Hospital ya Hindu Mandal ipo sehemu gani?

MartinCoder

JF-Expert Member
Feb 20, 2018
700
629
Naombeni maelekezo kutoka kwa yeyote anayejua mahali ilipo hospitali ya Hindu Mandali na jinsi ya kufika katika hospital hiyo kutokea Gongolamboto
 
Kama ni ya City Centre... Fika Azam Ice cream Centre Round about Jamhuri na Mkwepu Street ulizia kuanzia hapo.
 
Ipo Chusi Street jirani na hapo Azam Ice cream Round About... Ki mjini mjini ni bora uanzie hapo. Miaka yooote Sijui ipo mtaa gani
 
Naombeni maelekezo kutoka kwa yeyote anayejua mahali ilipo hospitali ya Hindu Mandali na jinsi ya kufika katika hospital hiyo kutokea Gongolamboto
Panda dldl za Kivukoni ukitokea huko Gongo la Mboto, Shuka Posta Mpya, rudi nyuma hadi kituo cha mafuta GBP, fuata barabara inayoenda Azam Ice cream (Mtaa wa India), ulizia mtaa wa Chusi au Chewa au ulizia Msikiti wa Ngazija/hospitali ya Hindu Mandal. Msikiti huu umetenganishwa na barabara, utaanza Hospitali unayotaka kufika. Vlvl waweza kutumia Google map
 
Sorry Nikishashuka then Nikarudi nyuma hyo barabara inayoelekea azam ice cream ipo kulia au kushoto ?
 
Unarudi nyuma kama unakwenda Maktaba. Mkono wa kushoto utaona kituo cha mafuta cha GBP. Kati ya kituo hicho cha GBP na jengo la Haidery Plaza kunatenganishwa na barabara. Hy barabara ndiyo inaelekea Azam Ice cream (Barabara ya mtaa wa India)
 
IMG_3846.JPG
IMG_3845.JPG
 
Kama unatumia Smartfon, ukishuka Posta mpya pale, ingia kwenye cmu yako, fungua google map, kisha search Hindu Mandal.. Itakusaidia hiyo.. Otherwise kama utaweza kuielewa hiyo ramani niliyoi-screeshot hapa, inaweza kukusaidia..
Screenshot_20180913-230018.jpg
 
Unarudi nyuma kama unakwenda Maktaba. Mkono wa kushoto utaona kituo cha mafuta cha GBP. Kati ya kituo hicho cha GBP na jengo la Haidery Plaza kunatenganishwa na barabara. Hy barabara ndiyo inaelekea Azam Ice cream (Barabara ya mtaa wa India)
Thanks
 
Nilitembelea maeneo mengi Sana Dar Tena kwa mguu kwa kutumia Google Map bila kuuliza mtu.
 
Back
Top Bottom