Hospital Na Madaktari Tz Hawaaminiki?

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
19,855
34,061
MBUNGE wa Mbeya Vijijini, Bw. Richard Nyaulawa (CCM), Mbunge wa Chakechake, Bibi Fatuma Maghimbi (CUF) na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bw. Joseph Rwegasira, ni miongoni mwa Watanzania waliolazwa katika hospitali ya Apollo, jijini New Delhi, India.

Wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Meya wa Manispaa ya Tabora, Bw. Peter Lembeli, mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), Bibi Fatuma Ndolanga, Bw. Ali Rashid Umande, Bw. Peter Mapunda na Bibi Juliana Magufuli.

Wagonjwa hao walitembelewa juzi na Makamu wa Rais, Dkt. Ali Mohamed Shein, ambako alipata fursa ya kuwajulia hali na kuwaombea wapate nafuu haraka ili waweze kurudi nyumbani.

Katika ziara hiyo hospitalini hapo, Makamu wa Rais na ujumbe wake, walitembezwa katika maeneo mbalimbali ambapo alijionea vifaa vya kisasa vinavyoiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma bora.

Akizungumza na uongozi wa Apollo, Dkt. Shein alielezea kufurahishwa kwake na huduma zinazotolewa na hospitali hiyo na kusema yeye na ujumbe wake walikuja hapa kujadili uwezekano wa kuimarisha ushirikiano na Tanzania.

Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo, Dkt. Prathap Reddy, aliahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania na kusema mfano hai ni mpango walionao wa kujenga hospitali ya aina yake Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa Tanzania na nchi jirani.

Dk. Shein aliridhishwa na kauli hiyo na kusisitiza hospitali hiyo ijengwe haraka iwezekanavyo, ili kusogeza huduma za matibabu ya moyo na magonjwa mengine karibu na wananchi.

Akichangia katika kikao hicho, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dkt. Mary Nagu, aliuomba uongozi wa hospitali hiyo kuanzisha mpango wa kubadilishana wataalamu ili kuboresha ujuzi katika sekta ya afya.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyihaji Makame, aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuchunguza kwa makini viwango vinavyotozwa kwa wagonjwa, kwa kuwa inadaiwa ni vikubwa ikilinganishwa na hospitali nyingine za Apollo za Chanai na Hyderabad.

Kikao hicho pia kiliitaka timu ya wataalamu kutoka Tanzania na India ikamilishe taratibu zote za kuwezesha kusainiwa kwa makubaliano ya kushughulikia masuala ya kuleta wagonjwa India na kujenga uwezo wa wataalamu katika fani ya afya.

Wakati huo huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, alisema Serikali ya Tanzania inashughulikia deni la dola zipatazo 424,000 za Marekani linalodaiwa na hospitali hiyo na kwamba fedha hizo zitalipwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Hospitali hiyo ambayo ni maarufu kwa kutibu magonjwa ya moyo na saratani, pia inashughulikia upasuaji bandia na wa ubongo na mishipa ya fahamu.

Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini India, Bw. John Kijazi, wagonjwa wapatao 626 wametibiwa katika hospitali hiyo na jumla ya sh. bilioni 2 zimetumika kwa matibabu hayo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka jana.
source : majira
 
Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini India, Bw. John Kijazi, wagonjwa wapatao 626 wametibiwa katika hospitali hiyo na jumla ya sh. bilioni 2 zimetumika kwa matibabu hayo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka jana.
source : majira

Mkuu Operation za kichwa na miguu umesahau!! mmmhhh hospital za Tz ni kwa sisi walalahoi na "wafa kwa kulima" Hivi hizo Bil 2 zingeweza kujenga viyuo vingapi vya afya ama maboresho ya hospitali zetu? nina maana pamoja na kuongeza malipo na posho kwa madaktari wetu.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom