Hosipitali zetu zinakasoro gani mpaka hawa watoto kupelekwa marekani?

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
Kitendo cha kupelekwa marekani kwa watoto watatu walionusurika kwenye ajali binafsi kimenisikitisha sana, kwani ni dhahiri kuwa hosipitali zetu zina kasoro, na kama ikimtokea mtu ambaye hana connection basi ndiyo anapoteza maisha kwa upande wangu naongea kwa ushahidi kuwa hili ni aibu kwa taifa tena ilibidi lingefanyika kwa kificho nashangaa viongozi wanajichukulia kiki kwenye swala la aibu kama hili ambalo limedhirisha kuwa hatuna wataalamu ama vifaa mahususi kwa matibabu. nimepata hasira sana na ukija na comment yako ya kipumbavu napasua hii tablet.
 
1st to reply,,,,uwezo wetu upo chini,hatuna vifaaa maana hata vifaa vikiletwa hua wanavikorokocha makusud ili wagonjwa waende kwa hospital za washkaji zao,,so hawa wanakwenda kupata matibau haswa,sio bla bla kama hapa
 
Duh, hilo nalo ni swali?ni sawa sawa ukauliza, hivi Tanzania ni nchi masikini? Iko wazi sana mkuu, siyo tu hospitali zetu zina kasoro gani bali hospitali zetu ni hatari kwa afya ya mgonjwa. Mtu aliyeumia unampeleka hospitali zetu uku ukiwa unalia, unawasiwasi pengine angeweza kupona kabla ya kwenda kwenye hizo hospitali.
 
Kitendo cha kupelekwa marekani kwa watoto watatu walionusurika kwenye ajali binafsi kimenisikitisha sana, kwani ni dhahiri kuwa hosipitali zetu zina kasoro, na kama ikimtokea mtu ambaye hana connection basi ndiyo anapoteza maisha kwa upande wangu naongea kwa ushahidi kuwa hili ni aibu kwa taifa tena ilibidi lingefanyika kwa kificho nashangaa viongozi wanajichukulia kiki kwenye swala la aibu kama hili ambalo limedhirisha kuwa hatuna wataalamu ama vifaa mahususi kwa matibabu. nimepata hasira sana na ukija na comment yako ya kipumbavu napasua hii tablet.
Turiwapereka watoto Marekani wariopata ajari kure Arusha tunajari wananchi wetu.
 
Baadae mtaambiwa gharama za matibabu na usafirishaji wa hao majeruhi zinatosha kujenga hospitali ya wilaya! Hapo kutakuwa na wakubwa watakaofaidika na hili zoezi.
 
Hospitali zetu hazina uwezo wa kuweza kutatua matatizo kama haya . hili ni janga kwasababu ikitokea mtu ambaye hana connection kama hao watoto maana yake lazima upoteze maisha
 
Kitendo cha kupelekwa marekani kwa watoto watatu walionusurika kwenye ajali binafsi kimenisikitisha sana, kwani ni dhahiri kuwa hosipitali zetu zina kasoro, na kama ikimtokea mtu ambaye hana connection basi ndiyo anapoteza maisha kwa upande wangu naongea kwa ushahidi kuwa hili ni aibu kwa taifa tena ilibidi lingefanyika kwa kificho nashangaa viongozi wanajichukulia kiki kwenye swala la aibu kama hili ambalo limedhirisha kuwa hatuna wataalamu ama vifaa mahususi kwa matibabu. nimepata hasira sana na ukija na comment yako ya kipumbavu napasua hii tablet.
Mkuu mbona hukuuliza swali hili wakati wa kikombe cha babu wa loliondo!
 
Back
Top Bottom