Hongera Waziri Prof. Mbarawa, Juma Aweso na Prof. Kitila Mkumbo kwa kuinyosha wizara ya MAJI

Mligo Augustino

Senior Member
Nov 29, 2017
126
278
Wizara hii nyeti kwa wananchi ilikuwa hovyo sana. Hawa jamaa wamepambana sana kuhakikisha inakuwa na tija kwa Taifa. Hongereni sana. Msilegeze kamba. Makandarasi wa hovyo fukuza. Mainjinia wa hovyo fukuza. Hii ndo dawa ya wizara hii. Wizara hii sasa inanyoka na kuleta matumaini kwa wananchi.Miradi iliyokuwa haitoi maji, sasa maji yanatoka.
 
Mbona wanashindwa kulipa made ni kwa walukwisha kukabidhi miradi na inatumika vizuri tu?
 
Kitila Mkumbo naye shaingia kwenye mkumbo?
Pale wizarani kuna watu wenye long time entreched interests.

Pamekuwepo makatibu wakuu wengine kabla ya Mkumbo, lakini inaelekea waliingia mkumbo wa ulaji wa fedha za miradi.

Haingii akilini fedha za miradi zinapitishwa na bunge, zinafika wizarani toka wizara ya Fedha, lakini kwenye miradi fedha hazifiki.
 
Naomba kujua miradi ambayo ipo kwenye hatuq za awali.
ki utekelezaji!
na pia bonde gani lipo kwenye miradi au ufadhili
 
Wizara hii nyeti kwa wananchi ilikuwa hovyo sana. Hawa jamaa wamepambana sana kuhakikisha inakuwa na tija kwa Taifa. Hongereni sana. Msilegeze kamba. Makandarasi wa hovyo fukuza. Mainjinia wa hovyo fukuza. Hii ndo dawa ya wizara hii. Wizara hii sasa inanyoka na kuleta matumaini kwa wananchi.Miradi iliyokuwa haitoi maji, sasa maji yanatoka.
Prof Mbarawa alipelekwa kwenye wizara hii na JPM kwa sababu maalum. Yule mzee ambaye sasa yupo mawasiliano, alishindwa kwenda na uhalisia wa wizara ya maji.
Prof anapiga kazi na hapendi longolongo.
 
Prof Mbarawa alipelekwa kwenye wizara hii na JPM kwa sababu maalum. Yule mzee ambaye sasa yupo mawasiliano, alishindwa kwenda na uhalisia wa wizara ya maji.
Prof anapiga kazi na hapendi longolongo.
Tatizo ni la kitaalam dhidi ya ufisadi pale Wizarani.
Haijalishi mtu gani anaingia pale.

Bila kuanzisha Agency ya Project Execution and Management, kama walivyo fanya Wizara ya Ujenzi kuanzisha TANROADS, fedha zitaendelea kuliwa na mafisadi wizarani humo.
 
Prof Mbarawa alipelekwa kwenye wizara hii na JPM kwa sababu maalum. Yule mzee ambaye sasa yupo mawasiliano, alishindwa kwenda na uhalisia wa wizara ya maji.
Prof anapiga kazi na hapendi longolongo.
Wengine tukadhani maskini Mbarawa ndio hivyo aanza kuteleza, kumbe ni kinyume chake? Huyo Profesa namkubali kwa utulivu wake, ndio maana namweka kwenye watu wenye 'potential' ya urais Tanzania.

Achape kazi.

Aaah, nili'quote' bila kuangalia. Kumbe ni wewe? Potelea mbali, kwa hili tutakubaliana.
 
Back
Top Bottom