Hongereni Watanzania kwa kumtambua adui wetu nambari wani, taratibu tutafika !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,296
20,841
Nawapa pongezi Watanzania popote pale walipo ambao bila kujali itikadi, dini, jinsia wala rangi, kwa kuamka na kutoka usingizini, usingizi mzito wa miaka karibu hamsini, na taratibu wanaanza kuuona mwanga wa mabadiliko, mwanga wa matumaini na mwanga wa mafanikio.

Ilianza kama ndoto lakini Watanzania pole pole wanaanza kumtambua adui mkubwa wa taifa letu, zimwi linalotutafuna bila huruma na genge ambalo bila haya wala soni limejimilikisha hatimiliki ya taifa letu kwa mabavu, hila na udanganyifu ili kulinda maslahi yake na si ya taifa.

Nawashukutu Watanzania wazalendo ambao bila kujali vitisho na manyanyaso, wamejitolea kuyaongoza mapambano ya ukombozi dhidi ya utawala huu usiozingatia sheria, utawala usiojali haki, utawala wa kimabavu na utawala wa kifisadi, wahanga wakiwa ni raia wema wasio na hatia.

Heko Watanzania ambao hivi sasa wamechoshwa na utawala huu wa CCM na wanasema hapana, hali kama hiyo katu haiwezi kuruhusiwa kuendelea. Watanzania hawakubali kuendelea kugeuzwa kama mandondocha ndani ya nchi yetu huru, nchi ya asali na maziwa.

Ndugu zangu Watanzania, wale woote wenye uchungu wa kweli kwa taifa letu bila unafiki, kwa sasa tunalo jukumu moja tu, kuitoa madarakani CCM ! Hebu sasa tujipange tuweze kulikomboa taifa letu mikononi mwa hawa wezi na wanyang'anyi kwa kutafakari, tufanye nini kabla ya 2015 ?
 

mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
endapo elimu ya uraia itasambaa hadi vijijini na watu wa mjini kuelezwa kua hzo buku mbili mbili na wali havitawafikisha miaka mitano
 

mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
185
hongera watanzania wote mlio litambua hilo jukumu letu ni kutoa elimu kwa watu wengine angalau watano hadi kumi kwa kila mmoja na kuhakikisha anatambua hili na kulifanyia kazi.
 

Konya

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
921
112
ni elimu ya uraia tu basi..tutathubutu,tataweza na tutazidikusonga mbele
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom