Hongereni wabunge wa CCM - kwa msaada wenu mageuzi yananukia !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,037
22,728
Nawapa hongera sana Wabunge wa CCM chini ya kamanda wao Spika Makinda. Mshikamano wanaouonesha hivi sasa ndio unaotakiwa kwani unaondoa kabisa matumaini ya Watanzania kuwa anaweza akatokea mkombozi miongoni mwao. Kikao hiki cha Bunge kimetuthibitishia kuwa ndani ya CCM hakuna wa kumnyooshea mwingine kidole kwani wote ni wazi wameoza na anaedai vinginevyo ni mnafiki na huenda kaoza zaidi.

Sitaki tena kusikia eti fulani na fulani ndani ya CCM ni afadhali, la hasha, hao wanaoonekana afadhali ndio hatari zaidi na hivi sasa yatubidi tuanze kuwaanika ili wananchi wakae nao mbali ! Ukweli kuwa CCM imegeuka na kuwa kimbilio la wezi na mafisadi umedhihirika hivi sasa kuliko wakati wowote mwingine katika historia ya Tanzania. Wazalendo, kwa matendo ya wabunge wa CCM, njia ya kuelekea mageuzi yabakia sasa nyeupee !

Kwa kuanzia lazima sasa tuwataje kwa majina yao waliodaiwa wapiganaji ndani ya CCM kumbe ni mazimwi wala watu na wasaliti wakubwa waliovaa ngozi ya kondoo. Mimi leo naanza na Spika wa zamani Samweli Sitta, historia ya utumishi wake siku za nyuma ? alivyotetea matumizi makubwa ya ofisi ya Spika ? matibabu na kodi kubwa ya nyumba ? mnakumbuka alivyozima Richond ? alivyowaka mkewe alipotuhumiwa kwa rushwa ? ni mengi !
sitta-na-chenge.jpg

  1. Sita
  2. Mwakyembe
  3. Nape
  4. Kilango
  5. Ole Sendeka

tuendeleee............
 
Wa pili Dr. Harrison Mwakyembe, mbunge wa Kyela ambaye kwa tamaa ya madaraka kama walivyo wasomi wengi ndani ya CCM alishawishiwa kuficha ukweli ili kumsetiri Jakaya Mrisho Kikwete, mhusika mkuu wa sakata la Richmond. Wakati huo yeye alidai anaisetiri serikali, na kama fisi amezawadiwa mfupa na sasa katulia tuli mafichoni akiwa bize akimeza bila kutafuna safari hii giza lililotanda nchini likimsetiri yeye. Wapiganaji, my foot !


IMG_2005.jpg


tuendelee...........


 
Wa pili Dr. Harrison Mwakyembe, mbunge wa Kyela ambaye kwa tamaa ya madaraka kama walivyo wasomi wengi ndani ya CCM alishawishiwa kuficha ukweli ili kumsetiri Jakaya Mrisho Kikwete, mhusika mkuu wa sakata la Richmond. Wakati huo yeye alidai anaisetiri serikali, na kama fisi amezawadiwa mfupa na sasa katulia tuli mafichoni akiwa bize akimeza bila kutafuna safari hii giza lililotanda nchini likimsetiri. Wapiganaji, my foot !
tuendelee...........
taja bhana.
 
taja bhana.

Watatu ni Nape Nnauye, huyu sitapoteza hata muda kumjadili kwa sababu huko kumtaja tu nakubali nimeshaidhalilisha nafsi yangu vya kutosha.
07_11_jefsce.jpg


tuendelee.............
 
Ndugu' naunga mkono hoja.KAMA WOTE WAMEMTETEA CHENGE BUNGENI' WAKATI WAKIWA NJE YA BUNGE WANAMTAJA KAMA GAMBA UJUE KWELI WABUNGE WA CCM SIYO WA KUWAAMINI TENA! Hv wamepitisha ile bajeti ya afya ambayo 97% inategemea misaada ya nje?! Ni ujinga' badala ya bunge kuisimamia serikali ,serikali ndiyo inawaongoza wabunge(kumbuka nazungumzia wabunge wa ccm) BAHATI NZURI WANANCHI WA TANZANIA WAMEANZA KUELEWA-hebu angalia ushindi wa D.Silinde,D.Kafulila na vijana wengine! HONGERENI WATANZANIA.
 
Ndugu' naunga mkono hoja.KAMA WOTE WAMEMTETEA CHENGE BUNGENI' WAKATI WAKIWA NJE YA BUNGE WANAMTAJA KAMA GAMBA UJUE KWELI WABUNGE WA CCM SIYO WA KUWAAMINI TENA! Hv wamepitisha ile bajeti ya afya ambayo 97% inategemea misaada ya nje?! Ni ujinga' badala ya bunge kuisimamia serikali ,serikali ndiyo inawaongoza wabunge(kumbuka nazungumzia wabunge wa ccm) BAHATI NZURI WANANCHI WA TANZANIA WAMEANZA KUELEWA-hebu angalia ushindi wa D.Silinde,D.Kafulila na vijana wengine! HONGERENI WATANZANIA.

Mmmh, hakika inasikitisha ! Wa nne ni Mh. Anne Kilango, mbunge wa Same ambaye kama kinda akisikia njaa, hupanua mdomo na mama kinda bila ajizi humsukumizia naye akishashiba kelele yote huisha. Miongoni mwa akina mama wanafiki, huyu katia fora.
Untitled-1.jpg

jk-same-1.jpg


Haya tunaendelea ...........
 

Attachments

  • jk-same-1.jpg
    jk-same-1.jpg
    25.2 KB · Views: 24
Watano ni Christopher Ole Sendeka, mbunge wa Simanjiro anayejulikana kwa ulafi, uhuni na ugomvi kwa kiwango cha kutisha licha ya kisomo cha wasi wasi. Huyo mtupie mfupa tu na atawasaliti hadi ndugu zake.

Tuzo%2BBiashara%2B026.jpg


sehemu ya hili lundi naambiwa hivi sasa liko Mbeya !

tunaendelea...............................
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom