Hongereni sana mabinti/wanawake wa Kisukuma kwa haya

Mdau umeongea ukweli, yaani ukoo wangu wote kwa baba na mama hakuna aliyeoa au kuolewa na hayo makabila. Wote wana ndoa na wasukuma, wakerewe na wanyamwezi basi.
Asili ya msukuma ni upendo tena ule wa dhati kabisa! hatunaga zile mambo za kumkrimu mtu jujuu tu then akitoka nyuma unamng'ong'a!
Kwa wasukuma ugali au chakula chochote kinapikiwa nje na kinaliwa hadharani. Mgeni au mpitanjia ukiona ugali unaliwa huna haja ya kusubiri karibu tule! Ukiona, nawa kula utashiba na utaacha chakula!! Ugali unapikwa mkubwa kwelikweli tena in extra amount mle mpaka ubaki na ukiisha kuna uwezekano ukapikwa mwingine!
Kwetu wali na viazi sio chakula ila ugali ndo humaliza milo yote!
Tunakula mboga zote huwezi kukuta mtoto wa kisukuma anasusa au kuchagua mboga!

Kwa makabila mengine haya mambo ni ngumu sana kukutana nayo! Nafikiri ni kwa sababu hawazalishi vyakula vingi ndicho kinapelekea kuwa wabahili na wabinafsi!
 
Mmh sio kweli mnakwepa kuoa wachaga bhana.
Fanya uchunguzi wa kina mkuu!
Miaka ya sasa ndo kidogo kumekuwa na mabadiliko hasa usomi na umjini mwingi ndo mtu anaamua kuvunja miko.
Asili ya msukuma sio ubahili au umimi!
Sasa wachagga wana hizo character so inakuwa ngumu sana ku mingle mkaendana!
 
Back
Top Bottom