakuja kumsumbua tena , lakini nowdays ukizibwa jino huwezi maliza hata miezi 2 kabla ya kupata matatizo , Swali , tatizo ni uafrika wa wataalamu wetu ? Ushauri kwa wagonjwa msizibe meno muhimbili , kesi za matatizo ni nyingi mno , bora kung'oa .
   
 5. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  juzi juzi mh Pinda alisema eti Muhimbili inaongoza kwa
  vifaa bora vya matibabu ya meno Afrika mashariki na kati.
  sawa wanaweza kuwa navyo, lakini kama wahudumu wenyewe ndio hao
  hata haileti maana yeyote.
   
 6. m

  mpenyo Member

  #6
  Nov 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Fanya uchunguzi usikurupuke,cancer haina specific cause ina risk factors. Una uhakika kama hakuwa nayo kabla ya kuwekewa hizo risasi? Na umejaribu kuulizia kama hizo risasi zina risk ya kusababisha cancer? Hayo maumivu yalikuwepo na ndiyo maana akaenda muhimbili,je unawezaje kuthibitishi kama hayakuwa yanatokana na cancer aliyonayo ila hawakuigundua maana hata sasa hivi maumivu hayo hayo ndiyo yamefanya wagundue kuwa ana cancer.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kuwa na vifaa na kumismanage mgonjwa ni vitu viwili tofauti. Kama daktari alijua ahana vifaa vya kutosha kumuwekea risasi mgonjwa hakupaswa kufanya hivyo na kurisk afya ya mgonjwa.
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Umejitahidi kumjibu kwa logical questions lakini naweza mikawa na swali la ziada kwako.

  Is it ethical mtu akija kwsko complaining of toothache wewe kama dentist or dental therapist kufikilia kuling'oa without finding the root cause of pain and there is any predisposing disease to that pain?
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Da namkumbuka sana huyo mama ameacha watoto warembo kweli na mwingine yupo USA,siku ya mazishi yake nakumbuka mwanawe alikuwa anaangalia live thru skype maana alishindwa kuja ni mama wa kipare!!
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  katika pita pita yangu kwenye mavitabu sijawah kitu kinachosababisha kansa ila nimekutana na predisposing factors ambazo humfanya mtu apatehiyo kansa. yawezekana kabisa mama huyu tayari alikuwa na hiyo kansa na ndio ilomsababishia maumivu hayo ya jino, lkn pia isingekuwa ni rahisi sana kwa dr kugundua kwa siku moja kwani inahitajika diagnosis ya muda mrefu hasa kwa nchi zetu zinazoendela.kwa wenzetu najua ni kitu cha sikunde tu.

  kwangu m simlaumu dr kwani kama mama tayari alikuwa na viashiria vya kansa ambavyo hakuvijua pia sio kosa lake ni kosa la diagnositic facilities. lakin pia dr alipoendewa kwa mara ya pili alipaswa afanye uchunguzi zaid kuliko kukata tamaa mapema na hata kufikia kukubali lawama eti risasi iliekwa vibaya................ angejiuliza kama ikiekwa vibaya fate yake ni kansa?? kama ndio kwan inapoekwa kwenye jino isilete kansa baadae?? siamini kama risasi za meno ni predisposing factor za kansa ila kama kuna vitu kama matumizi ya tumbaku, ulaji wa kabichi, upakaji wa rangi za midomo nk haya yanaweza asababisha.

  ni vyema basi kwa wizara husika kuongeza nguvu katika kugharamia vifaa tima hasa kwa ajili ya diagnosis ili kukwepa mgonjwa kutibiwa ugonjwa tofauti kwa dalili zinazoshbihiana hasa ukiangalia dalili za magonjwa mengi zinafanana sana.
   
Loading...