Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,369
- 217,426
Nikiwa kama Raia wa Kawaida wa Tanzania nachukua nafasi hii kuipongeza Chadema kwa kukataa kushiriki Mkutano ulioiitwa wa wadau wa siasa ulioandaliwa na TCD , hii ni kwa sababu Mkutano huo pamoja na kuhudhuriwa na Rais wa nchi lakini HAUKUWA NA AJENDA , wala hata wajumbe wake hawakujua hata wanachoenda kujadili , ni kama waliburuzwa tu ili kukamilisha malengo ya waandaaji .
Wala hakuna mjumbe aliyehudhuria mkutano huo ambaye anaweza kutoka hadharani na kusema kilichojadiliwa akaeleweka , mpaka naandika hapa bado ni MARUFUKU KWA VYAMA VYA SIASA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA wala MAANDAMANO YA AMANI , miaka ya nyuma baada ya Mwl Nyerere kugundua umuhimu wa Demokrasia , aliwahi kuwaambia viongozi wenzake na wananchi kwamba CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI , Kukataza harakati za kisiasa kwa vile ccm haina ajenda, haikubaliki na wala haisaidii chochote kile , hata Jakaya Kikwete aliwahi kuwaasa wanaccm wenzake .
Ulikuwa ni mkutano wa kusikiliza hotuba za ufunguzi na zingine hotuba za kejeli kutoka kwa Dr Mahera , mwanaccm ambaye alishirikiana kwa 100% na Dr Magufuli kuvuruga uchaguzi wa 2020 kwa udi na uvumba , ikiwemo kufanya utekaji na mauaji ya wagombea na wafuasi wa vyama vingine , yaliyotokea Pemba , Lindi na kwingineko bado hayajasahaulika , Wala kikao hicho kilichokosa ajenda HAKINA HATA MAAZIMIO YOYOTE , ni heri hata kikao cha harusi ambako mwishoni kunaandaliwa hata zawadi ya bwana harusi , hiki kilikuwa kikao cha hotuba tu , anayejua ajenda zilizojadiliwa ama hata maazimio yake atuwekee hapa tujadili .
Ajenda kuu ya KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI haikugusiwa hata chembe , hizi ndio ajenda za nchi zinazoweza kuondoa maloloso yote ya akina Mahera na Kaijage na kuleta mwanzo mpya nchini , bla bla zozote hazitasaidia chochote .
Itaendelea ......