Hospital inayotoa huduma nzuri Kwa Dar es Salaam kati ya Regency, Aga Khan na Hindul Mandal kwa vipimo vya mwili mzima?

King_Villa

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
575
378
Habar za mida wakuu,

Binafsi huwa napenda kila Mwisho wa mwaka kufanya full body check up.
Naangalia mwili wangu unahitaji nini.
Naangali sukari mwilin.
Naangalia sumu ikoje mwilini.
Damu naipima kila kitu.
Nachek H.I.V

Kiujumla naangalia mwili mzima.

Sasa nahitaji sehemu nzuri yenye vifaa vya kutosha kati ya hizo zilizotajwa.
 
Aga Khan ndio mwisho wa matatizo mkuu.
Yaani hata kama ulienda pale na stress zako kwa kweli unajisikia raha. No foleni, mazingira mazuri sana na ya kuvutia, huduma nzuri sana, madaktari na watoa huduma wana lugha za kuvutia na za kupendeza huku wakiwa na nyuso zilizojaa tabasamu na bashasha mwanana.
Nilimpeleka wife hapo mwezi wa kumi, aisee i never regretted!! The only thing ni kuwa gharama zao ziko juu, but i swear its worthy it!! Ultra sound ya tumbo tu ni Tshs 110,000 kudadadeki!!!
Kama gharama sio tatizo kwako au bima yako inapokelewa aga khan, go for it!!
Veyron
 
Dr. Wansegamila,
Hivi kwa nini wahudumu wa hospital za serikali wengi wako harsh?

Ni mazingira ya kazi ama kitu gani
Jana nilikua hospital moja ya serikali,Dr amenuna nimemuelezea sijamaliza kashaandika kanipa karatasi

Baada ya vipimo Dr mwingine akauliza mbona naona kuna kitu kikingine hukusema

Nikamwambia nilisema labda Dr wa kwanza alisahau kuandika

Usipokua makini unatibiwa maradhi ambayo hayakuhusu.

Kairuki wana customer care kwa ma Dr ila pale reception kuna katatizo kadogo

Agha khan
salute kwao.
 
Hornet,
Ngoja niongee kwa mifano.
Daktari X anayehudumia wagonjwa 20 kwa siku, na Daktari Y anayehudumia wagonjwa 120 kwa siku, yupi yupo likely kuwa na hasira kwa wagonjwa wake?

Daktari X aneshuhudia vifo vya wagonjwa wake kila siku, kwa sababu tu hakuna dawa Z au kifaa fulani ambayo ilikua inahitajika kuokoa maisha yao, na daktari Y ambae anapofanya kazi kuna kila aina ya dawa, vifaa na vipimo vitakavyohitajika kuokoa maisha ya mgonjwa pale ambapo daktari huyo ana uwezo wa kufanya hivyo, nani atakua na hasira zaidi kwa wagonjwa?

Daktari X ambae anakuja kazini huku akiwaza deni analodaiwa na mwenye nyumba, na ada ya mtoto wake ambae yuko hatarini kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada, na Daktari Y ambae anakuja kazini huku akiwa na uhakika na mahitaji yake ya msingi, nani ambae ana uwezekano mkubwa zaidi wa kuongea na wagonjwa kwa hasira na kukosa umakini?
Wala its not a suprise kuwa madaktari na watoa huduma wa hospitali za serikali wanakua na hasira zaidi na kukosa umakini.
Hornet
 
Back
Top Bottom