MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,756
- 48,401
Niko huku Sudan Kusini nasaka mpunga kwenye mishe fulani hivi na nimefaulu kukatiza maeneo mengi na kushududia namna Wakenya wamehusika pakubwa kwenye kubadilisha maisha ya hawa watu waliokua wamezoea vita maporini. Kiswahili kinazidi kutamalaki na kuzagaa, leo hii kuna ushindani mkali baina ya Juba Arabic, Kingereza na Kiswahili na kwa namna fulani Kiswahili kinapenya kwa kasi.
Wasudan wengi wamesomea Kenya na kurudi huku na kushika nyadhifa muhimu muhimu, pia shule nyingi za maana zina walimu Wakenya au hao Wasudan waliorudi baada ya kusomea au kuishi Kenya. Kinatumika mtaani, maofisini na nilishangaa kwenye vyombo vya habari wanachomekea sana maneno ya Kiswahili kwenye mada zao hata wakati wanajadili kwa matumizi ya lugha zao za asili kama vile Dinka.
Ni muda tu, rais hatakua na budi ila kukifanya mojawapo wa lugha za taifa, maana mawaziri wake na wabunge wote, watoto wao wanasomea Kenya na hurudi nyumbani wameiva wakiwa tayari kwenye ujenzi wa taifa.
Uganda tu ndio niliwashangaa nilipokua kwao, wameshupaza shingo, wamekomalia Kingereza fulu, unakuta mtu aidha umuongeleshe kwa Kiganda au Kingereza, hajui neno hata moja la Kiswahili.