Hospital ya KCMC yasitisha huduma kwa watumiaji wa bima za AAR, JUBILEE na NSSF

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,495
3,458
HOSPITALI ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro imesitisha kutoa huduma kwa wanufaika wa huduma za Afya kutoka kwa baadhi ya taasisi,mashirika na Kampuni za Bima zikiwemo AAR na Jubilee.

Baadhi ya taasisi nyingine ambazo Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC umezitangaza kusitisha huduma kwa wanufaika wake ni pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Strategies ,Shirika la Umeme (TANESCO) na kiwanda cha sukari cha TPC.

Hatua hiyo inatajwa kuwa ni Madeni yaliyotokana na utoaji wa huduma kwa wanufaika wa baadhi ya Tasisi,Mashirika na Kampuni hizo ,madeni yanayokadiliwa kufikia Bil 2.2.

Afisa habari wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Gabriel Chiseo alisema taasisi hizo zimeshindwa kulipa gharama wanazo dai kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba walioingia na taasisi pamoja na mashairika hayo ,gharama ambazo zinapaswa kulipwa kila baada ya mwezi mmoja.

Crdt: Dixon Busagaga, Moshi. .
 
Mwisho wa siku wanyonge ndio wanaathirika.
Kwa nini hayo mashirika yasiwajibishwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom