Hongereni Wabunge wa Mbeya ila msiishie hapo!

Hao wanaotumia daladala hawawezi jua ukubwa na ubora wa Mby, maana ukianzia Uyole highway kuelekea Iyunga, unapasua Km zaidi ya 15 katikati ya jiji, inakuruhusu kuingia kulia au kushoto zaidi ya km 5 kila upande. Huko ndiko utajua kama Mb ina majengo ya ovyo au vp? Sasa wao wakipita high way tu basi. Sidhani hapa Tz kama kuna miji zaidi ya 3 iliyojengwa eneo kubwa kama Mb.
Hawa ni kama wanaopima ubovu wa DSM kwa kutumia Manzese. Hata DSM nje ya Masaki na maeneo mengine kama hayo kuna mchanganyiko wa nyumba mbovu na za maana, mfano Mikocheni kuna nyumba za ovyo ikiwa nyingine ni nzuri ajabu mpaka huwezi amini kama ni mji mmoja.
Kinachokosekana Mb ni majengo makubwa ya taasisi za umma. Lakini wananchi ni wapambanaji sana.
Amka toka usingizini!

Mbeya ndo sehemu iliyojengwa hovyo zaidi ikifuatiwa na Mwanza na Dsm

Saivi Arusha nayo inaelekea kule kule
 
Kama reference yako ni Mbalizi basi unapaswa kupimwa mkojo. Maana Mbalizi ni Mbeya vijijini. Kwa upande mwingine inafurahisha kuipima Mb vijijini na hiyo miji yako mingine.
Kwa iyo Mbalizi haipo mbeya?
 
Unaota wewe jamaa,huo u hovyo ni upi?
Kuna thread zaidi ya 3 humu jamvini waneleta watu 3 tofauti kuhusu ujenzi wa hovyo wa Mbeya!

Wewe unaepinga inawezekana ukawa hujui ujenzi wa kisasa au wa kimpangilio ni nini?

Nakusaidia, nenda Ilazo Dodoma tembea Ilazo yote utajua maana ya ujenzi wa kisasa na wa kimpangilio ukoje?
 
Mada ni Mbeya yote ndo mana imesemwa Wabunge wa Mbeya
Basi umepandanisha mambo! Mara jiji limepangiliwa ovyo! Wabunge wa Mbeya.
Ulipaswa uzungumzie mkoa wa Mbeya. Hapo ungekutana na Rungwe mji wa aina yake Tanzania. Unakutana na misosi ya ukweli, kijani yote. Ndizi zote mia. Sasa wewe umeenda kuishi Mbalizi unaleta story za jiji la Mbeya.
 
Sawa
Ila Rungwe nako zaidi ya hali ya hewa nzuri Ila nyumba bado za hovyo
 
:p:p:pMiaka ya 2000 niliishi Jiji la Mbeya eneo la Mbalizi. Nilikaa kwenye jiji lile kwa miaka 4

Humu JF nimekuwa mkosoaji mkubwa wa Jiji la Mbeya Hasa kwa namna lilivyojengwa hovyo na nimekuwa nikisema humu halistahili kuwa jiji

Nimekuwa pia mkosoaji sana wa watu wa Mbeya kwamba sio watu wa maendeleo ila ni watu wanaoendekeza ushamba, ujenzi holela na hawajui kubambania maendeleo ya eneo lao hasa kwenye miradi mikubwa ikiwemo kuacha reli ya SGR kujengwa kwenda Kigoma na Mwanza huku wao TAZARA ikizidi kufa!

Baada ya kuanza kwa Bunge la Bajeti napenda kukiri kwa Mara ya kwanza nimependezwa na namna wabunge wa Mbeya walivyoonekana kuanza kuamka hasa baada ya kuanza kudai upanuzi wa barabara zao kuu na ujenzi wa Barabara bora!

Napenda kuwasihi watani zangu hawa kuwa wasiishie kudai barabara Nzuri tu na bypass, waende mbele zaidi kuzilazimisha halmashauri zao kupanga makazi na kuhakikisha ujenzi wampangilio unaanza kufanyika mkoani kwao!

Ni aibu Green city kujengwa hovyo namna ile sasa wabunge wa Mbeya waanze kulazimisha halmashauri zao kupanga makazi na miji yao! Waelimishemi na wananchi wenu basi wajenge nyumba nzuri na za kisasa!

Hongereni wana Mbeya kwa kuamka! Endeleeni kukomaa mjengewe hizo double road na msiache kukomaa pia utanuzi wa Barabara uanzie Mlima nyoka!
Tatizo watani zangu ni ubishi tu.
 
Hao wanaotumia daladala hawawezi jua ukubwa na ubora wa Mby, maana ukianzia Uyole highway kuelekea Iyunga, unapasua Km zaidi ya 15 katikati ya jiji, inakuruhusu kuingia kulia au kushoto zaidi ya km 5 kila upande. Huko ndiko utajua kama Mb ina majengo ya ovyo au vp? Sasa wao wakipita high way tu basi. Sidhani hapa Tz kama kuna miji zaidi ya 3 iliyojengwa eneo kubwa kama Mb.
Hawa ni kama wanaopima ubovu wa DSM kwa kutumia Manzese. Hata DSM nje ya Masaki na maeneo mengine kama hayo kuna mchanganyiko wa nyumba mbovu na za maana, mfano Mikocheni kuna nyumba za ovyo ikiwa nyingine ni nzuri ajabu mpaka huwezi amini kama ni mji mmoja.
Kinachokosekana Mb ni majengo makubwa ya taasisi za umma. Lakini wananchi ni wapambanaji sana.
Umeichambua vizuri mkuu.
Pia Jiji Wangefanya utaratibu wa kupima yale mashamba pale Uyole watu wanunue wajenge majengo. Watu wa Kilimo Uyole wakaanzishe mashamba darasa nje ya mji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom