Hongereni Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngorongoro, Arusha!!

Mau Mau

JF-Expert Member
Dec 30, 2012
673
478
Wadau Heshima Kwenu,
Mnyonge mnyongeni Haki yake Mpeni, Mimi nimekuwa ni mtu nisiyevutiwa mara nyingi na utendaji kazi wa Jeshi letu la Polisi, mwaka 2016 nilienda LOLIONDO wilayani Ngorongoro kikazi hali ilikuwa mbaya mno, Ninaposema mbaya ni MBAYA hatari!!

Watu walikuwa wakitekwa hovyo, Watalii wametekwa mno, mchana kweupe Risasi zinarindima Hafu unakuta wamepora Laki moja tu, kule ilikuwa ikifika Usiku unakosa uhakika wa kufika asubuhi.

Nimeenda Juzi nikawa na hofu ile ya Awali, nimekuta hali ni salama, nikaambiwa kuna kikosi kazi kikishirikiana Na Jeshi la Polisi Loliondo wamefanya kazi kubwa na wanewakamata wahalifu wengi mno na mabunduki yao.

Sikuwahi kuona wananchi wakiwasifu askari kiasi kile.Sasa hivi hata ukisafiri una uhakika wa kufika salama tofauti na zamani unasafiri huku simu na vihela vyako umevificha chini ya Seat yako.
Wito wangu Jeshi letu kwa weredi huo mlioutumia huko Loliondo Hebu mfanye hivo na maeneo mengine, wananchi wasipoonewa wanawapenda sana hasa mnapotimiza majukumu yenu.

Muachane kujihusisha na wanasiasa na kule nasikia wanaharakati ni wengi laana Hafu wote wana interest tofauti kuinyonya hiyo wilaya iliyojaaliwa vivutio vingi vinavotegemewa kwa mapato!!!

Kwa Hilo Viva Jeshi La Polisi
 
Hii post obvious imekuja baada ya harakati za makundi ya haki za kibinaadamu kuanza kumulika jeshi la Polisi Loliondo kufuatia vitendo visivyo vya kibinadamu walivyofanyiwa vijana watatu wa Ngorongoro waliosemekana kumuibia mzungu.

Picha za majeruhi wale zilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii na watu walisikitishwa sana na utesaji huo usio kuwa na hata chembe ya utu.

Ikumbukwe pia kuwa watu wengi huko wamekuwa wakibambikiziwa kesi za ajabu ajabu na hao hao wanaosifiwa na mleta mada
 
Kile kikosi kazi tena cha vijana wadogo kimefanya kazi iliyotukuka
 
Back
Top Bottom