Hongereni TBC kwa kuboresha muonekano

Majs

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
229
481
Habari waungwana,

Binafsi huwa naamini TBC 1 na TBC Taifa huwa na vipindi vingi vizuri ukiacha habari na baadhi ya vipindi vya kisiasa ambayo bado inajadilika lakini pia kuwa chombo cha serikali ni rahisi kuwa upande uliopo kwani sehemu nyingi duniani chombo cha habari cha taifa(Serikali) huwa kinasimama upande wa serikali.

Pamoja na kupenda vipindi vyake vingi kuanzia kilimo, biashara, technolojia, lugha na Zaidi TBC nahisi ndio televisheni yenye makavazi mengi na bora namba moja nchini, vipindi vinatengezwa popote Tanzania na vingine ukiangalia unaona gharama ya kuvitengeza ni kubwa kuliko matarajio jinsi watakavyonufaika hasa vinavyoelimisha.

Pamoja na yote lakini muonekano ulikuwa unachosha mpaka kukatisha tamaa. Ukifungua TV nyingine muonekano mzuri lakini mwendo wa muziki na burudani kwa ujumla, wengine mahubiri na mawaidha.

Karibuni naona muonekano bora wa TBC 1 kulinganisha na awali, angalau picha imekuwa angavu na haichoshi kama zamani. Naamini wataendelea kuboresha ili walingane na umri wao kwenye tasnia ya habari hasa luninga, nyingi zilizokuja miaka ya karibuni ziliwapita tena nyingine zikionekana kuwa na mitaji midogo mpaka unajiuliza wanakwama wapi. Mna gari la kisasa la matangazo bora kuliko yote nchini lakini ikija kwenye mubashara, Azam, ITV na wengineo wanawaacha mbali sana.

Hongereni lakini boresheni Zaidi.
 
Huenda! Lkn ikiwa ni tv ya umma wajitahidi kuboresha kama ZBC2 inayotufurahisha sana kwa vipindi mubashara vya michezo, bigup ZBC 2!

Sent using Jamii Forums mobile app

ZBC 2 nahisi ina ushirikiano Fulani na Azam, designs zinazotumika siku ya mechi utaona zinafanana sana na Azam pia sio ajabu kusikia watangazaji wa mechi ni kutoka Azam, kuthibitisha ZBC 1 iko ovyo sana kulinganisha na ZBC 2.
 
TBC ilianza kuonyesha uhai enzi za Mkurugenzi Tido Mhando. Ungeweza kuona wanakata matangazo ya CCM na kujiunga na matangazo ya CDM ya Dr. Slaa. Sasa hiv thubutuuuu!


Wajuvi wa TV za bongo hiv C2C ipo wap?
 
TBC ilianza kuonyesha uhai enzi za Mkurugenzi Tido Mhando. Ungeweza kuona wanakata matangazo ya CCM na kujiunga na matangazo ya CDM ya Dr. Slaa. Sasa hiv thubutuuuu!!


Wajuvi wa TV za bongo hiv C2C ipo wap?

Kuna DTV pia, sielewi kwanini haikusimama au walikosea wapi mpaka kudondoka.
 
Kwa kweli sasa hivi huchoki kuangalia TBC, nimeangalia tarifa ya habari yao, na muonekano mzuri, nilitamani habari isiishe. Hongera TBC.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom