Hongera wana JamiiForums: Mbunge Nyambali Nyangwine ameanza kuwalipa mishahara wafanyakazi wake

jiji101

Member
Jul 9, 2013
22
12
Baada kuweka post yenye kichwa cha habari ' https://www.jamiiforums.com/habari-...i-nyangwine-awanyanyasa-wafanyakazi-wake.html na kupitia michango yetu ya wana JF mbunge uyu jana ameanza kuwalipa mishahara wanfanyakazi wake.

Amewalipa mshahara wa mwezi mmoja kwahiyo bado mishahara ya mwezi miwili ( December na January) kumbuka tupo mwezi February kwahiyo kunauwezekano mkubwa wa iyo mishahara ikakutana na mwezi February, sasa sijajua kama atawalipa mwezi yote.

Ila mwazo mzuri kama aweza kusikia kilio cha wafanyakazi wake na kuanza kuwalipa mishahara na mpongeza kwa ilo. Naomuomba Mh. Mbunge amalizie kuwalipa mishahara iliyo baki maana ni haki yao kulipwa.

Vile vile awa wafanyakazi wengu wao nimeambiwa wanamadeni mitaani kwao kwahiyo wamekuwa wakikosa raha wanapo sumbuliwa na wadeni wao maana wanashindwa kujua lini walipwa mishahara yao ili wakalipe madeni wanayo daiwa.

Nakupongeza Mh. Mbunge kwa kusikia kilio cha wafanyakazi wako ila nakuomba sana umalizie umalizie mishahara ilio baki.

Kwa pamoja wanaJamiiForums tunaweza.
 
Wewe ulidhani tupo humu tunapoteza tu muda? tunajenga nchi kidijitali na mabadiliko ni kama hayo unayoyaona.
 
Sio kulipa mishahara tuu apeleke na hela zao za mafao katika mifuko husika sio achezeshe kitambi hapo bungeni tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom