Hoseah agoma kuzungumzia uchunguzi wa mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoseah agoma kuzungumzia uchunguzi wa mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Aug 23, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema imefunga mjadala kuhusu suala la mawaziri waliokuwa wakiwachunguzwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na wengine kushindwa kuwajibika na kuisababishia serikali hasara, hali iliyomlazimisha Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa na kuunda upya Baraza la Mawaziri.

  Akizungumza na NIPASHE, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, alisema kwa sasa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa alishasema kuwa wanachunguzwa. “Kwa sasa suala hilo tumefunga mjadala, hatuwezi kulizungumzia tena tulishasema tunawachunguza basi,” alisema Dk. Hoseah

  Ripoti ya kamati za kudumu za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Augustine Mrema, ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na John Cheyo na kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira inayoongozwa na James Lembeli zilizua mjadala mkubwa bungeni na kutajwa kwa baadhi ya mawaziri kuwa ni wabadhirifu. Miongoni mwa waliotajwa ni pamoja aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye anadaiwa kuhusika katika ubadhirifu wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).

  Pia aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, aliyetajwa kuhusika katika kumkingia kifua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango la Taifa (TBS), Charles Ekelege, kutokana na kusema uongo katika kazi ya ukaguzi wa magari nje ya nchi.

  Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, naye alidaiwa kushindwa kusimamia matumizi bora ya fedha za umma kiasi cha kuruhusu nyumba yake kukarabatiwa kwa mamilioni ya fedha.

  Wengine katika sakata hilo ni aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), ambaye sasa amehamishiwa Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, ambaye anadaiwa kushindwa kusimamia fedha katika halmashauri mbalimbali nchini ambako ufisadi wa kiwango kikubwa uligundulika.

  Pia yupo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, anayetuhumiwa kwa kushindwa kusimamia sekta ya madini na umeme, kuweko kwa manunuzi makubwa ya mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL ambayo yameongezwa bei. Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alituhumiwa kushindwa kudhibiti ubadhirifu katika wizara yake kama ulivyobainika katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii na usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi.
  CHANZO: NIPASHE

   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  sheria haimruhusu!
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu kila akiwataja mafisadi serekali haichukui hatuo zozote si bora akaushe 2

  ngoja nikate kei na mbege
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Huo ni uamuzi sahihi kabisa, maana Jaji werema alikataa kubadilisha sheria itakayowapa TAKUKURU nguvu za kisheria za kuwakabili wabadhilifu/Mafisadi. Jaji Werema (AG) amefanya makusudi ili awalinde watuhumiwa wa UFISADI ambao wengi ni watumishi wa ngazi za juu serikalini.
   
Loading...