Hongera TRA kwa makusanyo ya trilioni 5.9 ila bado Serikali haijawawezesha kukusanya kwa upana wake

Tawfiq 77

Member
Jul 5, 2021
5
10
Nitoe pongezi za dhati kabisa kwa mamlaka ya mapato kwa kufanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha ktk muda huo maoni yangu. Pamoja na mafanikio hayo lkn bado tra inauwezo wa kukusanya zaidi km serikali itaamua kuwekeza ktk rasilimali watu na vitendea kazi.

Kama tunavyojua baada ya ubinafisishaji wa mashirika ya umma serikali ilijondoa rasmi ktk kufanya biashara hivyo basi mapato mengi ya serikali yanatokana na kodi na TRA ndio muhimili mkuu wa ukusanyaji kodi hizo.

Naomba nigusie maeneo manne ninayaona km yakifanyiwa kazi yanaweza kuchangia kuongeza mapato mosi Nchi yetu mfumo wa walipa kodi unawaumiza wachache kwa manufaa ya wengi.

Mosi Watanzania tunakadiliwa tunafika zaidi ya miliomi 55 kati ya hao walipa kodi waliandikishwa na mamlaka ya mapato hawafiki hata miliomi kumi maana yake watanzania chini ya 20% ndio wanalipa kodi na zaidi ya 80% hawapi kodi na tunategemea maendeleo hakuna muijiza hiyo duniani.

Jambo la msingi ambalo km serikali walitakiwa kuhakikisha kila mtanzania mwenye kazi ya kumuingizia kipato ni lazima anakuwa na number ya mlipa kodi awe mkulima, mfanyabiashara, mfanyakazi.

Na hapa naomba nifafanue kidogo kwenye haya makundi nikianzia na wakulima hapa ndio kwenye kipato cha watanzania wengi hivyo basi serikali inatakiwa kuliangalia kundi hili kwa namna ya pekee ikiwepo kuwatafutia masoko ya mazao kuongeza dhamani ya mazao nk hali hii itapelekea kukusanya mapato mengi kutokana na ukubwa wake.

Wafanyabiashara serikali inatakiwa kuwawezesha kupata mitaji ktk tasisi za kifedha na Kupunguza wingi wa kodi ili kila mfabiashara aone fahari kulipa kodi.

Wafanyakazi hapa kuna tatizo kiasi kikubwa naona linachangiwa na serikali yenyewe sababu asilimia kubwa ya wafanyakazi sasa sio waajiliwa ni vibarua hasa viwandani unakuta mtu ni operate wa mashine lkn ni kibalua hana ajira maana yake serikali inakosa kodi ya paye na mfanyakazi anakosa haki zake sielewi tatizo lipo wapi.

Na mwisho nizungumzie vitendea kazi nafikili serikali ilitakiwa iwezeshe sana hii mamlaka ingewezekana office za TRA zingekuwa na mfumo km wa tamisemi yaani office za tra zianzie taifa mpaka kata maana kwenye office ya serikali ya mtaa pia kuwe na office ya TRA yenye miundo mbinu yote hadi counter ya malipo ya bank kodi zianzie kukusanywa ngazi ya chini kabisa office za tra zitapakae nchi nzima na kila mtu alipe kodi km tunataka maendeleo ya kweli
 
Kama anakusanya Sana awalipe basi wafanyakazi wa serikali arrears za mishahara Yao za tangu 2018! Hayo malimbikizo ya mishahara anataka wadai waipeleke serikali yake mahakamani wakadai na riba? Hebu afanye chap kabla uchaguzi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom