Hongera waalimu kwa kugoma kulipa fidia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera waalimu kwa kugoma kulipa fidia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Aug 16, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Serikali inaendelea kufanya tathmini ya hasara iliyojitokeza wakati wa mgomo wa waalimu na kwamba itahakikisha hasara yote inalipwa na CWT kilichoratibu mgomo huo!

  Hata hivyo Katibu Mkuu wa CWT amesema chama hicho hakitalipa hasara hizo kwa sababu serikali ilijua kuwapo kwa mgomo wa waalimu na hivyo ilitakiwa ichukuwe tahadhari na kuhakikisha kuwa mali zake ni salama. Aidha hakuna hata mwalimu mmoja aliyekamatwa kuhusika na uharibifi huo na kama yupo serikali inatakiwa kumfikisha mahakamani!

  HOJA YANGU: Serikali acha kugandamiza vyama vya wafanyakazi na kuwanyanyasa waajiriwa wako!
   
 2. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Wanagandamizwa kwa kuwa hajajua kuitumi nguvu waliyonayo.
   
 3. ufisadi no

  ufisadi no Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Halipi mtu hapa.mwalimu ana akili zake,hawezi kufanya uhalibifu kama inavyo daiwa.ndiyo maana hadi sasa hakuna teacher anayeshikiliwa.
   
 4. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida serikali itaenda mahakamani!
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wasipinge kwa maneno wakapinge mahakamani tuone nani ndio nani.
   
 6. Gooogle

  Gooogle Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahakama ya LUMUMBA!?
   
 7. F

  FATHER OF HISTORY JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 545
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 60
  Wa ache sanaa bwana,fidia ya nini?
   
 8. F

  FATHER OF HISTORY JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 545
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 60
  Mafisadi wa rada,ndege ya rais,Twiga waliotajwa kwenye riport ya CAG,Richmond,TANESCO,waziri aliyesababisha watoto 5000 na zaidi waende sekondari bila kujua kusoma na kuandika kwani hizo siyo hujuma kwa serikali? fidia zitalipwa lini?
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  Hivi hili swala si bado lipo mahakamani?...nani karuhusu mjadala tena?
   
 10. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kikwete alikwisha toa hukumu! Nani zaidi Kikwete au mahakama?
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Chama cha walimu ni mayeboyebo tu!!
   
 12. T

  True Leader New Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hivi tunafahamu ya kuwa sisi wananchi ndio Serikali yenyewe?

  Tatizo letu hatujifahamu ndio tunaburuzwa,walimu wakigoma inatakiwa nchi nzima tunagoma na kuhakikisha hakuna litakoloendelea mpaka jamii ya kimataifa iingilie kati.

  Tuache kuwa watu wa maneno tu, vitendo ziro, hivi bila walimu nani angekuwepo?

  Halafu first lady nae anajua kila kitu mpaka nini cha kufanya lakini sijui anampango gani na wafanyakazi wenzake wa zamani.

  Inatakiwa walimu ndio wadeke kipindi chote ambacho yeye ni first lady,there is no too late once you decide to change.
   
 13. Ukwelinauhakika

  Ukwelinauhakika Senior Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  kilichobakia 10+10= 100. sababu hamna klchoeleweka mpaka sasa, watakoma wanafunz na serikali.
   
 14. Mapambano Yetu

  Mapambano Yetu JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 180
  walim nao wana haki kama walivyo maofisa wa jeshi la wananchi, kama afisa wa jeshi ambaye pia ni mwalim anapata stahili zake zote bila wasi, kwa nini huyu mwingine afanyiwe mizengwe? walimu ndio wenye uwezo wa kuliangamiza taifa. fahamu kwamba unyanyasaji kwa walim utasababisha tuwe na taifa lililojaa kizazi cha wajinga. huwezi kumlazimisha utakavyo wewe, leo atalazimishwa kuingia darasani lakini atawaimbisha wanafunzi na kuondoka zake. fahamu kwamba "utamlazimisha ng'ombe kwenda mtoni lakini hutaweza kumlazimisha kunywa maji"
   
 15. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Serikali ya kishetani huwafanyia raia wake mambo ya kishetani kama kuwateka, kuwatesa na kuwaua
   
 16. Kwisimla

  Kwisimla Senior Member

  #16
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wanaonea na kudharau wadogo, mbona mafisadi hawa ambiwi walipe fedha zote walizo iba?
   
 17. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  huwa waziri naona ameshaanza kuchanganyikiwa maana nilisikiliza alichokuwa anaongea ilionyesha anaropola kabla ya kutathimini afanye nini na kwa nini afanye vile
   
 18. k

  kaeso JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uharibifu gani uliotokea wakati wa mgomo?
   
 19. mito

  mito JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,619
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  Huyo katibu mkuu nadhani ni mbumbumbu w sheria. sidhani kama anajua nini maana ya amri ya mahakama. Kulipa watalipa tu unless a appeal is in favour of chama cha walimu
   
 20. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna kampeni ya kuikomoa CWT, ukifuatilia hata mijadala ya baadhi ya wabunge utagundua ilo
   
Loading...