Hongereni mliovujisha mpango huu wa siri kubwa kwa wabunge (upinzani)

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,626
870
Kuna wadau labda mmeshanga sana ni nini kimetokea katika majadiliano bungeni kuhusu sakata la escrow, hasa baada ya kufika kifungu cha 7 cha kumuwajibisha muhongo etc

hii gemu ilichorwa siku nyingi sana tangu j3 wiki hii (master plan mkuu alikuwa chenge, wengine waliotoa mawazo ya kufanikisha hili walikuwa pinda, wassira, makinda, na kinana)

serikali iliona hakuna jinsi inaweza kumnasua muhongo, maswi na waziri mkuu katika uzembe huu na watuhumiwa hawa waliahidiwa kulindwa kimkakati

zaidi ya yote serikali ilishapima upepo kwa nyakati hizi za uchaguzi wa serikali za mitaa, na uchaguzi mkuu ujao ikaona si vyema kuruhusu serikali kuanguka tena maana yale makundi ya uraisi yanazidi kuhasimiana, na pia ikaona itatoa image mbaya sana kwa jamii

sasa plan ikawa kama ifuatavyo

sasa bwana job ndugai intelejensia ya chama ilionyesha kuwa si mtu strong anayeweza kuliendesha bunge na kulikuwa na hisia kuwa huenda anapokea maelekezo kutoka kwa wabaya wa serikali hii, kwahiyo ishu mbili zikafanyika faster 1. Kumuondoa job ndugai katika kiti, na kupewa karipio kali sana kwa kuruhusu majadiliano haya

2. Plan b hii ilikuwa kali sana serikali ikafanya mawasiliano na iptl, na kuwaamuru wanasehria wake kupeleka zuio mahakamani la bunge kujadili ishu hii, na zaidi ya yote barua hiyo ilikuwa on the way na ilifika dodoma, ndipo serikali wakawa wanajaribu kupima kina cha maji, lakini pia mahakama tena ingizwa katika kulitega bunge kwa kuwatisha kuwa hawapaswi kujadili suala hilo kisa liko mahakamani wakati shauri lililopo mahakami ni suala la madeni/madai,

lakini lengo hasa lilikuwa ni kumtumia makinda leo atumie kete ya kuruhusu demokrasia na kutoingilia mamlaka zingine kisa tayari kashaingilia suala la mahakama, na alipangiwa zaidi kuonyesha kuwa anaruhusu democrasia ili kupesha kuikwanza serikali kuu eti kisa kashaikwaza mahakama kwa kuruhusu majadala huu kuendelea. Lakini suala hilo lilikuwa limepangwa kabisa kuwa ionekane kuna mtifuaano wa kimamlaka kati ya bunge na mahakama

sasa leo ndio maana mama makinda karuhusu sana watu wajadiliane kwa kupitia azimio moja badala ya lingine na kujifanya anaomba sapport ya wabunge hasa wa upinzani. Na lile lililotokea kwa chenge kupewa nafasi ya kutoa muongozo na kushauri anavyoona hayo maazimio yakaeje hasa yanayogusa watendaji walioteuliwa na raisi, plan hiyo ilikuwa imepangwa kupigiwa chapuo na wakina mama mawaziri, ilikuwa ni plan, sasa information zikaliki zikamfikia mbowe , na mbowe akawajulisha watu wote wa karibu yake kuwa hapa tayari kuna mtego. Maana kama kila jambo la mtu ambaye hawakumchagua wabunge kuwaachia mamlaka za uteuzi maaana yake ulikuwa huwezi baadae kufuatilia tena kudai why fulani hakuwajibishwa.

Na ndio maana kila wakati spika alijifanya, kuwa ohh nataka jinsi ya kuweka hapa form ikaaje ili kuzuia kuingilia mamlaka zingine, eti kisa tayari anakesi kwa kuingilia mahakama, lakini plan hapa ilikuwa ni kumukoa muhongo, na waziri mkuu, maana huteuliwa na rais mbali ya kwamba waziri mkuu huthibitishwa na bunge, lakini kwa hari ilivyokuwa tangu juzi katika vikao vya ccm, tayari watu walishaadaliwa kumtetea mno waziri mkuu, maana serikali ilikuwa inaenda kuanguka, hasa ni visa vya madaraka vya wasaka urais. Chuki binafsi baina ya wabunge wa kamati ya pc toka ccm na wale wasio wajumbe. So mbowe alipenyezewa mchongo huu mwishoni kabisa, na kuamua kufanya aliyofanya.

Lakini plan ilikuwa ni kila mtu ambaye hakuchaguliwa na bunge basi bunge lishauri tu akawajibishwe na mamlaka za uteuzi baada ya uchunguzi, na suala hilo lingefika hadi mwakani bunge linavunjwa wakina muhongo, maswi, na pinda wangekuwa madarakani wakati woote huo;

sasa tayari kuna ugomvi mkubwa unaendelea kati ya wale wajumbe 19 wa pac walikuwa ni wa ccm, wanalaumiwa sana na ccm wenzao kwa kuandika yale mapendekezo na kumshambulia muhongo, na baadhi yao wameanza kutishiwa;

kwa jinsi hili suala la uchotwaji wa pesa hizi za escrow lilivyo mamlaka ya juu kabisa inalijua, na wamefaidika kabisa na mgao huu, ni mission nyeti sana ya serikali kupata pesa hizi kupitia kwa singa singa ili kutumika mwakani wa kati w chaguzi na kampeni;

kwa jinsi hali ilivyokuwa imepangwa hakuna cha kuwalaumu watu wa vyama pinzani, na pac yoote, ccm walidhani hii mission yao isingeliki; maana wakina ngeleja, au kagasheki waliwajibika kwa uzembe wa watu wengine na, si wao tu direct walienda kutenda makosa yale sasa iweje hawa wakina muhongo wakafikiriwe tena na rais, eti kisa tu wamegoma kujiudhuru.

Hongereni wabunge woote mlioamua kuangalia maslahi ya taifa.
 
Mi nadhani kama kweli ulikua unafahamu kuhusu huo mkakati ni either ungeuleta mapema hapa jamvini,ama ungeandika mtiririko wote na sio kuishia walipo ishia leo meani ulitakiwa kwenda beyond ya leo walipo ishia other wise ulichokipost hapa kila mtu aliyekua anafatilia bunge kakiona na wala hakuna kitu kigen hapo ulochokipost ni flow tu ya shughuli za bunge...
 
Ilinishangaza Chenge anaform mapendekezo!!"""
Zitto naye alikwishachoka.
Zitto hakuchoka alishagundua muda mrefu ndiyo maana alivyochangia Change baasi Zitto akakubali mapendekezo yote yapitishwe kwa hoja ya Chenge.
Then, tunarudi kwa wananchi wa UKWELI
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana nashauri akina Lissu wasirudi Bungeni
Why wasirudi? Hamjifunzi tu?
Kwani wasiporudi kuna kitakachosimama?
Wamegomea vingapi na wakapata faida gani?
WARUDI NA WAENDELEZE.
Hata hivyo hii sio UPINZANI Vs CCM

Ni PAC Vs MAFISADI
UPINZANI KUGOMEA NI KUIGAWA PAC.
 
Kwanini wasirudi bungeni mkuu mwanaume akimbii matatizo,anayakabili,waache waende wapambani,sisi wananch uku tunaona itakapo chezwa rafu tutaona na mwsho wa siku tutaamua..!!

Wakapane na watu waliofunga akili kwenye vyupi??

Mkuu ktk hali yoyote ile wakirudi watakwenda kupigwa bao la kisigino
 
Yani Zitto alisha maliza mchezo wote pale maana kwa huruma ya Rais kati ya Muhongo,AG au Waziri mkuu kuna mtu angeondoka!

Nilitamani wapinzani wote wange muelewa lakini haikuwa hivyo!
 
Why wasirudi? Hamjifunzi tu?
Kwani wasiporudi kuna kitakachosimama?
Wamegomea vingapi na wakapata faida gani?
WARUDI NA WAENDELEZE.
Hata hivyo hii sio UPINZANI Vs CCM

Ni PAC Vs MAFISADI
UPINZANI KUGOMEA NI KUIGAWA PAC.


Kwa hatua iliyofikia suala la ESCROW imedhirika ni udhalimu na ufisadi umefanyika so hakuna asiyejua na kwa vyovyote JK hawezi mrudisha Muhongo Wizarani.
 
Kwanini wasirudi bungeni mkuu mwanaume akimbii matatizo,anayakabili,waache waende wapambani,sisi wananch uku tunaona itakapo chezwa rafu tutaona na mwsho wa siku tutaamua..!!
dawa kukomaa nao tu si kutoka.....kitendo cha kutoka kitawafanya wapitishe maazimio ya......pale wakileta upuuzi wao ni kusimama tu na kuimba.
 
Yani Zitto alisha maliza mchezo wote pale maana kwa huruma ya Rais kati ya Muhongo,AG au Waziri mkuu kuna mtu angeondoka!

Nilitamani wapinzani wote wange muelewa lakini haikuwa hivyo!

no way, no way.. hujapata hasa hii ishu ilipangwaje, ccm wanajua sana kujipanga hata washambuliwe vipi wnaweza kujibu mapigo, na hili lilikuwa ni pigo lingine takatifu kwa woote waliokuwa wakitaka kuona watu wakiwajibika.. soma tena kwa makini mkuu
 
Kwa hatua iliyofikia suala la ESCROW imedhirika ni udhalimu na ufisadi umefanyika so hakuna asiyejua na kwa vyovyote JK hawezi mrudisha Muhongo Wizarani.


duuuhh.. dakika hizi jk abadilishe timu?? dakika hizi mkuu....??/
 
Mi nadhani kama kweli ulikua unafahamu kuhusu huo mkakati ni either ungeuleta mapema hapa jamvini,ama ungeandika mtiririko wote na sio kuishia walipo ishia leo meani ulitakiwa kwenda beyond ya leo walipo ishia other wise ulichokipost hapa kila mtu aliyekua anafatilia bunge kakiona na wala hakuna kitu kigen hapo ulochokipost ni flow tu ya shughuli za bunge...

Brother,
hawa wameshafilisika muda mrefu katika siasa za bongo. Wahuni wakubwa hawa.

Sasa we ona uzi huu wakidada kabisa huyu jamaa anatiririka tu. Yaani kanakili "hansard tupu"
WAKAE VYEMA KISAIKOLOJIA. HAWAWEZI KUTULETEA FUJO TUKAWA KIMYA. RAIA(sisi) tuko makini,na tutawaadhibu tu. UKAWA wamelowa!
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom