Hosea: Ole wenu mafisadi wa siasa

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
BAADA ya baadhi ya wadau wa siasa kuikejeli Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwamba haiwezi kudhibiti ufisadi kwenye uchaguzi, Mkurugenzi wake Mkuu Dk Edward Hoseah, ametoa onyo akisema watu wanaotarajia kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wasithubutu kutumia rushwa kwa ajili ya kuwashawishi wananchi kuwachagua kwani watashughulikiwa kikamilifu.

Kauli ya Dk Hoseah inakuja kipindi kifupi baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuikabidhi rungu kwa kuitaka kuwashughulikia wote watakaotumia fedha kwa ajili kununua au kuuza kura, huku akitumia salamu zake za mwezi kuuelezea kwa kina Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi akisema ni kitanzi kwa waovu hao.


Dk Hoseah akionyesha kuanza kutekeleza amri ya Rais na sheria, alionya: "Ole wenu mnaogawa baiskeli na pikipiki katika maeneo mbalimbali kwani kuna baadhi ya watu wameanza kupita pita huko kwa kuwarubuni wananchi ili waweze kuwachagua katika Uchaguzi Mkuu ujao,... sisi tumejipanga kutekeleza agizo la Rais (Jakaya) Kikwete bila kumwonea mtu aibu kwani hii si nguvu ya soda kama wengine wanavyodhani."


Dk Hoseah akitangaza kiama cha mafisadi kutekeleza amri ya mkuu wake wa kazi kwa mafisadi hao wa uchaguzi, tayari joto la uchaguzi limezidi kupanda huku baadhi ya makada ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiweka bayana kwamba, bila rushwa chama hicho hakiwezi kushinda.


Lakini, Dk Hoseah ambaye taasisi yake ina dhamana ya kushughulikia makosa yote makubwa ya ufisadi na madogo, jana alitilia mkazo kauli ya Rais wakati akifungua jengo la kisasa la Wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga, ambako alitoa onyo pia akisema chombo hicho nyeti hakifanyi kazi sawa na nguvu ya soda.


Dk Hoseah ambaye uongozi wake katika Takukuru ulichafuka hasa baada ya ripoti ya taasisi hiyo kusafisha mkataba wa Kampuni ya Richmond Development (LLC), alionekana kutaka kufa na mtu baada ya kuweka bayana kwamba, wananchi wasirubuniwe kwa kununuliwa kwa chumvi, sukari na khanga, ili waweze kumchagua mgombea yoyote katika nafasi ya kuwawakilisha kwani kwa kufanya hivyo ndiyo maana kila siku wanalia wimbo wa ufisadi.


“Watanzania wenzangu mwaka huu ni wa uchaguzi, tusikubali kununuliwa ili kumchagua mtu, kwani kwa kufanya hivyo tutapata viongozi wasiofaa na ndicho chanzo cha kulia kila siku wimbo wa ufisadi,”alisisitiza Dk Hoseah.


Awali, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Leonarda Ngaiza alisema kufunguliwa kwa jengo hilo kunawapatia faraja kwani wanafanya kazi zao kwa ufanisi kuliko ilivyokuwa hapo mwanzo kwani ofisi hiyo ilikuwa mtaani na hivyo wananchi kushindwa kuifikia kwa uhuru zaidi.


Jengo hilo la ofisi hiyo ambalo ni la ghorofa moja limetumia kiasi cha fedha Sh 742,288,634 ni miongoni mwa majengo matatu yaliyojengwa Mwaka jana mengine yako Mkoa wa Lindi na Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.


Katika siku za karibuni, Rais Kikwete amekuwa akiitaka Takukuru kushughulikia wote wanaotoa na kupokea rushwa wakati wa uchaguzi huku akiwa mstari wa mbele kuhakikisha muswada wa gharama za uchaguzi unakamilika na kuanza kutumika kabla ya uchaguzi.
 
Huyu si amewahi kusema mafisadi wale Christmas kwanza and they did, tht's 2008 wakala pia na 2009 na wataila pia hii ya 2010. Does he think anybody takes him serious?
 
Tumezoea kusikia mwimbo na ngonjera hizi hizi na wakati umefika na kusema no kwa namna ya watu kama hawa
 
Kwanza yeye mwenyewe alitakiwa awe segerea mida hii bahati yake yuko Tanzania nchi ya amani na upendo angekuwa nchi zenye viongozi wenye uchungu na nchi yao story ingekuwa si hii
 
Mimi bado narudi tena tatizo ni mfumo wa utawala katika Tanzania na hasa katiba na kutokuwa na mfumo imara wa vyama vya siasa na hivyo hivyo tunazaa Serikali dhaifu na watu dhaifu na vice versa yake
 
Ningekuwa mkuu wa chuo kilichomtunuku PhD Hosea, ningeiomba Senate yangu imvue degree zote tatu huyu "Dr. Ozea"!!

He failed to deliver right from d1, naamini ingekuwa enzi za kiongozi wetu shupavu Mwl. Nyerere (Mungu amlaze mahali pema Mzalengo wetu), mtu kama huyu tungesha mstaafisha kwa manufaa ya umma!!
 
Ningekuwa mkuu wa chuo kilichomtunuku PhD Hosea, ningeiomba Senate yangu imvue degree zote tatu huyu "Dr. Ozea"!!

He failed to deliver right from d1, naamini ingekuwa enzi za kiongozi wetu shupavu Mwl. Nyerere (Mungu amlaze mahali pema Mzalengo wetu), mtu kama huyu tungesha mstaafisha kwa manufaa ya umma!!
Alisoma PhD yale ya sheria UDSM na wale wakongwe wa sheria ndio hapo UDSM hivyo ndio alikosoma hiyo PhD yake
 
Naona ingekuwa busara sasa baadhi ya hizi nafasi za juu za vyombo nyeti vya serikali, baada ya uteuzi wa Rais, wahusika waidhinishwe na bunge.
Huyu jamaa naye ni mpiga story mwingine Tanzania iliyowahi kumtengeneza. Kazi kama hizi sio za kujitangaza tangaza kwenye media kwa maneno. Ni kwa idadi ya vitu ambavyo umevifanya.
 
Sasa hizi Phd za UDSM ni political!
Nchimbi akipata Phd Mzumbe,atakuwa sambamba na akina Magufuli ,Hosea etc.
 
Kweli Tanzania tunajua kupeana uongozi. Hata kama mtu una shit everywhere watu hawasikii kinyaa wamo tu na wewe till death do us apart.
 
Alisoma PhD yale ya sheria UDSM na wale wakongwe wa sheria ndio hapo UDSM hivyo ndio alikosoma hiyo PhD yake

Josh hainishangazi kama Hosea kapata PhD yake UDSM, si unajua hata mkuu wa chuo pale ni nani? Ni yuleyule aliyeiboronga Tanesco (Chairman wa bodi ya Tanesco) na VC wake ndo best Chanda na pete na Mkuu wa kaya, unategemea nini hapo???????

Ni ushikaji kwenda mbele......
 
Serikali hii ya Kikwete na chama anachokiongoza hawana dhamira ya kuthibiti rushwa katika jamii ya Tanzania; wangekuwa na dhamila ya kweli ya kutokomeza hiyo rushwa wanayoisema huyu Hosea sio mtu wa kuongoza mapambano hayo!! Nasema huyu Hosea sio mtu mwenye dhamira ya kupambana na kutokomeza rushwa kwasabababu anapata amri ya nini cha kufanya kutoka Ikulu, kwahiyo wale wote watakaokamatwa ni wale ambao Ikulu inataka wakamatwe na wengi wao watakuwa ni wapinzani wa utawala uliopo irrespective of their political Affiliation na wengi wao watakuwa watoaji na wapokeaji rushwa ndogo ndogo na sio zile KUBWA!. Kwasababu hiyo hiyo ya kupokea amri kutoka Ikulu ya jinsi ya kufanya kazi zao ,huyu Hosea na team yake, ukamataji wao wala rushwa na mafisadi utaishia kwenye geti la Ikulu; wale wala rushwa kubwa kubwa ambao wako ndani ya uzio wa Ikulu hawawezi kuwagusa, na kwasababu hizo nasema Takukuru ya sasa kwa muundo wake hawawezi kupambana na rushwa ya aina yeyote ile kikwelikweli!!
 
Josh hainishangazi kama Hosea kapata PhD yake UDSM, si unajua hata mkuu wa chuo pale ni nani? Ni yuleyule aliyeiboronga Tanesco (Chairman wa bodi ya Tanesco) na VC wake ndo best Chanda na pete na Mkuu wa kaya, unategemea nini hapo???????

Ni ushikaji kwenda mbele......
Ni kweli kabisa na pia kama ndio hivyo basi kuna umuhimu sana wa kufanya mabadiliko haraka sana na pia itakuwa faida kubwa sana katika Taifa letu na hivyo hawa wanasiasa wetu wameshindwa kazi
 
Huyu si amewahi kusema mafisadi wale Christmas kwanza and they did, tht's 2008 wakala pia na 2009 na wataila pia hii ya 2010. Does he think anybody takes him serious?

X-mas azija isha bado mpka yesu arudi ndio zitaisha, Pili si huwa wanakula wote hiyo x mas then Boxing day huwa anaenda kucheki salio New Jersy.
 
Huyu hana jipya la kutueleza wakati wa kashfa ya Tanesco alisema kuwa mkataba ulikuwa halali kabla ya kulindwa na vigogo ambao walimsafisha vile vile. Kashfa kubwa ameshindwa kuzifuatilia!
 
Hosea na bla bla bla zake. Hii ni nchi ya maneno na maneno zaid.
Najiuliza sana, hawa jamaa akili zao zikoje? Wanaongea ongea tu. Wana ahidi ahidi tu na hawatendi. Au sababu ni kwamba watu wengi hajui siasa na wanaamim chochote wasikiacho kutoka kwa wanasiasa.Hosea, just suprise us. Acha ahadi. We will love suprises than promoses. Tumechoka ahadi. Zimekua nyingi mna hadi we have lost tract ni kitu gani wewe na boss mulituahidi a month ago. Pls
 
Ningekuwa na uwezo fulani ningewakusanya hawa wote wanaokuja na "maonyo" yao na kuwapeleka kwenye genge kubwa na refu na mmoja ningeanza kuwasukumiza chini. Yeyote aliyewahi kutoa maonyo kwa wahalifu angerushwa toka kwenye genge hilo huku amening'inizwa kamba shingoni.
 
Ningekuwa na uwezo fulani ningewakusanya hawa wote wanaokuja na "maonyo" yao na kuwapeleka kwenye genge kubwa na refu na mmoja ningeanza kuwasukumiza chini. Yeyote aliyewahi kutoa maonyo kwa wahalifu angerushwa toka kwenye genge hilo huku amening'inizwa kamba shingoni.
Kwanini tena Babu, Tena umebadili avastar yako. duh sasa mimi naona afadhali ile ya kwanza tu maana hii sasa hivi sio nzuri sana,
 
SILENT CORRUPTION Hosea reacts

oseahreact.jpg

Edward Hosea

By Sunday Citizen Team

Ongoing public sector reforms should focus on Wrld Bank report' Tanzania's anti-corruption tsar Edward Hosea says serious acts of omission, executed quietly and usually unnoticed by most people, occupy the biggest corruption space in the country.


Dr Hosea told the Sunday Citizen that up to 80 per cent of acts of corruption against the nation are those best described as `silent' while the other 20 per cent comprise cases of outright bribery or pilfering by those in positions of authority.

According to the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Director General, `silent' acts of corruption do not attract public scrutiny and anger, despite their serious effect on the lives of millions of people.

Dr Hosea, whose office is one of the most sensitive and most watched over in the war on corruption, was commenting on a new World Bank report that has highlighted the huge price paid for ignoring the consequences of simple acts as absenteeism by teachers, unqualified health personnel or even the provision of substandard farm inputs.

The report was issued this week as part of the World Bank's periodic releases on the African Development Index (ADI). This year's report zeroed in on the problem of public servants who fail to deliver goods or services paid for by governments that, it said, was widespread across Africa.

Dr Hosea said he agreed with the findings of the World Bank, adding that the ongoing public sector reform programmes should focus on such issues because of the inherent benefits.

The PCCB boss, who was recently in the news sparring with Parliament when his bureau launched investigations into alleged double payment of allowances to MPs, added that the problem of silent corruption was caused by either incompetence, negligence or sheer ignorance.

A Cabinet minister also readily admitted that there was failure to act on the vice even though it was widespread.

"For sure, you will notice civil servants earning a lot of money through that kind of corruption... but the ministry to answer queries on this one is that of Good Governance; this issue is really about good governance," said Philip Marmo, the Minister of State, Office of the prime Minister, (Policy, Co-ordination and Parliamentary Affairs).

Marmo said failure by public servants to deliver services or inputs paid for by the government could not be denied, and added that it was a major area that has not been fully addressed.

He said, for instance, that it has been a routine for civil servants to attend workshops, seminars and conferences rather than provide services to wananchi as stipulated in the public service code.

The minister for public service management, Ms Hawa Ghasia, could not be reached for comment and her permanent secretary, Mr George Yambesi, said he could not respond before reading the `silent corruption' report.

Meanwhile, several civil society officials and a politician were among those who acknowledged the threats of silent corruption to public good and development. They said this form of graft was to blame for the low productivity Tanzanians notice in most public offices.

The Executive Director of ForDIA, a NGO advocating development Initiatives, Mr Bubelwa Kaiza, said public offices had no clear-cut evaluation system to gauge their output.

Mr Kaiza said there was a need for the government to look into ways of at paying its employees as per each individual's performance.
"Due to lack of such a system, accountability is almost non-existent and everyone is doing what they want," said Mr Kaiza.

The Executive Director of Development Concern (DeCo), Mr Robert Nyampiga, said the World Bank report was timely and spot-on as regards the real rot in Tanzania's public service.

"In most cases people take a long time waiting for services in public offices, even when it would have been possible for one to be served immediately," he said, adding that his explains why the government is always blamed for inefficiency.

A lecturer of the University of Dar es Salaam, Mr John Jingu, said silent corruption could be equated to fraud. He said the money lost by paying for undelivered services runs into billions of shillings. NCCR Mageuzi Chairman James Mbatia said lack of ethics, accountability, integrity and poor governance principles were a major cause of silent corruption in Tanzania.

Mr Mbatia said public mindset was another contributing factor. He said authorities played a role by hiring people without bothering much to verify competencies.

According to the report, "quiet corruption, although smaller in monetary terms, is particularly harmful to the poor, who are more vulnerable and more reliant on government services and public systems to satisfy their most basic needs".

The term "quiet corruption" represents various types of malpractices of frontline service providers teachers, doctors, inspectors and other government representatives but does not involve monetary exchange.

The most common examples cited in the latest World Bank report on social and economic conditions across the continent are absentee teachers in public schools and absentee doctors in primary health clinics.

Others include drugs being stolen from public health facilities and sold in the private market as well as subsidised fertiliser being diluted before it reaches farmers.

According to the report, findings indicate that primary school teachers in a number of African countries, including Tanzania, abscond from their stations for 15 to 25 per cent of the time, but, in addition, a considerable fraction of those in school don't even teach.

The Bank's report also cites high absentee rates of health-care workers, with a number of studies suggesting that quality and effort on the job are very low. In Tanzania, the report found that health provision competence is considerably poor, notably in the rural areas.

A survey of malaria deaths in rural Tanzania established that nearly four out of the five children who died had sought treatment in hospitals. It says the absence of diagnostic equipment, drug thefts, provider absenteeism and very low level of diagnostic effort are some of the manifestations of "quiet corruption" that have contributed to deaths.

"Quiet corruption does not make the headlines the way bribery scandals do, but it is just as corrosive to societies," said Dr Shanta Devarajan, the chief economist for the World Bank's Africa Region.

"Tackling `quiet corruption' will require a combination of strong and committed leadership, policies and institutions at the sectoral level, and most important increased accountability and participation by citizens."

The World Bank report has focused on "quiet corruption" in this year's ADI to serve as a tool for Africans to hold their governments accountable.


Reported by Mkinga Mkinga, Bernard Lugongo, Beatus Kagashe and Frank Kimboy.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom