Elections 2010 Hongera wana Kigoma kwa Kutodanganyika

ludoking

Senior Member
Oct 5, 2008
124
71
Kwanza naomba niwapongeze wana Kigoma kwa kuonyesha moyo wa dhati wa mageuzi ya kweli. Kigoma wamewanesha watanzania kuwa wamechoshwa na utawala dhalimu wa CCM. Sasa Kigoma imekuwa ngome ya upinzani kwani upinzani wamechukua takribani majimbo sita (6) ya ubunge kati ya nane. NCCR wamechukua 4 na CHADEMA 2. Hiki ni kiashiria cha ukombozi kwa wana Kigoma. Wamechoshwa na kudhihakiwa na CCM kwa kunyimwa maendeleo. Ilionekana Kigoma kusahauliwa katika nyanja mbalimbali. Hii inadhihirishwa na kauli ya Kikwete katika baadhi ya mikutano yake aliposema akichaguliwa "ATAIUNGANISHA KIGOMA NA TANZANIA" as if Kigoma siyo Tanzania. Nawapongeza wabunge wateule TENA WOTE VIJANA kazeni buti tuko nyuma yenu katika kuleta mageuzi ya kweli. Mungu ibariki Kigoma, Mungu ibariki Tanzania
 
Chadema kigoma wamepata majimbo mawili? Moja najua ni Zitto, Lingine?
 
Back
Top Bottom