Hongera waziri Nahodha kwa maamuzi magumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera waziri Nahodha kwa maamuzi magumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LENGIO, May 7, 2012.

 1. LENGIO

  LENGIO JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 1,033
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Nampongeza aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Mh Nahodha kwa maamuzi magumu aliyotoa kwa wezi wa madini yetu,wakenya wenye urai wa nchi mbili waliokuwa wanabebwa na na mzindakaya na mwanae.

  Waziri Nahodha ametoa amri divis antony ngoo aondolewe haraka na baba yake Antony mraga ngoo achunguzwe kwa kina na achuliwe hatua kali.sasa hivi wakenya hao wako dar kujaribu kuwahonga viongozi wetu ambao sio waadifu ili wawapatie urai.

  Huyo davisi kwanza alistaili kifungo kwanza amegushi cheti cha kuzaliwa pili paspoti ya tz tatu kusafirisha madini nje ya nchi kupeleka kenya. Tunao ushaidi kutoka kijiji anachosema amezaliwa mzee antony ngoo toloha kwamba hawamjui hata hapo kahe hawamjui hata mzee wa ukoo wa mwanyika ukoo antony ngoo anasema ni ukoo wake.

  Watz tumechoka kuibiwa na wakenya. madereva wa utalii wa tanzania kenya hawaruhusiwi huku wanaingia hadi migodini.serikali ikawashindwa tutatumia nguvv ya umma. sourse mchimbaji mireran
   
 2. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Uamuzi mgumu upi?
  mbona unasema bado wako huru DSM wanafanya jitihada za kuhonga ili wapate uraia?
  Halafu Ongeza juhudi kwenye lugha ya kutoa taarifa kwa kuandika.
  Inabidi mtu aangalie mdomo wako unavokwenda ndo ajue unamaanisha nini!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Jifunze kiswahili! Huo sio uamuzi mgumu!
   
 4. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  hata mi nimekomaa nikisoma kuona uamuzi mgumu lakini holaa!! huo niuamuzi wa kawaida sana..
   
 5. The Eagle2012

  The Eagle2012 Senior Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  ha ha ha ha ha,Kaka reporting skillz ni tunu ambayo si kila mja kakabidhiwa!!
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Amefanya maamuzi magumu au amefanya wajibu wake?
   
 7. kijenge

  kijenge Senior Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Mwacheni huyo ni mmasai kwanza kajitaidi sana.nimesoma kwenye mwananchi ya leo 7.5 2012 nimeona hiyo habari inaoneka hao wakenya wamewatesa sana maana naona kaandika kwa jaziba sana ndio maana.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Na hii ndiyo alitakiwa kuandika. Maamuzi magumu yana maana pana na ya msingi sana!
   
 9. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  unaelewa maana ya uamuzi mgumu?hilo alilolifanya ni wajibu wake wa kila siku
   
 10. Ronn M

  Ronn M JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 1,283
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wala sijaelewa alichoandika
   
 11. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nahodha (Captain)

  Life is all about change and misery is an option

  Kuwa nahodha lazima uwe tayari kukabiliana na mabadiliko na pia husuni ni chuguo.

  ukiwa na sifa hiyo basi hushindwi mtu kutoa maamuzi magumu hata kama utapatwa na msukosuko.
   
 12. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kwa uandishi huu sidhani kama nitakuwa na lakuchangia, kwaheri
   
 13. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sijaona maamuzi magumu hapo, au kwa mtazamo wako ndio maamuzi magumu? Analipwa kwa kazi gani kama sio hiyo?
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu umeshachangia tayari
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu huo ndo uamuzi mgumu naunga mkono kwa sababu nani ndani ya magamba anaweza kufanya hayo??
  Ndani ya magamba ni rushwa tuu imetawala! Huo ni ulaji mzuri tuu!
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu huo ni uwajibikaji wa kiongozi mahali popote. si kila kitu ni maamuzi magumu.
  Nilitegemea Nahodha angechukua maamuzi magumu wakati wa mauaji ya watu wasio na hatia Arusha na North Mara. cha ajabu hakuchukua maamuzi magumu, na wala hakuenda kwenye eneo la tukio.
  Matokeo yake alitoa tamko akiwa ofisini kwake Dar.
  Hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi magumu ndani ya ccm zaidi ya Lowassa.
  Wengine wote waliobaki hawana dhamira njema na nchi yetu.
   
Loading...