Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Niliposema humu kuwa:CCM hamna sifa ya kumuunga mkono Rais Magufuli katika suala la madini nilimaanisha. Nashukuru kuwa CCM mlinielewa na mmeufanyia kazi ushauri wangu.
Hadi sasa, kama chama, mmejitenga mbali na utendaji wa Rais Magufuli na Serikali yake katika kulinda rasilimali za Tanzania, hasa madini. Mmetambua kuwa nyinyi ndiyo wakosaji wa kwanza na hamna moral authority ya kupongeza juhudi za Rais Magufuli.
Kama CCM, mmezidiwa kete hata na Bunge ambalo limejitokeza kumpongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa juhudi za dhati za kulinda rasilimali zetu kama nchi. Hadi sasa, CCM hamkutoa taarifa rasmi ya kumpongeza Rais. Hakika, mmefanya vyema.
Mmejitambua na kuyatambua makosa yenu. Kama chama, majuto yenu yanaonyeshwa na ukimya wenu katika kinachoendelea. Kudos CCM kwa ukomavu wa kisiasa mliouonyesha!