Hongera Yericko: Ikulu ihamishwe ndani ya miezi 18

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Huu ni ushauri alioutoa #Yericko Nyerere mwana JF mwenzetu mwaka jana, kuwa Ikulu ihamishwe ndani ya miezi 18 kuanzia tarehe 1/1/2015 ila Lumumba walimbeza sana. Leo rais Magufuli kaliona hilo.

Soma maoni yake hapa.

Ikulu (State House) ya nchi ya Tanzania lijengwa kwa namna ya kipekee na Wajerumani mwaka 1891 na gavana wa Kihuni Chakosi Dikwe na kutumika kama ngome ya gavana. Iliharibiwa wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia. Baada ya vita ya kwanza ya Dunia Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Waingereza na hapo ngome hiyo (state house) iliitwa Government House na ilijengwa tena mwaka 1922 ambapo gavana wa Kiswahili Sir Unapima Mkali alipochukua utawala. Majengo hayo yamejengwa kwa ubora wa pekee na ni ya kihistoria kwani yalikuwa ni Ngome za magavana.

Makazi haya ya rais nchini Tanzania yaliko Kaskazini Mashariki mwa jiji la Dar katika nyuzi 2 kutoka usawa wa bahari ndio makazi ya kiongozi wa nchini yaliyohatarini zaidi kuliko makazi ya rais yeyote barani Afrika kwa sasa,

Mathalani, kutoka lango kuu la ikuu kwenda mpaka chumba anacholala rais ni mita 63.2. Hii inaonyesha kuwa Rais wa nchi hii hayuko salama hasa linapokuja suala la artificial security,

Eneo la ikulu hii ni dogo, halizidi eneo la mraba 13,200 Ambacho ni kipimo kidogo kabisa kwa dunia ya leo kwakuweka makazi ya kiongozi wa nchi.

Upande wa Kaskazini mita 10 kuna bahari yenye kina cha mita 18 hadi 33, hii inaweza kuruhusu nyambizi ndogo zenye makombora ya masafa mafupi kuifikia ikulu, ulinzi wa eneo hili ni natural security jambo ambao linatia shaka zaidi usalama wa rais wetu,

Upande wa mashariki mwa Ikulu kuna majengo manne yenye urefu kati ya mita 30,43 na 56 ambayo ni wizara ya ardhi, wizara ya utumishi, mnara wa kuongozea meli, na chuo cha ukarani. Katika itifaki ya kiusalama majengo haya ni hatari kubwa mno kwakuwa yapo umbali wa mita 40 hadi 160 tu, eneo hili laweza kutumiwa na walenga shabaha kuelekea ikulu, hii inatokana na sehemu kubwa ya vyumba vya shughuli za rais kuelekezwa upande huu wa mashariki, mfano, chumba cha mazozi, Choo na bafu na chumba cha siri cha mikutano (PU),

Sniper yeyote akitumia moja ya majengo ya eneo hili anaweza kumuua kiongozi wetu aliye ndani ya bafu,choo ama chumba cha mikutano tena bila idara za usalama zilizo ndani ya ikulu kutambua mlenga shabaha huyu alipo mpaka uchunguzi wakutumia carbon fire missile ambao kimsingi sniper atakuwa keshatokomea.

Eneo hili pia lina soko la samaki ambapo kiafya ni hatari zaidi kwakuwa moshi unaotokana na ukaangaji wa samaki hujaa ikulu waweza dhani mapishi hayo yanafanyika ndani ya ikulu hii.

Upande wa kusini mwa ikulu kuna majengo matatu marefu, Wizara ya fedha, Benk kuu na magereza eneo hili linatazama lango la ikulu, majengo haya yapo umbali wa mita 200 na 240, japo kuwa majengo haya ni ya serikali na yanatumiwa na serikali lakini kiusalama haya hayafai kuwepo maeneo haya, ikiwa adui yeyote mlenga shabaha za mbali (sniper) atatumia majengo haya basi shabaha yake itakuwa ni nyakati za rais kuingia ama kutoka ndani ya ikulu hii ya Dar.

Upande wa Magharibi lipo jengo moja ambalo ni refu linalokadiriwa kuwa na ghorofa 18, jengo hili lipo umbali wa mita 370 kutoka chumba cha kulala rais ndani ya ikulu hii, na katika upande huu wa Magharibi mwa ikulu ndiko chumba cha cha kulala rais kiliko maarufu kama DDO,

Jengo hili refu ni eneo la kibiashara na makazi ijapokuwa sehemu ya makazi ya juu kabisa ya ghorofa yamechukuliwa (yamepangishwa) kwa maafisa usalama wa serikali lakini hilo haliondoi uhatari uliopo kutokana na uwepo wa majengo haya marefu pembezoni mwa Ikulu hii,

Mlenga shabaha yeyote mwenye nia mbaya na taifa hili ikiwa atatumia jengo hili basi shabaha yake itakuwa ni wakati rais yupo chumbani na shabaha yake kuu itakuwa kichwani kwenye usawa wa dirisha la magharibi.

Haya ni vema tukayasema ili kuliweka taifa mahali pausalama zaidi kutokana na taifa liendako, ikumbukwe kuwa miaka michache tu iliyopita eneo hili la ikulu halikuwa na uzio kabisa na watu walikuwa wakijatiza langoni kabisa kule wakitoka feri kwenda Hospital ya Saratani. Lakini kadiri mageuzi ya nchi yanavyokwenda mambo yamebadilika sasa angalau ukifika hata getini kuna artificial security kuliko natural security,


Sasa Tanzania tunaingia kwenye nchi zennye uchumi mkubwa kutokana na raslimali gesi tuliyonayo, ambayo kwa sasa inakadiriwa kuwa Tz ina wingi wa gesi yenye futi za ujazo cub mita 9.4 trilioni, kiwango hiki ni robo tatu ya gesi izalishwa Urusi, na bado utafiti zaidi bado unaendelea.

Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na gesi nyingi kwa sasa ambapo kwa kiwango kulichogunduliwa tu inauwezo wa kuihudumia Italia, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza na kukidhi mahitaji yao kwa miaka mia moja mbele.

Kaimu mkuu wa shirika la gesi nchini Urusi Korov Matoriv anasema, ikiwa gesi iliyogunduliwa nchini Tanzania serikali ya nchi hiyo ikiandaa sera na kuzifanya kuwa kwa maaslahi ya nchi hiyo basi Tanzania itakuwa nchi yenye uchumi mkubwa kwa miaka 15 tu kuanzia 2015,

Katikati ya neema hii ya utajiri ndipo viongozi wa kitaifa huhitaji ulinzi maradufu na chuki za nje huongezeka huvi ulinzi wetu ukiwa legelege tutarajie assassination kwa viongozi wetu toka mataifa makupe ya kimagharibi hasa CIA na M16,

Kwa sasa njia mwafaka ni kuhamisha ikulu hapa ilipo na kuipeleka Dodoma ikiwa dhamira ya uhamiaji Dodoma bado ipo, lakini kama Dodoma bado ni kizungumkuti basi sehemu mujarabu na yenye uwiano mzuri wa protokali za kijasusi na kiulinzi basi ni Kigamboni.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Rais ajae 2015
 
Sio kila sababu lazima isemwe au iwe wazi.
Wacha kujiundia sababu

Ingekuwa sababu ni usalama wa ikulu ingehamishwa yenyewe tu.

Msome hata yeriko anatembea kwenye hoja ya serikali kuhamia dom. Au kama aihami basi ipelekwe kigamboni

Acheni kutuwazisha kitoto toto hapa.
 
Napata shida kidogo kwa maneno ya yericko, ni kitu gani ambacho rais wa tanzania anahofia maisha yake kama kweli anachotenda mbele ya watu wake ni cha haki, ni kitu gani hasa ambacho tunahofia usalama wa mkuu wa kaya? hivi karubuni tumesikia nchi za ufaransa na marekani zikivamiwa na vikundi haramu, ambazo ni nchi kubwa kwa eneo wingi wa watu lakini pia kiulinzi na usalama, kama nchi kubwa kama hizo zilishindwa kuzuia vikundi hivyo kufanya unyama huo, tanzania sisi tutawezaje? Nafikiri maneno anayosema ndugu yericko ni ya miaka ya 70s kipindi ambacho tekinolojia ilikuwa ni ya chini sana, lakini kwa dunia ya leo ambayo tekinolojia imekuwa kwa kiwango kikubwa sidhani kama tanzania inaweza kujifanya kuwa kama kisiwa, kwamba haiwezi kufanywa lolote. Kikubwa magufuli anatakiwa awathibitishie watanzania sababu za serikali yake kuhamia mji wa dodoma, je ni zile za kipindi cha mwalimu za miaka ya 70s ambazo hazina uhalisia kwa sasa au kuna nyingine, kama kuna nyingine ni wakati sasa wa kuzileta tuzipime tuone kama zina mashiko ama la, na siyo tu kusema ya kuwa mchakato ulianza miaka ya 70s hadi leo tupo kwenye mchakato. Yericko unaweza kuwa na mawazo mazuri lakinu jaribu kuyapitia tena hayo mawazo yako uone kama yanaendana na hali ya sasa
 
Hapa ndiyo pa kujadili!!




Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na gesi nyingi kwa sasa ambapo kwa
kiwango kilicho gunduliwa inauwezo wa kuihudumia
Italia,
Ujerumani,
Ufaransa
Uingereza
na kukidhi mahitaji yao kwa miaka mia moja mbele.
 
Acha utoto mkuu, kwani raisi kahama kwa sababu za kiusalama ama kutimiza kauli ya serikali kuhamia dodoma.
Nyambizi huwa zinakuja usiku kumchungulia hadi ndani ya mjengo, si unajua jwtz hawana uwezo wa kununua hata kanyambizi kadogo ka kulinda Bahari chini kwa chini, ni hatari ikulu kukaa karibu na Bahari hasa ukizingatia kuwa jeshi la marekani lipo mombasa na lina Nyambizi wengi ambao wanaweza kuja usiku na kuchungulia ikulu na kupiga picha za kila aina.
 
Wacha kujiundia sababu

Ingekuwa sababu ni usalama wa ikulu ingehamishwa yenyewe tu.

Msome hata yeriko anatembea kwenye hoja ya serikali kuhamia dom. Au kama aihami basi ipelekwe kigamboni

Acheni kutuwazisha kitoto toto hapa.
"Ikulu haiko salama" Magufuli.
 
Back
Top Bottom