Hongereni sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa na Msemaji Dkt. Hassan Abbas

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Nitoe tu pongezi zangu za dhati kabisa kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuamua kabisa bila kushinikizwa na Mtu yoyote kumteua Bwana Hassan Abbas kuwa Msemaji wake na pia kuwa ndiyo Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo.

Kwa sifa alizonazo Msomi huyu wa Shahada ya Juu kabisa ya Uzamivu ( PhD / Doctor of Philosophy ) Hassan Abbas ni dhahiri kabisa kwamba ataisaidia mno Serikali katika kutekeleza kile inachokitaka hasa katika suala zima la Kuwahabarisha Watanzania juu ya mambo mbalimbali.

Hizi Sifa alizonazo naamini akiendelea nazo Dkt. Hassan Abbas atakuwa mahiri sana katika nafasi yake ya kuwa Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari na Maelezo kwani anaziweza na anazitendea haki mno kila anapoitisha Press Conference zake:

  1. Anacheka cheka pasipo hata kuchekeshwa na Mtu yoyote
  2. Anaogopa kuulizwa maswali mengi na magumu na Waandishi wa Habari
  3. Anachagua Waandishi wa kumuuliza maswali
  4. Hajiamini na muda mwingi anababaika babaika hivi kama mtu anaetaka kukimbia
  5. Anaharakisha Press Conference imalizike ile akapumzike Ofisini
  6. Anajibu maswali magumu na nyeti sana Kiuwepesi mno
  7. Hana taarifa za kutosha juu ya yale anayoyaamini na anababaisha mno kimaelezo
Nimalizie tu kwa kusema kwamba naipongeza kwa kiasi kikubwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo ipo chini ya Chama Tawala cha CCM hasa kwa kuamua kuwa na ' Wasemaji ' wao mahiri Dkt. Hassan Abbas wa Serikalini na Bwana Humphrey Polepole wa CCM kwani wanatuonyesha ni jinsi gani walivyo ' mizigo ' katika suala zima la ' upashaji ' Habari kwa Wananchi na Wanachama wao.

Ama hakika ' TUNATEKELEZA ' kivitendo.

Nawasilisha.
 
We Genta weee Gentaaa!
 
Kuna Watu wanaiharibu sana hii ' tasnia ' nzima ya Habari na Mawasiliano hasa kwa upande wa ' Usemaji ' wa Taasisi muhimu. Kila nikimwona Msemaji wa IKULU ya Marekani Mwanadada Sarah Huckabee Sanders na Msemaji wa Serikali ya Marekani Mwanadada Heather Nauert halafu nikija kuwalinganisha na Wenzao wa Tanzania wenye Vyeo hivyo hivyo au Majukumu hayo hayo huwa naiona tofauti kubwa sana hasa ya Kitaaluma na Kiuweledi.
 
Nitoe tu pongezi zangu za dhati kabisa kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuamua kabisa bila kushinikizwa na Mtu yoyote kumteua Bwana Hassan Abbas kuwa Msemaji wake na pia kuwa ndiyo Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo.

Kwa sifa alizonazo Msomi huyu wa Shahada ya Juu kabisa ya Uzamivu ( PhD / Doctor of Philosophy ) Hassan Abbas ni dhahiri kabisa kwamba ataisaidia mno Serikali katika kutekeleza kile inachokitaka hasa katika suala zima la Kuwahabarisha Watanzania juu ya mambo mbalimbali.

Hizi Sifa alizonazo naamini akiendelea nazo Dkt. Hassan Abbas atakuwa mahiri sana katika nafasi yake ya kuwa Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari na Maelezo kwani anaziweza na anazitendea haki mno kila anapoitisha Press Conference zake:

  1. Anacheka cheka pasipo hata kuchekeshwa na Mtu yoyote
  2. Anaogopa kuulizwa maswali mengi na magumu na Waandishi wa Habari
  3. Anachagua Waandishi wa kumuuliza maswali
  4. Hajiamini na muda mwingi anababaika babaika hivi kama mtu anaetaka kukimbia
  5. Anaharakisha Press Conference imalizike ile akapumzike Ofisini
  6. Anajibu maswali magumu na nyeti sana Kiuwepesi mno
  7. Hana taarifa za kutosha juu ya yale anayoyaamini na anababaisha mno kimaelezo
Nimalizie tu kwa kusema kwamba naipongeza kwa kiasi kikubwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo ipo chini ya Chama Tawala cha CCM hasa kwa kuamua kuwa na ' Wasemaji ' wao mahiri Dkt. Hassan Abbas wa Serikalini na Bwana Humphrey Polepole wa CCM kwani wanatuonyesha ni jinsi gani walivyo ' mizigo ' katika suala zima la ' upashaji ' Habari kwa Wananchi na Wanachama wao.

Ama hakika ' TUNATEKELEZA ' kivitendo.

Nawasilisha.
Inaonekana uwezo wako wa kufikiria ndiyo umeishia hapo. Na kwa kawaida ya siku zote upinzani mmekuwa mnazidi kupungukiwa vitu kichwani. Dkt Abbas anatumia weledi kujibu utumbo wenu, na majibu yake yanajitosheleza vilivyo. Pole sana kwa kuwa na uwezo mdogo wa kufikiria maana akili zenu zimeshikiriwa na upingaji
 
We Genta weee Gentaaa!

Niambie Mkuu valet de chambre. Kama una Simu hapo hebu tafuta Press Conference ya Msemaji Msomi wa ' gavamenti ' ujionee ' mazingaombwe ' yake ya Kitaaluma na ya Kiuweledi halafu rejea hizo Sifa Saba ( 7 ) hapo juu kisha unipe nawe mrejesho wako. Hivi hizi PhD's Watu huwa wanazipataje kwani mbona wengi wao haziendani na ' Utendaji ' wao hasa katika ' Nyadhifa ' walizopo?
 
Inaonekana uwezo wako wa kufikiria ndiyo umeishia hapo. Na kwa kawaida ya siku zote upinzani mmekuwa mnazidi kupungukiwa vitu kichwani. Dkt Abbas anatumia weledi kujibu utumbo wenu, na majibu yake yanajitosheleza vilivyo. Pole sana kwa kuwa na uwezo mdogo wa kufikiria maana akili zenu zimeshikiriwa na upingaji

Hivi kumbe ' Purely Talented and Charismatic Fella ' GENTAMYCINE ni mwana CHADEMA? Pumbavu mkubwa Wewe naijua CCM kuliko Wewe na hata Wazazi wako na Mimi ni mwana CCM tena nimekuzwa na itikadi mahiri za CCM ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na ukiona nasema kitu au nina wasiwasi nacho kaa chini ukitafakari kwani huwa sikosei katika tathmini na uchambuzi wangu.

Halafu hii dhana ya nyie wana CCM wenzangu na baadhi ya Watu wa Serikalini kudhani kwamba kila anayeisema vibaya Serikali au Watendaji wake basi ni mwana CHADEMA ndiyo inatufanya tuzidi kuonekana ' Wapumbavu ' mbele ya wenye ' akili ' zao.

Halafu ujione Wewe ni ' Mpumbavu ' Bosi wako mwenyewe wa Chama chako ' maandiko ' yangu haya mengi huwa anayasoma na hata Watendaji wake huwa wanampelekea na mengi ambayo nimeyasema humu humu JamiiForums yamefanyiwa Kazi na ndiyo maana unaona ' najiamini ' hivi.

Hopeless mkubwa Wewe. Nasubiri urejee ili nikupe ' dozi ' ya mwisho ukasimulie vizuri Kwenu.
 
Msamehe mkuu, watu wengine hawajui kama wanajibishana ovyo ovyo na watu walio wazidi umri baba zao.
 
Saa nyingine kama huna cha kuandika ukae kimya. Ficha upumbavu wako.ivi ujui kama ile taarifa ya Dr Abbas kuna baadhi ya vituo vya redio na Tv watairudia na watanzania walio wengi wataitizama na watakudharau kwa bandiko lako hili?
Dr Abbas ameulizwa maswali baada ya kutoa taarifa ya serikali na akajibu maswaliyao kwa ufasaha na katika majibu aliyokua akitoa amejibu na kufafanua kwa mifano iliyohai.
Mwishoe aliwauliza waandishi kama kunaswali lolote lakini waandishi hawakua na lakuuliza.

Ivi uta mfananisha na DJ alivyo ita wanahabari kuongelea afya ya Lisu!!?

Jasho lilikua likimtoka mbaka kwenye matundu yasiyo stahili kutoka majimaji. Achakutumika kama Tishu za kujisafishia.
 
Dr Abbas ni Msemaji wa Serikali.
Vipi kuhusu Bunge na Mahakama...???
Sakata la Nyalando,tumeona NEC,BUNGE na CCM wakijikoroga,kwa nini wasiwe na wasemaji ili watoe kauli thabit..???
Nina wasiwasi hizi kauli pinzani zitakuwa na gharama ifikapo 2020 panapo uhai na majaaliwa yake MOLA
 
Back
Top Bottom