Hongera star tv kwa kipindi hiki cha asubuhi show,lakini wageni hawa............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera star tv kwa kipindi hiki cha asubuhi show,lakini wageni hawa.............

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ligendayika, Oct 8, 2012.

 1. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Tunapongeza kipindi hiki cha asubuhi kwani kimesheeni habari nzuri na motomoto lakini tatizo ni baadhi ya wageni mnaowaita hapo kweli wanatuharibia hata hamu ya kuendelea kutazama wanakuja na misimamo yao na kutoa amri tu. ilihali kwa mtazamo wangu mnawaita watoe maoni na namna ya kutatua au kusuruhisha baadhi ya mambo na pengine kutoa maelezo fulani . Lakini kuna baadhi ya watu wao ni kutoa amri kuwataka watu au viongozi kuchukua hatua sasa sijui wao nao ni viongozi au Star tv mnawaita ili wawasemee viongozi wetu. Nawasilisha.
   
 2. C

  Chipolopolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu.Angalia isijekuwa labda na wewe umeshindwa kuwaelewa.Bila shaka na wao ni maoni yao tu japo wewe umeyatafsiri kama amri.Jambo la msingi ni kuangalia katika hilo walisemalo lina mashiko?Kama hoja ina mantiki basi acha na iwe amri tu...!
   
 3. damper

  damper JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Hasa hao wageni wanaokuwa studio ya Mwanza, mimi binafsi hata kama mada ni nzuri napata shida sana kuwaelewa baadhi ya hao wageni!! Kwangu mi Channel ten kwa Kibwana Dachi nawakubali sana.
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kipindi cha toungee asubuhi kiko fresh ila kuna siku waliwaalika wazee wawili makada wa magamba waliboa watu wengi sana.
   
Loading...