Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,671
- 40,913
Kwa moyo wa dhati nipende kuwashukuru watendaji wote wa Law School of Tanzania (shule ya sheria ) kwa kuzingatia weledi katika kufundisha na hatimaye kutoa wanasheria ambao watatumika serikalini pamoja na sekta binafsi.
Napenda nikiri wazi kabisa kwamba shule hii ni moja wapo ya taasisi chache za Serikali zinazozingatia weledi.
Watendaji wake hawafungwi na jina la mwanafunzi wala uwezo wake kiuchumi.
Wanazingatia kujiweka mbali na ukaribu na wanafunzi utaopelekea kutoa upendeleo katika usahihishaji.
Wanazingatia mno ubora wa mwanafunzi katika kutoa kile alicho nacho kichwani kwake.
Nawaomba wasiache hata mara moja ubora huu kwani kwa kufanya hivyo wataliangamiza Taifa kwa kutoa wanasheria wasiokuwa na uwezo hivyo kuharibu taaluma ya sheria.
Mungu aendelee kuwatia nguvu kwa kusimamia taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa.