Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,260
Taarifa zinasema wafanyakazi tisa (9) wa TBC wamesimamishwa kazi baada ya kushiriki katika kuandaa na kutangaza taarifa ya habari ya UONGO na ya KUTUNGA kwamba eti MAGUFULI amepongezwa na TRUMP, jambo ambalo halipo na halikuwahi kutokea.
Dr. Ayoub Rioba ambae ni Mkurugenzi mtendaji wa TBC amethibitisha.
Wakati TBC wanachukua hatua hiyo kumekuwa na madai kwa muda mrefu sasa kuwa RC mmoja wapo amefoji vyeti/kutumia cheti kisicho chake hivyo kujipatia nafasi ya kusoma na baadaye kazi.
Kelele hizi zinapigwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandano ya kijamii. Mpaka sasa si mtuhumiwa wala serikali aliyeonesha kuchukua hatua yoyote ha kujisafisha au kueleza ukweli.
Hapo ndipo panapo leta maswali kwanini serikali imeamua kunyamaza kimya kuhusu mtuhumiwa wa vyeti wakati yenyewe ndiyo inafanya uhakiki wa vyeti na kutaka wananchi kutoa taarifa kuhusu mtu yeyote aliyetumia cheti kisicho chake au kughushi vyeti.
Ni jambo la kushangaza mpaka sasa rais yupo kimya wakati huko nyuma ameonekana kutumbua watu hata kwenye mikutano ya hadhara hata bila kupata ushahidi wa uhakika kabla ya kumtumbua mtu. Where are you Mr President?