MANILABHONA
JF-Expert Member
- Apr 1, 2015
- 462
- 348
Nimefurahi kuona TBC walivyofanya uamuzi wa kwenda Uganda kujifunza namna ya uandaaji wa vipindi vya TV na urushaji wa matangazo. Kongole kwao.
Kwa kweli ilifika mahali watanzania walio wengi hawapendi kuangalia televisheni za humu ndani kutokana na kukosa ubora wa vipindi, kukosa maudhui.
Baadhi ya televisheni zikageuka kuwa majukwaa ya kisiasa au ya mikutano ya kisiasa. Wengi tulijiuliza hivi waandaaji wa vipindi vyetu wanabahatika kuangalia televisheni nyingine hata za hapo kenya tu au uganda au hata rwanda. Sasa TBC mkirudi murudi mkiwa mmejifunza siyo 'business as usual'.
Mnatia aibu, aibu, aibuuuuuu! Fanyeni tathmini ya vipindi mnavyorusha wenyewe si kwa kuuliza watu. watanzania hatuna kawaida ya kukueleza ukweli hata kama tunaona unaharibu.
Wanaoangalia tv za humu ndani wengi ni wale ambao hawana namna, TBC kipindi pekee huangaliwa ni Zilipendwa, pengine na taarifa ya habari.