Hongereni sana wanawake hakika ninyi ni malkia wa nguvu

Richard chilongani

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
324
112
HONGERENI SANA WANAWAKE HAKIKA NINYI NI MALKIA WA NGUVU.

Tarehe 8 march kila mwaka tunaazimisha siku ya wanawake duniani, katika maazisho ya 2017 naomba tukumbushane haya kwa pamoja.

Mwanamke anaweza kulala njaa watoto wale washibe , mama pekee ndiye yupo tayari kuacha chakula ili wale watoto wala siyo rahisi kumkuta mama anakula hotelini watoto wakiwa hawana chakula, wakati baba akipata supu, nyama choma, kahawa vijiwe mwanamke huteseka ili watoto wapate kushiba , bila chakula ndani mwanamke anaweza kufanya lolote ili kipatikane lakini siyo baba. Mwanamke hawezi kutelekeza watoto kisa njaa lakini baba ni rahisi mno kuondoka kwa kisingizio cha kwenda kutafuta maisha bila kujua watoto wanakula nini , hakika wewe ni malkia wa nguvu jikubali.

Mwanamke ni mzazi mwenye Taaluma nyingi ni mwalimu mzuri elimu yake haina gharama lakini ubora wake hauna mfano, ni daktari mzuri mwenye utambua tatizo la mtoto hata bila vipimo vya kitaalamu, ni hakimu mzuri daima humaliza kesi za watoto kwa amani na upendo mkubwa, ni mguuzi mzuri mwenye huruma , ni mhasibu mzuri daima hesabu zake kwa familia hazina utata, ni mwanadiplomasia daima humaliza migogoro kwa amani bila upendeleo, hakika wewe ni malkia wa nguvu jiamini na jikubali popote.

Mwanamke ni rafiki mwema wa watoto ni rahisi sana mtoto kuwa karibu na mama wakati wa shida na raha , mtoto akipata matatizo kituo chake cha kwanza kwa mama wakati mwingine mtoto kufikia hatua ya mkutumia mama kufikisha ujumbe kwa baba hii ni kipimo kikubwa kuwa mama ni msikivu, mwenye huruma, mwenye kuunganisha, hakika urafiki wa mama kwa watoto ni mtakatifu.

Mwanamke ni kiongozi makini mwenye hekima, busara,msikivu asiyekuwa na upendeleo mwanamke anaweza kulea watoto wengi wenye tabia tofauti wagomvi,wapole,walevi, washari kwa upendo,uongozi wa mwanamke ni wenye utukufu daima wala hauna shaka,wakati mwanamke anaweza kuishi na mwanaume mlevi, watoto wasumbufu mwanaume hawezi kuvumilia changamoto za watoto,ni rahisi sana mwanaume (baba) kuachana na kumpuuza mtoto mtukutu wakati mwanamke (mama) huendelea kuwaongoza watoto bila kujali madhaifu yao ilimladi wafikie ndoto zao,furaha ya mwanamke ni mtoto kufikia ndoto zake daima huwa kiongozi mwema kwa watoto bila kuchoshwa na madhaifu yao.

Mwanamke ni jasiri mwenye kusafiri usiku wa manene umbali mrefu kutafuta dawa za mtoto,mwanamke haogopi kupita kwenye pori kufuata huduma ya mtoto mgonjwa, mwanamke wala haogopi kubeba mimba miezi tisa akiwa kijijini kisicho hata na kituo cha afya , mwanamke wala haogopi kumlea mtoto bila baba baada ya kutelekezwa, ujasiri wa mwanamke hauna mfano duniani hasa kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto, pengine bila ujasiri wa mama zetu wengine tungepoteza uhai wetu tukiwa vichanga kabisa, hongera sana mwanamke popote ulipo wewe ni malkia wa nguvu.

Mwanamke anaweza kuwa baba lakini baba hawezi kuwa mama , tunashuhudia katika jamii mwanamke akiwa na vyeo vyote kwenye familia hasa baada ya kukimbiwa na mwenza daima wala mwanamke harudi nyuma huchukua majukumu yote ya kwake(mama) na ya baba kuhudumu vema familia kwa upendo mkubwa , ni ngumu sana mwanaume kubeba majukumu ya mama kwenye familia hii inaonesha kiasi gani mwanamke ni zaidi ya mama katika jamii zetu , tunashuhudia familia zilizotekelekezwa na mwanaume zikiwa zenye upendo, furaha na amani na mshikamano. Mwanamke popote ulipo wewe ni shujaa ,jivunie kuwa mwanamke.

Mwisho,ndugu mtanzania mwenzangu kwa pamoja tuseme hapana ukeketaji, tukomeshe mimba za utotoni, tupige vita mfumo dume, tuseme inatosha mtoto wa kike kutembea umbali mrefu kufuata masomo, tuseme imetosha kusitisha masomo watoto wa kike kisa ujauzito huku watia ujauzito wakila maisha mtaani, tuseme hapana tena vifo vya uzazi, tuseme imetosha unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Serikali, Taasisi binafsi na wananch kwa pamoja tutimize wajibu wetu kulinda utu wa mwanamke kwenye sekta ya elimu, sekta ya afya , serikali itimize wajibu kwa andaa mazingira, Taasisi binafsi na wananch pia tutimize wajibu wetu.

TANZANIA YENYE USAWA WA KIJINSIA INAWEZEKANA,ANZA SASA KULINDA UTU WA MWANAMKE.

Hongereni sana wanawake binafsi siku zote natambua thamani yenu wala sisubiri tarehe 8 March.

Ndimi LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331
 
Back
Top Bottom