Hongera TRA kwa kuvunja Rekodi ya Mapato

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Kwa mara ya kwanza tangu Tanganyika ipate uhuru, mapato ya serikali kwa kila mwezi yamfika Trilioni, hata mwezi wa nne ambao kwa kalenda ya kodi Tanzania unatajwa kuwa ni mwezi mgumu ambapo makampuni husamehewa kodi lakini mwaka huu imekuwa tofauti.

Pongezi za pekee ziendi kwa vyama vya upinzani chini ya GWIJI la siasa za nera Laigwanani Edward Lowassa ambapoo bila yavyo serikali ingezidi kulimaliza taifa hili.

Pongezi kubwa pia siende kwa Mkurugenzi wa TRA na boss wake.

Kizuri kisifiwe na kibaya kikosolewe,

Tunataka hali ya maisha ya watu itengamae sio takwimu za makaratasi huku mtz akila nyasi.

IMG-20160506-WA0210.jpg

IMG-20160506-WA0209.jpg
 
Watu tunadai arrears za mishahara karibu mwaka sasa hawatulipi alafu kila mwezi wanatutangazia mapato kuongezeka!Tumeshawachoka!
 
Haya ndo matunda ya kupiga kelele, hatimaye tumeshinda wote, tunataka vyanzo vipya vya mapato ikiwemo mgawanyo sawia wa kodi Kwa kila Mwananchi kulingana na kazi na vipato vyao...........

Tumpongeze pia rais, at least kwa kuipenda Tanzania....
 
Hujui tu wewe.Mtu unapanda cheo tangu mwezi June mwaka jana ila mpaka leo malimbikizo yako hupati.Wanatakiwa wawe na vipaumbele vinavyogusa maisha ya watu wa kawaida. Wakikusanya fedha hela nyingi ni kulipa wakandarasi wakubwa huku watumishi mkilipwa kwa mafungu mafungu mpaka watu mnakata tamaa. Jiulize mbona wao wakijipandishia mishahara huwa hakuna huu urasimu?Inaudhi sana!

Tunaodai malimbikizo nchi tuko wengi na sio walimu tu kama ilivyozoeleka ila sisi wengine huwa tunaamua kukaa kimya tu.
 
MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) kwa mwezi uliopita imekusanya Sh.Trioni 1.035 ambayo ni sawa na asilimia 99.5 ya lengo kukusanya sh.trioni 1.040 .
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa katika makusanyo ya miezi 10 wameweza kukusanya sh. Trioni 10.92 ambayo sawa na asilimia 99 ya lengo ya sh.trioni 11.02 katika lengo la kipindi hicho.
Amesema kuwa TRA imedhamiria kukusanya zaidi ya sh. Trioni 1.4 na kuvuka lengo la mwaka wa fedha wa 2015/2016 katika miezi miwili ya kumaliza mwaka wa fedha ambalo ni sh. Trioni 12.3.

Kidata amesema kuwa TRA itaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015 / 2016 licha kuwepo kwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo.
Amesema kuwa wananchi wamejua umuhimu wa kodi na kuanza kutoa ushirikiano katika kudhibiti mianya ya magaendo, pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ikiwa katika usimamizi wa mifumo ya mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu wowote.
 
Aongeze Tax base na sio kuwakamua wafanyakazi tu.Sekta ya Utalii na Madini vimechangia kiasi gani katika hiyo Kodi? Au bado Sigara na Pombe zimeendelea kuwa juu na vyanzo vipya vya mapato kutoka kwa wahalifu wa usalama barabarani? Unaongeza kukusanya mapato kwa kukamua wafanyakazi huku ukipoteza Trilioni moja na Ushehe kwa sababu ya kukumbatia ubakaji wa Demokrasia kule visiwani.Tuone expenditure ya serikali itakuwaje sasa
 
Kwa mara ya kwanza tangu Tanganyika ipate uhuru, mapato ya serikali kwa kila mwezi yamfika Trilioni, hata mwezi wa nne ambao kwa kalenda ya kodi Tanzania unatajwa kuwa ni mwezi mgumu ambapo makampuni husamehewa kodi lakini mwaka huu imekuwa tofauti.

Pongezi za pekee ziendi kwa vyama vya upinzani chini ya GWIJI la siasa za nera Laigwanani Edward Lowassa ambapoo bila yavyo serikali ingezidi kulimaliza taifa hili.

Pongezi kubwa pia siende kwa Mkurugenzi wa TRA na boss wake.

Kizuri kisifiwe na kibaya kikosolewe,

Tunataka hali ya maisha ya watu itengamae sio takwimu za makaratasi huku mtz akila nyasi.

View attachment 345230
View attachment 345234
kwahiyo kina kitilya wamekula vichwa saaana hapa eeeh
 
Safi sana , bila shaka sisi tunaodai hela zetu miaka na miaka baada ya kulisha mashule na maeneo mengine sasa tutalipwa , asante Mungu .
 
Sasa nitachangia nini bila mada kushibishwa kwa data sahihi !!!!!.......

Uthibitisho ni muhimu zaidi kama utaleta Mada nyingine maana kupost kitu haikugharimu kitu...
Zingatia credibility ya habari yako
 
Juzi tu kuna watu walifungua thread wakilaumu TRA kwa nini haitangazi mapato yaliyopatikana April
 
Kwa mara ya kwanza tangu Tanganyika ipate uhuru, mapato ya serikali kwa kila mwezi yamfika Trilioni, hata mwezi wa nne ambao kwa kalenda ya kodi Tanzania unatajwa kuwa ni mwezi mgumu ambapo makampuni husamehewa kodi lakini mwaka huu imekuwa tofauti.

Pongezi za pekee ziendi kwa vyama vya upinzani chini ya GWIJI la siasa za nera Laigwanani Edward Lowassa ambapoo bila yavyo serikali ingezidi kulimaliza taifa hili.

Pongezi kubwa pia siende kwa Mkurugenzi wa TRA na boss wake.

Kizuri kisifiwe na kibaya kikosolewe,

Tunataka hali ya maisha ya watu itengamae sio takwimu za makaratasi huku mtz akila nyasi.

View attachment 345230
View attachment 345234
Baada ya kumtukana sana Lowasa kwenye mitandao, sasa mmeamuriwa kumtaja kwa kila mnachotupia humu jamvini hata kama hausiki katika kufanikiwa kwake.
Hivi huyu Lowasa anamchango upi hasa katika haya mafanikio ya TRA?
 
Ni jambo zuri sana kwa serikali yetu kufikia mafanikio haya. Hongera Serikali yetu, Hongera TRA. Kazi nzuri.
 
Back
Top Bottom