Hongera watanzania kwa kufanya imani chanzo cha mapato

Invarbrass

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
504
111



Nimegundua watanzania ni wa janja sana. Baada ya kushuhudia makanisa ya maombezi yanachuma pesa kama mchezo vile tena bila kulipa kodi wameamua nao kutoka kindoto. Ubunifu mkubwa uliopo ni kudhibiti soko maana dawa anatoa muotaji tu na simwingine(hati miliki?).Pili dawa lazima itolewe katika eneo la makazi ya muhusika. Faida ni kuwa baada ya mwaka loliondo itakuwa bonge la mji.(rejea mipango inayoendelea), babau ndani ya miezi miwili ana hera ambayo professor wa chuo hawezi kupata akistaafu. So Tabora, Mbeya loliondo Marangu na sehemu nyingine watakapoibuka waotaji tutashuhudia maendeleo ya mihundo mbinu ya hali ya juu. Huu utaratibu nimeupenda maana hata serikali yetu isiyo toa kipaumbele kwa mipango ya maendeleo inathamini ndoto. Si tunaona wataalamu wanakwenda kufanya utafiti wa mti wa babu, je asingeota wangeenda lini? Tuombe watu wengi waote dawa serikali iende kuboresha mazingira. Mwisho wa siku nchi yetu yote itaendelea tena kwa muda mfupi. Hongera waota ndoto maana mna faida kuliko hata wa bunge​
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom