Hongera zenu nyingi kwa kazi nzuri mnayoifanya

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,029
Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Sababu za ‘mbongo’ St Francis zatajwa
Deogratias Mushi
Daily News; Saturday,February 02, 2008 @19:02

MAZINGIRA mazuri ya kusomea, ushirikiano kati ya wazazi au walezi na utawala sanjari na umakini wa uongozi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Francis ya Mbeya wakati wa kudahili watoto wanaojiunga na shule hiyo ni miongoni wa sababu zinazofanya shule hiyo iendelee kung’ara katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne, imefahamika.

HabariLeo Jumapili pia imebaini kuwa, utaratibu wa shule hiyo kuzingatia uwezo wa mtoto katika masomo ya hisabati na Kiingereza wakati wa kufanya udahili wa watoto wanaoanza kidato cha kwanza unaiwezesha shule hiyo kupata watoto wenye uwezo mkubwa darasani hivyo kuwa rahisi kwao kufanya vizuri katika mitihani.

Katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa Alhamisi wiki hii kwa mara nyingine tena shule hiyo iliendelea kuwa ya kwanza kitaifa na ikaweka historia baada ya wasichana 10 bora kitaifa kutoka katika shule hiyo. Wasichana walioiwezesha shule hiyo ijivunie ushindi huo sambamba na wazazi na walezi wao ni Violet Rukambeiya, Lilian Kakoko, Gloria Samwel, Jackline Seni na Mary Mrosso.

Wengine ni Caroline Yambesi, Gloria Kahamba, Doreen Bateyunga, Lilian Mhamilawa na Winnie Muangi. Mkuu wa Shule hiyo, Sista Juliana DeSouza alisema kuwa, miongoni mwa mambo yanayoiletea ushindi shule hiyo ni ushirikiano wa walimu na wanafunzi sanjari na umakini wakati wa kudahili wanafunzi.

Kwa mujibu wa Sista DeSouza, kabla ya mwanafunzi kuchaguliwa kujiunga na shule hiyo, huwa kuna mawasiliano kati ya utawala wa shule na wazazi au walezi ili kila upande ufahamu majukumu yake katika mchakato wa kumpatia elimu mwanafunzi husika. Alisema, endapo mwanafunzi anapata tatizo lolote kila wakati kuna walimu wanaokuwa tayari kuwasaidia na hata wanapokuwa katika kazi za nje wanakuwa na mwalimu.

Kwa mujibu wa mkuu wa shule, motisha, kujituma kwa walimu na wanafunzi, nidhamu na dhamira ya walimu na wanafunzi vinafanya shule hiyo iendelee kung’ara. Alisema, walimu na wafanyakazi wengine wa shule hiyo wanapata motisha kwa namna mbalimbali hivyo kufanya watumie muda wao kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

DeSouza alisema, shule hiyo inayomilikiwa na watawa wa Mtakatifu Charles Borromeo wa Kanisa Katoliki kutoka Ubelgiji ina mazingira mazuri ya kusomea, ina maktaba inayojitosheleza na maabara yenye vifaa vyote vinavyohitajika kufanya majaribio mbalimbali. “Uje uone shule ilipo, sisi tunawapa wanafunzi misaada yote wanayohitaji ili kuwawezesha wazingatie masomo yao,” alisema Sista DeSouza.

Shule hiyo ina wanafunzi 360, walimu 25 na watawa wanaofanya kazi kubwa kama wanavyofanya wenzao kutoka shirika hilo hilo waliopo katika shule za sekondari za Loyola ya Dar es Salaam na Shule ya Msingi ya Mtakatifu Charles iliyopo mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa DeSouza, kwa ujumla wanafunzi wa shule hiyo hupata elimu katika muda wa kawaida wa kuwapo madarasani, lakini kuna wakati hujigawa katika makundi madogo ya kujadili mambo mbalimbali kwa kusimamiwa na walimu na kwamba wanafunzi hufundishwa pia namna ya kutumia muda ili waelewe, wafanye nini na wakati gani.

Tofauti na shule nyingi nchini, wanafunzi wa shule hiyo hupata pia huduma ya ushauri ili kuwasaidia katika maendeleo yao kijamii, fani, kitaaluma, mipango ya kusoma, migogoro, udhalilishaji na Ukimwi. Alisema, wakati wa kujisomea usiku hadi saa nne kamili usiku, mtawa hutembelea madarasa yote kuhakikisha kwamba kuna utulivu ili wafanye maswali waliyopewa na kazi zao nyingine walizopewa za kitaaluma.

Alisema, hata mwishoni mwa wiki na wakati wa likizo shule hiyo huwa na program maalumu ya kujifunza na kwamba wanafunzi husaidiwa kwa namna ya pekee kutegemea na uwezo wa mwanafunzi husika.

Kuhusu chakula alisema, wanafunzi wa shule hiyo wanakula vyakula vya kawaida vya Kitanzania na wakati wa asubuhi hunywa uji uliopikwa kwa unga wa mahindi. Katika matokeo ya Mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, shule hiyo ilitoa mwanafunzi bora kitaifa, Evelyne Lupimo, na ikatoa wanafunzi watatu kati ya sita bora kitaifa akiwamo Innes Muganyizi, na Erica Kafwimi. Lupimo alipata alama A katika masomo yote aliyofanya, na aliungana na wenzake 11 wakiwamo sita kutoka shule za serikali kupongezwa na viongozi wa serikali Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
kinachofanya tofauti na seminari, seminari wanadhali sala tu ndiyo zinazomfanya mtu ashinde wakati hawa wanajua kuwa vyote vinaenda pamoja

pili seminari lengo lao ni kujiandaa kuwa padre hata kama una pasi ya kawaida wakati hawa lengo kuuu ni kumjengea maisha yake ya baadaye.

tatu seminari wanasoma kwa presha kuofia kufukuzwa huku hawa wanasoma kwa malengo ya kuibuka the first lady of the year.
 
Back
Top Bottom