Hooooodi wajameni!

Think Tank

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
233
25
Eid Mubarak wanajamii!Mimi ni mgeni katika jukwaa lenu hili,ila nimelifatilia kwa muda mrefu sana kwa kusoma fikra zenu,dira na maoni mbalimbali hivyo nami nijiunge ili nami nitoe yaliyomo katika mtima wangu.Naomba ushirikiano wenu pindi takapokosea,ili niendane na maana halisi ya jukwaa hili.Pamoja tunajenga taifa!
 
Karibuu mgeni karibuu kwenye jamvii hili la CHADEMA!! Lakini kama wewe ni CCMm ni bora utoke berenge mapema
 
Mtambo bwana, mwache aje hata kama ni wa sisiemu ili tumsaidie kufikiria mbali. si unajua hawa jamaa wanafikiria kama kuku anavyoona, karibuuuuu so mwache tumpe mawazo mbadala yatakayomfanyia blood transfusion kutoka njano na kijani hadi ile ya chama kubwa CHADEMA
 
Kwanza rangi hzo mi sio mshabiki wake kabisa.Tukija kwenye chama ndio kabisaaa!Mimi mara nyingi huwa naangalia chama gani kinachomtetea Mtz.Alafu kwenye kupiga kura hatupigi kwa kwa kutumia kadi ya vyama,kwa hiyo tusiwe mashabiki wa vyama pasipo kuangalia mustakabali wa taifa letu.Nina miaka 33 sasa sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kile mpaka leo hii.Mwaka huu nimempigia kura Dr Slaa sio kwa ushabiki bali kwa sababu ni mpiganaji wa kweli na hata kama akigombea 2015 kwangu mmi kura yangu anayo.
 
Karibuu mgeni karibuu kwenye jamvii hili la CHADEMA!! Lakini kama wewe ni CCMm ni bora utoke berenge mapema

Kwani Ccm hawatakiwi?Mi napenda wawepo ili mshindane kwa hoja na sio vioja!Maana mkiwa Chadema hapatanoga mkubwa!Ni kama Simba au Yangu moja ikishuka daraja mpira utanoga?Ni hayo tu mkubwa.
 
You are really a Think Tank!!!!
 
Back
Top Bottom