Hosea ameathiri maisha yangu na familia yangu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hosea ameathiri maisha yangu na familia yangu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtimti, Sep 21, 2008.

 1. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 912
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  [​IMG]
  aliyekuwa mhariri wa family mirror, bwana Musendo

  Ilikuwa siku, wiki mwezi na miezi na hatimaye miaka mitatu na miezi kadhaa ilikwisha, Zephania Musendo alijikuta kuwa mtu huru tena juzi baada ya kumaliza adhabu yake ya kutumikia kifungo cha miaka mitano. Aliachiwa huru kutoka Gereza la Mkuza lililo Kibaha mkoani Pwani.

  Musendo ni mwandishi mwandamizi ambaye amepitia vyombo mbalimbali vya habari, mara ya mwisho akiwa analiongoza Gazeti la Family Mirror akiwa mhariri mkuu.Lakini bidii yake ya kazi na ujuzi aliokuwa nao ulizimwa ghafla baada ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu kumhukumu kifungo cha miaka mitanojela kwa madai ya kula rushwa ya Sh 100,000 baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCB) kumshtaki.“Imeathiri sana maisha yangu, imeharibu familia yangu na nimepata hasara kwani kipato kimesimama kwa muda wote na mipango yangu imeparaganyika,” anasema Musendo katika mahojiano maalum na Gazeti la Mwananchi jana.

  Musendo, ambaye kwa sasa ameungana na familia yake nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam, anasema kuwa mipango yake kwa sasa ni kujiweka sawa, na kama akipata kazi atashukuru ili aweze kuisaidia tena familia yake akiwa kichwa cha familia.Lakini anapokumbuka kusimama ghafla kwa maisha yake, Musendo anaongea kwa masikitiko.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu ilimuona Musendo kuwa ana hatia ya kupokea rushwa ya shilingi 100,000, lakini katika mazungumzo na Mwananchi, kama alivyojieleza mahakamani, Musendo anazidi kusisitiza kuwa hakupokea rushwa na kukamatwa kwake kulikuwa ni njama za kumzima asitekeleza wajibu wake."Yote haya yalinipata baada ya Family Mirror kuandika tuhuma za rushwa ndani ya PCB na kumhusisha kiongozi mwandamizi, Edward Hosea ambaye kwa kipindi hicho alikuwa Mkurugenzi wa Operesheni," anasimulia.

  "Kulikuwa na taarifa kuwa Hosea anajihusisha na masuala ya rushwa, na aliagiza mwandishi wake ili kuweza kufuatilia hilo na kuthibitisha hata ndani ya taasisi hiyo. “Mwandishi alikwenda na hata (mkurugenzi wa PCB, Anatory) Kamazima alithibitisha kusikia tuhuma hizo. Hivyo tukawa tunazifanyia kazi.”

  Kwa maoni yake, Musendo anaona kuwa kutokana na habari hiyo, Hosea (sasa ni Mkurugenzi wa PCCB) aliamua kumwadhibu na kwamba, alifanikiwa kwani mahakama ilimuona kuwa ana hatia na akakaa jela kwa miaka yote mitatu."Kutumikia kifungo kwa miaka yote mitatu si mchezo," alisema.

  "Sikuwahi kukutana na Hosea hata siku moja. Alikuwa akifanya jitihada ili niweze kuonana naye." Anasema Hosea, alimtumia mwandishi mwingine ili amfuate waweze kuonana naye. Anasema baada ya kukutana Sheraton waliongea mambo mbalimbali na Hosea alimsihi kuwa habari hiyo isitumike, (wakati huo ilikuwa bado haijaandikwa) na kudai kuwa ilikuwa ni njama za baadhi ya watu ili asipate cheo cha juu cha taasisi hiyo.“

  Aliniambia kuwa mambo yote hayo yalikuwa majungu, na kuwa wakati huo bosi wake alikuwa anatarajia kustaafu hivyo watu walikuwa wakitaka asipate nafasi ya ukurugenzi. Mimi nilimjibu kuwa tutatuma mwandishi ikithibitika tungeitoa,” anasema. Musendo anaeleza kuwa baada ya habari kutoka Hosea alimtafuta tena na kutaka wakutane Sheraton tena ili wazungumze na alitaka kuwa wakutane saa 10:00 jioni, naye alitimiza hilo kwa kuitikia wito.

  Hata hivyo, anasema kuwa ilipofika saa 11:00 aliamua kuondoka hotelini hapo kwa gari la ofisini ili arejee kazini kwake kuendelea na shughuli nyingine.“Nilipofika pale Red Cross Hosea akanipigia na kuomba radhi kuwa alikuwa amechelewa kidogo na kuwa kwa muda huo alikuwa ameshafika pale hotelini, nilimwamuru dereva turudi na nikakutana naye mlangoni. “Nilipofika ndani tukatoka na kukaa nyuma kwenye bustani, akanieleza kuwa aniagizie bia lakini mimi sikutaka kunywa bia nikaagiza soda yeye akawa anakunywa chai.

  "Tulizungumza kwa muda na ghafla Hosea alinyanyuka na kulikuwa na watu kama sita walioingia na kuzunguka meza yetu na mmoja alimwingiza mkono mfukoni. “Wakaniambia nitulie nisifanye vurugu yoyote na kuwa walikuwa wanashuku nimepokea rushwa, wakaniamuru nitoe vitu vyote mfukoni na mimi nilitelekeza kwa kutoa kila kitu pamoja na pesa nilizokuwa nazo."Anasema baada ya kuweka mezani walikagua na kuweka pembeni baadhi ya pesa na kusema kuwa alikuwa na pesa zao kiasi cha Sh100,000 na hivyo aliamriwa kuwa yuko chini ya ulinzi. Baada ya hapo akasema kuwa walimchukua na kutoka naye nje wakidai kuwa na mahojiano zaidi.

  “Tulipofika nje nikawaomba nimtaarifu dereva wangu ili arudi ofisini, lakini hawakukubali na waliondoka na mimi hadi polisi Oysterbay ambako nililala huko," anasema.

  “Pia nilisikia kuwa hata dereva wangu alikamatwa baadaye na yeye alilala Central Police kwa kosa la uzururaji nadhani.”Anasema kwa mlolongo huo wa matukio alijua kabisa kuwa hawa watu hawakuwa na nia njema naye na mpango huo ulikuwa kumkomoa, kwani dereva hakuwa na kosa lolote.

  "Kesho yake nilipata dhamana na wakaniambia kuwa siku inayofuata niripoti ili nifikishwe mahakamani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa."Tulipofika mahakamani nilitakiwa kuwekewa dhamana ya Sh500,000 taslim na kwa kuwa ofisini walikuwa wanashughulikia hilo, hawakusubiri na kunipeleka Keko ambako nililala kwa siku tano kabla ya dhamana kukamilishwa," anasema.

  Anaeleza kuwa kesi iliendeshwa kutoka mwaka 2003 na ilipofika Mei 17 2005 alihukumiwa kifungo hicho ambacho haamini kama ilikuwa halali kwa sababu alijaribu kuweka mambo yote hadharani, ikashindikana."Lakini namshukuru Mungu nimetoka," anasema

  BAADA ya hakimu Suma Seme kutamka kuwa amehukumiwa kwenda jela miaka mitano, Zephania Musendo anasema hakuamini macho yake! na alipata mshtuko mkubwa kwani hakutarajia kuwa angefungwa kutokana na imani yake kuwa mkasa mzima ulikuwa wa kutengeneza.

  Hakuamini, lakini alilazimika kukubali matokeo ya hukumu hiyo iliyotolewa asubuhi ya Mei 17, 2005."Sikuamini na hata mke wangu Paschalia na ndugu zake hawakuamini na nikawaona wanaangua kilio," anasema.

  Hali ilikuwa hivyo kwa mkewe.“Sikuamini kwa kuwa nilijua sasa anaenda jela na sitakuwa naye tena,” anasema mkewe. “Mpaka alipotolewa chumba cha mahakama na kuwekwa lock up (rumande) ya pale mahakamani na maaskari wakaniambia kuwa ‘huyu si wenu tena, ni wa kwetu’.

  Roho iliniuma sana, nikamshukuru Mungu.”Baada ya kutolewa hukumu hiyo, Musendo anasema alichukuliwa na kupelekwa katika gereza la Keko jijini Dar es Salaam, ambako alianza kutumikia kifungo hicho na maisha mapya ya jela.

  “Tulipofika pale gerezani, wana utaratibu wa watu kupekuliwa hasa wafungwa wapya, kwa hivyo tulivuliwa nguo zote kwa ajili ya upekuzi,” anasema.Anaeleza kuwa kitendo cha kuvuliwa nguo zote mbele ya wafungwa wengine ndicho kilikaribisha maumivu mengine kwani kuna baadhi ya wafungwa aliokuwa nao walikuwa na umri wa watoto wake, lakini hakuwa na uhuru tena, ilimlazimu kufuata amri.

  “Maisha ya Keko yalikuwa ni ya msongamano na niliona mambo mengi yanayohusu wafungwa, mbayo nilikuwa nasikia sikia tu, lakini nilikuja kuamini kuwa ilikuwa ni kweli”.

  Katika jela ya Keko, alikaa kwa muda wa mwezi mmoja inagawa kulikuwa na msongamano wa watu lakini kulikuwa na matandiko mazuri na walilala kwa kujipanga ili kuweza kutosha katika chumba kidogo.Baadaye alihamishiwa jela ya Mkuza, iliyoko Kibaha mkoani Pwani, ambako kwa maoni yake kuna tofauti kubwa na jela ya Keko, kwani haina ngome kubwa kama ilivyo kwa jela nyingine kubwa, Magodoro yamekwisha na hali si nzuri sana.

  “Kuna wakati roho inauma kwani tokea magodoro yaletwe mara ya kwanza hayajabadilishwa na vimebakia vipande vidogo ambavyo mtu unavikusanya na kuunganisha mpaka upate sehemu ya kulala.”

  Musendo anasimulia kuwa alipofika jela alikutana na watu wengi ,wakiwamo majambazi, vibaka na wengine ambao wamefungwa kwa mashtaka ya uhalifu au kesi za kusingiziwa na kubambikwa, lakini wote walikuwa wakitumikia vifungo vyao.

  Anasema kuwa chakula jela kilikuwa cha kawaida, kwani walikuwa wakila ugali na maharage kila siku, isipokuwa Jumamosi walipokuwa wakila wali na maharage wakati Jumapili kulikuwa na nyama.

  “Kwenye chakula ndio hivyo tena, unaweza kukutana na wadudu katika maharage au unga, utakula tu utafanyaje?”Kutokana na kuwa na matatizo ya kiafya hasa kwa magonjwa wa moyo na kisukari ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu kabla ya kufungwa, alilazimika kuomba kupatiwa chakula maalum (special diet), lakini ilishindikana kwani aliambiwa kuwa jela hiyo haikuwa na utaratibu kama huo.

  “Mkuu wa Gereza alinieleza kuwa hakukuwa na special diet hivyo aliniruhusu kama ndugu zangu wangeweza kuniletea sawa, kwa hivyo nikawa naletewa samaki, matunda na karanga kwa muda fulani.”

  Kuhusu maziwa mbayo aliomba, aliambiwa kuwa kwa kuwa ng’ombe wa gereza walikuwapo angetakiwa kulipiwa bili na ndugu zake na hivyo gereza kumpatia.

  “Lakini baadaye Bwana Jela alinionea huruma kwa kujua kuwa mimi ndio nilikuwa kichwa cha familia wasingemudu kulipia kwa muda wote, akaamua nipewe bure, namshukuru sana.”
  Siku iliyomuumiza

  Akisimulia siku mbayo imemuumiza na kumfedhehesha alipokuwa jela, alisema kuna siku upekuzi wa kawaida katika gereza ulikuwa ukifanyika na wafungwa wote walitakiwa kuvua nguo zote na kuchuchumaa.

  “Tulitakiwa kuruka kichura, nilipojaribu kuruka na hii hali yangu (ya ugonjwa) nilidondoka chini.

  Nilitarajia kuwa mtu wa kwanza kunisaidia angekuwa daktari wa jela, ambaye alikuwepo sehemu hiyo. Lakini hakufanya lolote na niliachwa nikigalagala chini.”“Roho iliniuma sana kwa kuwa Bwana Jela pia hakujali bali alisema hakuna taabu na kuwa mimi nilikuwa nazuga tu”.Anasema, alifikiria pale alipokuwa amelala akiwa uchi, kila mtu alikuwa akimwangalia, na kwa kuwa gereza hilo halikuwa na ukuta, basi hata watu wakiwamo wanafamilia wa askari waliweza kumwona.

  “Sitasahau siku hiyo kamwe.”

  Maisha ya dini gerezani
  Musendo anasema, kwa kawaida walikuwa wakiamka mapema asubuhi ili kupeana nafasi ya kuabudu ndani ya seli zao, “Kwanza tulikuwa tunawapisha Waislamu ambao walikuwa wananza sala zao mapema saa 11 alfajiri.

  Baadaye tunakuja Wakristo na kulikuwa na watu waliokuwa wanatuongoza”. Anasema pamoja na kuwa watu walikuwa wakisali ndani ya seli hizo, bado kuna wengine kwa hiyari yao walikuwa hawaabudu na hawataki kabisa kusali.

  “Ingawa sikuwa mtu wa dini sana, lakini nilikuwa nasali kila siku na wenzangu na tulikuwa tunapeana masomo ya biblia. Pia kuna watu wa Sabato walikuwa wanakuja kufanya sala na kutugawia vitu mbalimbali kama sabuni, ndala, nguo na hata viatu.”

  Baada ya sala, Musendo anaeleza walikuwa wananatolewa nje na kuhesabiwa, na ulikuwa utaratibu wkawaida na baadaye walikunywa uji na kupangiwa majukumu, ikiwamo kutafuta kuni, kwenda shambani, bustanini, kufyatua matofali na kazi nyingine za ndani ya gereza.

  Baada ya kutawanyika na kwenda maeneo ya majukumu, wote huendelea na kazi hadi saa nane mchana ambapo hurejeshwa gerezani kupata mlo wa mchana na baadaye saa 10 kufungiwa katika seli, kuhesabiwa na kuendelea na mambo mengine.

  “Wengine walikuwa wanapenda kucheza karata, ingawa sina hakika kama zinaruhusiwa na wengine walikuwa wanapiga ‘story’ na kuvuta sigara tukisubiri usiku ili siku ipite, ingawa tulikuwa tunafungiwa mapema lakini ilikuwa vigumu kulala saa 10 jioni.”

  Anaeleza kuwa cha kushangaza pamoja na kupekuliwa kwa uhakika lakini vitu mbalimbali visivyoruhusiwa vilikuwa vinapatika ndani ya jela, zikiwamo sigara na hata bangi, “Sijui ilikuwaje lakini nadhani kuna syndicate (njama) kubwa ya biashara hizo inawezekana inahusisha hata maaskari.

  ”Musendo anasema bahati yake nzuri aliheshimika sana, na watu walikuwa wakimpenda kwani alikuwa anajua vitu vingi, na hivyo kumfanya awe na mahusiano mazuri hadi kuwa kiongozi wa wafugwa (mnyampala) wa kuwasimamia wenzake.

  Lakini kuitu kilichokuwa kikimsumbua zaidi ni kuishi huko huku kijua kuwa mkewe hakuwa na kazi, na alikuwa na watoto watano wanaomtegemea. Hali hiyo ilimkera na kumsononesha, ingawa mkewe alijaribu kumweleza kuwa mambo yanaenda sawa kila alipomtembelea.

  Anasema hali hiyo ilimsononesha sana hadi siku moja walipotembelewa na watu wa Chama cha Kusaidia Wafungwa (International Prisoners Relief Organisation ) ambao misaada mbalimbali na kuwaahidi kuwa wanazisaidia hata familia za wafungwa.“Nilikuwa na taarifa kuwa mtoto wangu aliyekuwa kidato cha tatu, alikuwa amefukuzwa shule kwa kukosa ada na niliwaomba watu hao kama wangeweza kumsaidia ili arejee shule.

  Wakanieleza utaratibu, nikaandika barua, ikapitishwa na bwana jela lakini mpaka natoka jana sijajua ilikwamia wapi?, Lakini kikubwa nilifurahi kuona angalau kuna chama kama hicho cha kusaidia wafungwa, kwani wanahitaji msaada mno.”

  Musendo anasema pamoja na kutokea hivyo baadaye alimwandikia barua meneja wa benki na kumpatia mkewe, ili aruhusu pesa zitolewe kwenye akaunti yake ili isaidie ada ya mtoto.

  “Nashukuru sana meneja yule alielewa na mtoto alilipiwa.Kwa mujibu wa Musendo, kitu kilichomsumbua ni mwishoni wakati anakaribia kumaliza kifungo chake, “Unajua unapofungwa unaandikwa kifuani siku ya kuingia na siku ya kutoka.

  Sasa kadri siku zilivyokuwa zinakaribia kufika ndio ilikuwa kama ni mbali zaidi na maisha nayaona kama hayaendi.”Anasema anamshukuru Mungu siku hiyo ilifika wiki hii na pamoja na kuwa na matatizo ya maradhi yake, ametoka salama na alifurahi kuona mkewe na ndugu kadhaa wakiwa wamemfuata kumchukua.

  Alimshukuru Mungu na kuona kuwa ana kazi nzito ya kufanya na kuweka maisha yake sawa.

  “Kwa sasa ninajua nina majukumu mazito kwani kukaa jela miaka mitatu ,vitu vingi vinarudi nyuma, natamani nipate kazi kwanza na baadaye nikipata nafasi nitaandika kitabu kuhusu mambo ya jela hasa mateso wanayopata watu wenye Ukimwi”.
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi mtu ukiwekewa pesa mfukoni, si ina maana wewe hujawahi kuzishika hizo pesa. Je Tanzania hatuna utaalamu wa kuthibitisha kitu kama hicho?

  Habari ya huyu mwandishi inaweza kuwa kweli lakini pia inawezekana kabisa alichukua hiyo laki moja toka kwa Hosea na hivyo kuishia pabaya.

  Kama ni kweli alibambikiziwa hizo pesa basi Tanzania tunaelekea kubaya sana.

  Hivi sheria zetu za kumpekua mtu zikoje? Yaani mtu anaweza kuja bila kibali chochote na kuanza kukupekua? je ukikataa itakuwaje?
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mtanzania,

  Anadai aliamriwa atoe vitu vyote mfukoni mwake. Hivyo alivigusa. Hivi sijui mtu anakuwekea vipi pesa mfukoni. Maana lazima wakuzonge na pale ni hotelini kuna watu kibao.

  Lazima alikuwa STUPID SOMEHOW.
   
 4. D

  Darwin JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ungefanya hivyo mapolisi kanzu wa kibongo wangempiga nakumuongezea kesi nyingine. Na hata kama angetaka akapekuliwa Polisi, kama hao watu wana nia yao wangefanya hukohuko kituoni kumuwekea hizo pesa.

  Nakumbuka kuna jamaa alibambikiwa hivyo hivyo baada yakutembea na ex wa polisi mmoja.

  Hii ndio Tanzania
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli alionewa!inauma sana!lakini si wote walioko jela walipaswa kuwa jela!hii imenikumbusha habari ya yusufu na mke wa farao!
   
 6. D

  Darwin JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Naona hukuisoma hii habari vizuri

  Kuna sehemu iliyosema "Tulizungumza kwa muda na ghafla Hosea alinyanyuka na kulikuwa na watu kama sita walioingia na kuzunguka meza yetu na mmoja alimwingiza mkono mfukoni."Wakaniambia nitulie nisifanye vurugu yoyote na kuwa walikuwa wanashuku nimepokea rushwa,
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Yawezekana walitumia nguvu baadae na wakamkamatisha fedha hizo,
  Hizo ndizo tabia zao .
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Darwin,

  Kuna kitu hapo hakielezeki. Nimesoma sana alivyoingiziwa hela..... Cha ajabu hapo hapo akaambiwa atoe....Je muda gani alijua kama ana hela mfukoni?

  Kuna ka kitu hapo ndugu yangu. Huko kukutana na HOSEA kila mara mbili.... ina maana alidai rushwa mara ya kwanza ya pili akapewa!!!

  FP
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha pole sana
   
 10. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama kweli alionewa nafikiri ana option ya kufungua kesi tena na kutafuta haki yake, nafikiri wanaojua sheria vizuri wanaweza mshauri nini cha kufanya.
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Najua kwa TZ yote yanwezekana, ila tu case ikishafika mahakamani huko kuna nafasi ya haki kutendeka hasa kama una lawyer wa maana. Naamini huyu mhariri alikuwa na uwezo kabisa wa kupata lawyer wa maana.

  Mimi bado naamini kama hiyo pesa umebambikiziwa kuna uwezekano wa kuonyesha kwamba wewe hukuishika. Hata kama mtu atakushikisha kwa nguvu bado naamini kuna uwezo mkubwa wa ku challenge case ya namna hiyo.

  Namsikitikia huyu mhariri lakini pia maelezo yake yananifanya niwe na wasiwasi mkubwa hasa nikizingatia ukweli ambao wengi tunajua kwamba waandishi habari wanachukua pesa ili kuandika mabaya/mazuri ya watu wengine.

  Pili kama mwandishi wa habari ambaye mpaka alikuwa mhariri, huwezi kwenda kuhoji mtuhumiwa au mtu mwingine yeyote tena sehemu ya siri kama hotelini bila kuwa na vifaa vya kazi kama ku record mazungumzo, kuandika notes za mazungumzo nk.

  Siijui hii case vizuri lakini ni kama ina viraka vingi sana. Rushwa yoyote inakuja baada ya mazungumzo ya aina fulani, laiti ange record mazungumzo yao au hata kuandika, mtiririko unaweza kuonyesha kama kulikuwa na mazingira ya rushwa ama la.

  Kama ni kweli alichukua rushwa hana mtu wa kumlaumu zaidi ya yeye mwenyewe. Hosea alitumia njia mbaya lakini mwenye makosa ni mwandishi mwenyewe. Ni vizuri akubali makosa yake na kusonga mbele. Wengi tunajifunza kwa makosa.
   
 12. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  This is definetely one of the contenders of my sadest story of the year! I think kuna umuhimu wa kuwa na kamera kwenye all public buildings, kungekuwa na CCCTV hapa huu mchezo ungekuwa ni wa kitoto. Hainiingii akilini kabisa kwa mtu yoyote kumuomba rushwa Mkurugenzi wa Operesheni wa taasisi ya kuzuia rushwa, you will have to be insane to attempt anything near this!
  Pia kuna umuhimu wa watu wa human rights kuanza kutupia macho magereza yetu, the level of abuse huko is horrifying and shocking.
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2008
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  hivi ndugu yetu Hosea anajisikiaje kama kweli habari hii ni ya kweli? maana nasikia dhambi nyingine hulipwa hapa hapa duniani.............................
   
 14. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Musendo hapa kuna utata ambao mwandishi hakuutatua;

  Musendo alienda kuzungumza nini na Edward? na ile soda nani alilipia?
  Yeye ni mwandishi au mhariri tena mkuu?
  Mwandishi uliemtuma alishindwa kazi?
  Kama aliambiwa alichukua rushwa alietoa hio rushwa si Edward, alishtakiwa?
  Alimsema pale mahakamani?
  Inawezekana kuwa aliwekewa mtego akaingia kingi! kwanini hakukata rufaa kama alionewa?

  Ujanja wa kukamata watu kwa mitego ndio mbinu wanaitumia hawa jamaa kwa hio huenda aliingizwa mkenge nae akajaa.

  Musendo unamengi ya kutueleza. C'mon please.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kama ni kweli alionewa na kubambikiwa kesi.
  Mhusika kama alisingiziwa kesi..basi alichelewa sana kutafuta haki yake maana baada yakutumikia kifungo chake kamili itakuwa vigumu kudai
  " malicious prosecution". Angeweza kudai hivyo kama yafuatayo yangefanyika:
  1. He was maliciously prosecuted
  2 The prosecution resulted in acquital and not conviction
  Mwenzetu huyu alishtakiwa, kesi ikasikilizwa, akaonekana na hatia, hakukata rufaa kupinga conviction wala adhabu.
  Sijui sasa ataonyesha ushahidi gani wa malicious prosecution.
  Labda kuna lingine la zaidi ambalo hatulijui..ambalo likiwekwa bayana litamsaidia..sijui lakini!
  Its a pity that he lost 3 years of his good life in jail...
   
 16. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Huyu Mhariri ashukuru mungu na kuangalia mbele, mafisadi siku zote kufuta soo hukuangamiza kabisa na kufuta foot print yako duniani, negligency aliyoifanya na iliyotokana na yeye kujiamini kuwa Big man like Hosea hawezi kumfanyia mtego wa kitoto kama huo ndio iliyopelekea kufungwa jela, pia tukumbuke kuwa miaka ile aliyokamatwa ndio kwanza tongotongo hazijatutoka kikamilifu kuwajua mafisadi ni akina nani na kwa uwazi, hebu tuangalie kama akina Zombe wangekamatwa wakati huo je leo kungekuwa na kesi? kuhusu kubambikiwa kesi mimi sishangai hata kidogo kwani ni kawaida kwa Tanzania yote hakuna palipo salama, nimeshuhudia mke wa mtu akishirikiana na polisi kumbambikia mumewe kesi ya kumlawiti mtoto wao mdogo, Polisi walishawahi kuniomba msaada wa ushahidi wa uongo mahakamani ili tu washinde kesi dhidi ya kijana fulani kisa kikiwa kugombea binti wa JKT pale Ruvu etc. Ukweli ukiwa raia mwema na ukimuona Polisi wa Tanzania anakukaribia basi piga kelele ili uweze ku-attract watu watakaokusaidia au watakaokuwa mashahidi wako pindi mambo yakiharibika, please; never ever trust those fuc..@!&....in, Burstx...ds!!!!
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mh, ni kweli kuna maswali yanahitaji majibu ya kujitosheleza:

  Mhariri Mkuu unakwenda kukutana na 'mshukiwa' wako hotelini? pekee yenu?

  Inanikumbusha vile hawa baadhi ya waandishi wanavyokwenda kwenye ofisi na majumba ya wahindi kufanya uharamia wa kudai rushwa kwa kutumia vihabari vya kutishia. Kuna baadhi ya waandishi kazi yao ni kutafuta rushwa kwa kutishia kuandika jambo gazetini.

  Ushauri: Andika kitabu tu kinachoelezea maisha ya jela na umshukuru mungu kuwa umetoka salama
   
 18. D

  Darwin JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hata mimi hicho kitabu nakisubiri kwa hamu
   
 19. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama huu ni ukweli, basi malipo ni hapa hapa duniani.
   
 20. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145

  C'mon GM...kwa story yake huyu nakwambia hawezi fanya hivyo....Jela mchezo....bora asonge mbele na maisha yake kwanza aliacha watoto watano hajui wakati hayupo what was goin on...yote haya akae afanyie kazi..mambo ya kukata rufaa achane nayo atulie......unaweza kata rufaaa harafu ukashidwa...na
  kwa kuangalia bado anataka kuendelea na uandishi....ana guarantee gani hawezi mess up somewhere along the road...akarudushwa Keko tena?

  Kwa sasa ana shida sana...from this sad story anatakiwa afanya juhudi za msingi kurekebisha maisha yake...kuna mengi hajasema kuhusu jela?

  Tunahitaji....hayo ...kwanza amenigofya sana...kwa style ya hosea na technologia mbovu ya tanzania...kwa kweli ujanja hakuwa nao...

  Jamani jela tupasikie...tu...katika watu ambao siwaamini hapa duniani ni pamoja na polisi hasa wa east africa...jamani....dhiki..

  Fikiri umeenda kwenye ATM unamkuta askari pale kasimama kwa pembeni ya mashine kwenye kioo mean kwamba anakuona unatoa pesa ukitoka tu anasema mkuu niachie hata ya kahawa.....uffss.

  So kwa big fish kama hosea wasinge weza ku pinga kitu yaani wanafanya kama mbwa tu.
   
Loading...