Hongera wasomi hizi ni alama za nyakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera wasomi hizi ni alama za nyakati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kweleakwelea, May 23, 2011.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  kwa wale wanaopita pita mjini dodoma leo ni masimulizi ya jinsi FEDHA na UBABE wa siasa umeshindwa kufanya kazi katika jamii ya wasomi......

  pamoja na matumizi makubwa ya rasilimali yaliyotumika na CCM na mfumo wake, kuchakachua kazi ya tume ya uchaguzi, na kumpigia kampeni nzito ya aina yake mgombea wake Bwana Kwagilo na mgombea mwenza wake ambaye ni mke wa Mheshimiwa Juma Nkamia ameambulia kuwa wa mwisho kati ya wagombea watatu waliokuwa wakigombea uraisi wa serekali ya wanafunzi chuo cha mipango....WAMEANGUKIA PUA PWAAAAAAAAAAAA!!!!!

  kampeni zilizodhaminiwa na CCM zilikuwa nzito kiasi kwamba TAKUKURU walijikuta wakiingilia kati na kubaini kuwa kuponi za chakula zilikuwa zinagawiwa bure na wapambe wa mgombea waliokuwa wakiranda randa huku na kule wakiwa wametinga PIERRE CARDINI mpya kabisa katika migahawa iliyo maeneo ya miyuji...watumishi wa idara hii walienda mbali na kumhoji mgombea huyo baada ya kubaini tuhuma hizo,,,,hadi tunaenda mitamboni hatujapata kujua kilichoendelea bali tu mgombea huyo KUBWAGWA VIBAYA NA KUWA WA MWISHO KATI YA WAGOMBEA WATATU....

  huu ulikuwa ni mtihani wa aina yake kwa wasomi hawa ambao ni taswira katika jamii....swali walilokabiliwa nalo ni JE MATUMIZI MAKUBWA YA PESA, UCHAKACHUAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YANA NAFASI KATIKA FIKRA ZA WASOMI NA HATIMAYE WATANZANIA?

  baada ya kuona matumizi makubwa ya pesa, na vitisho, na misafara, wanafunzi haya waliamua kwa makusudi kabisa kumsupport mgombea asiye na makuu, na ambaye hakuwa na tambo zozote za kisystem...ambaye pia mtazamo wake ni waKILIBERALI na kuexercise nguvu ya umma kuwajambisha bwana kwagilo na mama nkamia....

  mgombea wa magamba anataka kukata rufaa, hata hivyo tetesi zinasema kuwa faili lake liko takukuru.....nadhani badio ana kizunguzungu cah KUTUMIA PESA NYINGI NA KUANGUKIA PUA

  my take;

  1. CCM lazima itambue wazi kuwa kizazi cha sasa hakitishiwi nyau...mapiki piki wala toli toli...inapaswa sasa kufanyia kazi kwa uadilifu kero za wananchi ili kuiwezesha nchi yetu isonge mbele......

  2. Wasomi wameonyesha dira, umma unafuata nyuma yao with full support......hongera sana wasomi

  3. Vyama vya siasa kusupport CHAGUZIi za vyuoni ni uhuni na unapaswa ukemewe VIKALI

  4. ni wakati sheria za uchaguzi kuanza kufuatilia chaguzi za vyuoni ie gharama za uchaguzi

  5. narudia tena HONGERA SANA WASOMI WETU....sasa ninyi ni WASOMI KWELI KWELI!

  Mungu ibariki Afrika,

  Mungu ibariki Tanzania!​
   
 2. m

  mshanga New Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahahahahahhahah !!!!!!!!!, usivunje mbavu mie.
   
 3. y

  yuxygaxy Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi ni vizuri
   
 4. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nashukuru kwa taarifa hiyo nzuri
   
Loading...