Hongereni CHADEMA, mnaishi kama familia kwenye shida na Raha; CCM ukipata janga unaondolewa kwenye ukoo

Solidarity ilipo Ndani ya wana Chadema nikubwa Sana. Leo nimefanikiwa kufika mahakama aliyofikishwa Mbowe na wenzake. Nimependa kuona Kwamba Hawa ndugu muda wa chakula wanakula pamoja bila kijali chama, mke wa mtuhumiwa kafika mahakama wamemchangia nauli, wakati watuhumiwa wanaondoka saa kumi na moja nyimbo za bashasha zinaimbwa. IL sense ya upendo unaiona wazi, sense ya umoja unaiona na spirit yakupambania haki unaiona.

Kwa upande wa pili CCM ukipata tatizo wote wanakukataa; walijitenga na Nape, Januari wakamkimbia Makonda, Sabaya kakosa msaada yeye na nduguze jela huko na juzi wamemtenga Mzee Ndugai. Unapozungukwa na watu ambao wao ni ndugu zako ukiwa na madaraka na ukiyapoteza siyo nduguzo yuo need to watch out.

Natambua kwanini wote wanaopata matatizo wanatengwa; ni kwa sababu mfumo wao ni sogea nikae. Na nikikaa nakaa na watu wangu sikai alone.

That solidarity Ndani ya Chadema natamani iwe solidarity ya Taifa. Lakini hawana solidarity kwa kila mtu wanasolidarity kwa anayeonewa. Nape alionewa wakamsemea, Mo akapata matatizo wakamsemea, ndugai kakosea utaratibu walisema so huu umoja na nguvu ya Chama hiki utakifikisha mbali.

Changamoto ya CCM ni Kwamba watu wao wakiwa wanakosea awawaambii, wakitumbiliwa pia inawawia vigumu kuwatetea Kwa sababu wanajua hawa ni waovu.
Hatuwezi kujenga taifa lakusubiri wakubwa watufundishe namna ya kuwaza. Lazima CCM iruhusu kuzalishwa kwa wanachama wanaoweza kupinga uovu kama wanavyofanya Chadema. Kinyume chake utegemezi wa dola utakuwa mkubwa sana na dola ikichoka lazima chama life
Umoja wetu ni nguvu yetu Umetuwezesha kuvuka milima na mabonde. Bado twapendana.

Ukitazama nyumba ya pili walichofanyiwa akina Polepole? Sabaya, Makonda, spika na wenzake hawaamini yaani
 
Back
Top Bottom