Hongereni sana EATV kwa kuanzisha kipindi bora kabisa cha mjadala wa wazi

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Kimeanzishwa kipindi kipya Cha mjadala katika Televisheni ya EATV, ambacho Kwa mara ya kwanza kilirushwa Jana Jumanne, tarehe 10/02/2023 chenye mada iitwayo Je Siasa safi zinawezekana nchini Tanzania?

Wageni waalikwa katika kipindi hicho walikuwa, mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema, John Heche na Katibu Mkuu wa chama Cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu

Niliamgalia kipindi hicho na nikiri wazi kuwa ni kipindi Bora kabisa kuanzishwa na luninga hapa nchini, ambapo viongozi hao wa kisiasa walipata wasaa wa kuelezea waziwazi uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan, wa kutoa ruhusa ya mikutano ya hadhara nchini, baada ya kupigwa marufuku, kinyume Cha Katiba yetu na Sheria za vyama vya siasa, mwaka 2016.

Wajumbe hao walijielezea Kwa uwazi kabisa bila woga wowote, ambapo niliona kuwa vyombo vya habari nchini, vimeanza kutoa habari Kwa uhuru bila kuogopa Kwa vituo hivyo kufungiwa.

Kama kipindi kama hicho kingerushwa katika utawala wa awumu a 5, chini ya Mwendazake, Hayati Magufuli, hakika kituo hicho kingefungiwa!

Walipoulizwa na mwendesha kipindi hicho, je wangependa Katiba mpya ipi iundwe?

Wote Kwa pamoja walisema ni Katiba mpya ya Jaji Warioba, ambayo ndiyo Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi.

Walichosisitiza waalikwa hao ni kuona nchi ikiongozwa Kwa mujibu wa Sheria zetu badala ya kuongozwa Kwa matashi ya kiongozi aliyeko madarakani!

Kwani ni wazi kuwa utawala wa awamu ya 5 ulipiga marufuku mikutano hiyo "kiharamu" Kwa kuwa hata Sheria zetu zinatoa uhuru huo wa mikutano ya hadhara Kwa vyama vya siasa.

Tunalazimika kutoa pongezi nyingi Sana Kwa EATV Kwa kuanzisha kipindi hicho Bora kabisa.

Niwahimize Televisheni nyingine kuandaa vipindi vya aina hiyo, badala ya Kila kukicha kuendeleza mavipindi yao ya kusifu na kumwabudu Rais aliyeko madarakani!
 
Uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu Sana, kwani umewekwa hata katika Katiba yetu tunayoiita ni "mbovu"

Katika ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, inasema hivi nanukuu "Kila mtu yuko huru kutoa maoni yoyote na kutoa mawazo yake, kutafuta, kupokea na kutoa habari zozote kupitia chombo chochote Cha habari, bila kujali mipaka ya nchi na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati na chombo chochote" mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom