Hongera watanzania kwa kufanya imani chanzo cha mapato | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera watanzania kwa kufanya imani chanzo cha mapato

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Invarbrass, Apr 1, 2011.

 1. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimegundua watanzania ni wa janja sana. Baada ya kushuhudia makanisa ya maombezi yanachuma pesa kama mchezo vile tena bila kulipa kodi wameamua nao kutoka kindoto. Ubunifu mkubwa uliopo ni kudhibiti soko maana dawa anatoa muotaji tu na simwingine (hati miliki?)

  Pili dawa lazima itolewe katika eneo la makazi ya muhusika. Faida ni kuwa baada ya mwaka Loliondo itakuwa bonge la mji. (rejea mipango inayoendelea), babu ndani ya miezi miwili ana hela ambayo professor wa chuo hawezi kupata akistaafu.

  So Tabora, Mbeya Loliondo Marangu na sehemu nyingine watakapoibuka waotaji tutashuhudia maendeleo ya miundo mbinu ya hali ya juu. Huu utaratibu nimeupenda maana hata serikali yetu isiyo toa kipaumbele kwa mipango ya maendeleo inathamini ndoto.

  Si tunaona wataalamu wanakwenda kufanya utafiti wa mti wa babu, je asingeota wangeenda lini? Tuombe watu wengi waote dawa serikali iende kuboresha mazingira. Mwisho wa siku nchi yetu yote itaendelea tena kwa muda mfupi. Hongera waota ndoto maana mna faida kuliko hata wa Bunge.
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Picha wapi kaka?
   
 3. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145

  Serikali iliyofilisika kimawazo lazima itegemee ndoto........Loliondo ni ushahidi tosha kuwa tunaongozwa na vilaza!
   
 4. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mimi naomba usiku na mchana Mungu anioteshe ndoto ili kwetu kijijini pabadilike
   
 5. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hivi nichukuwa yale maji nikaweka kwenye tank la mafuta gari yangu si itapona kabisa???
   
 6. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa
  sababu, ukimkiri Yesu
  kwa kinywa chako ya kuwa ni
  Bwana, na kuamini moyoni
  mwako ya kuwa Mungu
  ...alimfufua katika wafu,
  utaokoka. Kwa kuwa, kila
  atakayeliitia Jina la Bwana
  ataokoka. Warumi 10:9,
  13.
   
Loading...