Hongereni sana wanawake kwa uvumilivu mlionao katika ndoa zenu

projectman

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
349
486
Habari zenu wana JF,

Leo nimejaribu kufikilia na kuwaza sana historia ya maisha yangu vile mama yangu alivyo nilea mimi, ingawa tulipita katika magumu mengi rest in peace mama! Binafsi ninapenda kuwapongeza wanawake wote wanao vumilia na kuwa waaminifu katika ndoa zao.

Pia nimegundua kuwa sisi kama wanaume tumekuwa tukiwalaumu sana wanawake hata kwa makosa yasiyo yao hadi kupelekea mwanamke kudhalauliwa na jamii husika.

Maana ya hoja hii, sijamaanisha wanawake wote bali ni wale walio wavumilivu na heshima dhidi ya ndoa zao na watu binafsi nina zaidi ya sababu kuwashukuruni wote maana bila hawa hakuna mtu angezaliwa, mateso wanayo yapata katika kujifungu either kwa operation au kawaida+ miezi 9 tumboni ninaishiwa na kusema big up women.

Katika maisha tunayoishi tukiwa jinsia mbili tofauti huwa kunakuwa na mapungufu mengi hujitokeza lakini katika hayo jinsia zote zinahusika katika mapungufu na hekima, nikimaanisha kuwa hakuna aliye mzuri sana wala mbaya sana isipokuwa tukiwa kama binadamu sisi sote tunamapungufu na tumepungukiwa na maharifa.

Wanaume tukiwa kama viongozi katika familia zetu tumekuwa tukitumia fursa hiyo kuwanyanyasa hawa wanawake kwakuwa tunajiona kama ndio tunastaili na hatukosei tujifunze kuheshimiana na kupendana kwa uhaminifu huku tukimtanguliza Mungu.Popote ulipo mwanamke unayejitambua na unayatenda haya basi sina budi kukupa big up maana pasipo wewe hakuna generation.

Tafadhali kwa wale wenye mifomo dume please naomba msije huku.

Ninawasilisha.
 
Hongereni wanawake...endeleeni kutuvumilia tukichepuka msichoke...
 
Aisee mimi ni mwanaume lakini uvumilivu wangu huwezi kulinganisha na mwanamke yeyoye hapa Tz
 
Upo sahihi kabisa, wanawake ama wakinamama, ni watu tunapaswa kuwatetea sana haswa kuwaheshimu.

Mengi makuu wametutendea yaliyo Mema.

Ahsante Mama, popote pale ulipo. UPUMZIKE KWA AMANI.

Ahsante!
 
Sasa jaman tena 'MAMA' Daaah! Uvumilivu wa mama hauna mfano hata mapenz ya girlfriend na boyfriend hayafikii hata robo.
 
women's day.............
kiukweli mie haya ya siku ya wanawake dunian sionagi umuhimu wake.

kwakua wewe umetupongeza nami nasema ahsante san kwa pongezi.
 
Mimi kila mara nashangaa kuona kuna watu wasoni na elimu zao wanadhani kuwa.mfumo dume ni hatari na unatisha dhidinya wanawake.

Tatizo hapa sio mfumo dume, maana mfumo huu huwezi kuufuta badala yake utaufanya ete madhala zaidi. Tatizo ni matumizi mabaya ya mfumo dume.

If its patriachy your are runing from, then you just have no hiding place.

Mfumo dume ndio unatufanya tuoe na sio kuolewa, tuwatunze wanawake na kuwapenda na sio watutunze.
Mfumo dume ndio hufanya wewe uitwe baba yeye aitwe mama. Aitwe mwanamke wewe uitwe mwanamume, its natural and when you want to fight against nature madhara yake ni homosexualitu ambayo inapigiwa chapuo na watu waasi wa mapenzi ya Mungu.

Note; if its patriachy your are running from, you just have no hidding place.
 
Back
Top Bottom