Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
BAADA ya baadhi ya wadau wa siasa kuikejeli Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwamba haiwezi kudhibiti ufisadi kwenye uchaguzi, Mkurugenzi wake Mkuu Dk Edward Hoseah, ametoa onyo akisema watu wanaotarajia kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wasithubutu kutumia rushwa kwa ajili ya kuwashawishi wananchi kuwachagua kwani watashughulikiwa kikamilifu.
Kauli ya Dk Hoseah inakuja kipindi kifupi baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuikabidhi rungu kwa kuitaka kuwashughulikia wote watakaotumia fedha kwa ajili kununua au kuuza kura, huku akitumia salamu zake za mwezi kuuelezea kwa kina Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi akisema ni kitanzi kwa waovu hao.
Dk Hoseah akionyesha kuanza kutekeleza amri ya Rais na sheria, alionya: "Ole wenu mnaogawa baiskeli na pikipiki katika maeneo mbalimbali kwani kuna baadhi ya watu wameanza kupita pita huko kwa kuwarubuni wananchi ili waweze kuwachagua katika Uchaguzi Mkuu ujao,... sisi tumejipanga kutekeleza agizo la Rais (Jakaya) Kikwete bila kumwonea mtu aibu kwani hii si nguvu ya soda kama wengine wanavyodhani."
Dk Hoseah akitangaza kiama cha mafisadi kutekeleza amri ya mkuu wake wa kazi kwa mafisadi hao wa uchaguzi, tayari joto la uchaguzi limezidi kupanda huku baadhi ya makada ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiweka bayana kwamba, bila rushwa chama hicho hakiwezi kushinda.
Lakini, Dk Hoseah ambaye taasisi yake ina dhamana ya kushughulikia makosa yote makubwa ya ufisadi na madogo, jana alitilia mkazo kauli ya Rais wakati akifungua jengo la kisasa la Wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga, ambako alitoa onyo pia akisema chombo hicho nyeti hakifanyi kazi sawa na nguvu ya soda.
Dk Hoseah ambaye uongozi wake katika Takukuru ulichafuka hasa baada ya ripoti ya taasisi hiyo kusafisha mkataba wa Kampuni ya Richmond Development (LLC), alionekana kutaka kufa na mtu baada ya kuweka bayana kwamba, wananchi wasirubuniwe kwa kununuliwa kwa chumvi, sukari na khanga, ili waweze kumchagua mgombea yoyote katika nafasi ya kuwawakilisha kwani kwa kufanya hivyo ndiyo maana kila siku wanalia wimbo wa ufisadi.
“Watanzania wenzangu mwaka huu ni wa uchaguzi, tusikubali kununuliwa ili kumchagua mtu, kwani kwa kufanya hivyo tutapata viongozi wasiofaa na ndicho chanzo cha kulia kila siku wimbo wa ufisadi,â€alisisitiza Dk Hoseah.
Awali, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Leonarda Ngaiza alisema kufunguliwa kwa jengo hilo kunawapatia faraja kwani wanafanya kazi zao kwa ufanisi kuliko ilivyokuwa hapo mwanzo kwani ofisi hiyo ilikuwa mtaani na hivyo wananchi kushindwa kuifikia kwa uhuru zaidi.
Jengo hilo la ofisi hiyo ambalo ni la ghorofa moja limetumia kiasi cha fedha Sh 742,288,634 ni miongoni mwa majengo matatu yaliyojengwa Mwaka jana mengine yako Mkoa wa Lindi na Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Katika siku za karibuni, Rais Kikwete amekuwa akiitaka Takukuru kushughulikia wote wanaotoa na kupokea rushwa wakati wa uchaguzi huku akiwa mstari wa mbele kuhakikisha muswada wa gharama za uchaguzi unakamilika na kuanza kutumika kabla ya uchaguzi.