Hongera Simba kwa kumpa Mgunda timu kama Kocha Mkuu, apewe mshahara mnono na siyo kutumiwa kama njia ya kubana matumizi

Naskia washampa usafiri TATA NEXON
IMG_6373.jpg
 
Sio utaratibu ila ni hulka Hasa Kwa jamii zilizostrabika ambako level za critical thinking na ustaarabu Ziko juu! Hebu fikiria mshahara wa mgunda mashabiki wanaambiwa ni ml 20... Nini kitatokea??
Wachambuz Wetu wataacha kuongelea Soka na kujadili mshahara?
Familia Huko Kwa mgunda ni vita mura wanaona ndgu Yao anapesa
Mashabiki wa yanga na Simba nao vurugu kujadili.

Tisa kumi yote hya yanakuja kuiathir timu.mambo ya kutangaza mshahara tuachie wwnzetu kwanza, Akili zikue kwanza.
Hoja unayozungumza ina mashiko, tatizo ni pale usiri unapotumika kumnyonga mtu!! Kwanza huo mshahara wa ml 20 uliotolea mfano bado ni mdogo sana kwa hadhi ya timu kama simba!
 
Atafukuzwa tu hapo wacha tuwapige tarehe 23,halafu tuwapige Fa,halafu tuwapige round ya pili ya ligi...wameondoshwa wazungu akina uchebe itakua huyu?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Hajawahi kutokea kocha yeyote akawa wa kudumu!! Alifukuzwa mzee Wenger pale Arsenal itakuwa hapa bongo!! Tunachosema ni kuwa wakati bado ni kocha apewe mshiko wa kueleweka. Kwa mawazo yangu kitu kama milioni 50 kwa mwezi!!
 
Shida yako nn?UTOPOLO bana Simba walipopanda Pipa kwenda Angola siku Moja kabla ya mechi mlisema wamefilisika Leo hii UTOPOLO mmeiga hakuna anayesema mmeishiwa Kwa akili hizi Yanga Kuingia Makundi mwaka ni ndoto labda mwakani
Mbona umemshambulia hivyo? Hv kwani hamkukodi kama tulivyoaminishwa?
 
Hapo mtasemaje tena? Soka linaloendeshwa Tanzania linapaswa kufuata kanunu na utaratibu na utamaduni huo huo wa soka ulimwenguni kama tunataka kutoboza kwenye soka la kimataifa!!
Sisi tuna tamaduni zetu watz, wachezaji wa ulaya tunajua mishahara yao lakini hatukuwahi kujua mshahara wa Samata unazani kwanini?
 
Hajawahi kutokea kocha yeyote akawa wa kudumu!! Alifukuzwa mzee Wenger pale Arsenal itakuwa hapa bongo!! Tunachosema ni kuwa wakati bado ni kocha apewe mshiko wa kueleweka. Kwa mawazo yangu kitu kama milioni 50 kwa mwezi!!
Usiwapangie simba, mgunda kama ataona pesa anayopewa hailingani na anachodeliva atabwaga mzigo
 
Hajawahi kutokea kocha yeyote akawa wa kudumu!! Alifukuzwa mzee Wenger pale Arsenal itakuwa hapa bongo!! Tunachosema ni kuwa wakati bado ni kocha apewe mshiko wa kueleweka. Kwa mawazo yangu kitu kama milioni 50 kwa mwezi!!
Nimependa sana hapo uliposema KWA MAWAZO YANGU.
Kwa sababu, mawazo yako tumeshayasikia, nadhani sasa tuyape nafasi MAWAZO YA JUMA MGUNDA na mwajiri wake SIMBA SC yaamue suala la mshahara.
 
Ukiwa kocha mkuu unaandamwa na maswahibu yote , mgunda mtamkataa soon
 
Tutumie uzi huu kuipongeza Simba kwa kumpatia Mgunda nafasi ya kuwa kocha mkuu wa Simba. Naamini kabisa kuwa Mgunda almaarufu kama Gurdiola Mnene ataifanyia Simba maajabu ambayo hatujawahi kuyapata kwa makocha Wazungu.

Angalizo langu ni kuwa isitokee hata kidogo kuwa simba wamempa nafasi hiyo kama namna ya kubana matumizi kwa kumpa mshahara mdogo!

Hiyo itakuwa ni laana. Kama ambavyo mishahara ya makocha wa kigeni huwa inawekwa wazi (na huu ndiyo utamaduni wa kwenye soka), tunaitaka Simba iweke hadharani mshahara wa mgunda kama Kocha Mkuu wa Simba! Tusisikie eti mnampa vi milioni 10 - 20 huo utakuwa ni uchawi na kutaka kunyanyasa makocha wazawa! Napendekeza kuwa Mgunda apewe mshahara si chini ya kocha yeyote wa kigeni aliyeifundisha Simba hivi karibuni!

Nawasilisha!
Yaani milioni 20 ni kidogo?
Kuna watu mna vichaa vya mbwa
 
Kwa nini usiwekwe hadharani? Mbona mishahara ya makocha wazungu huwekwa hadharani? Ikiwa ni siri lazima atapunjwa!! Mbaya zaidi anaweza kupewa mshahara mdogo kuliko baadhi ya wachezaji wa kigeni na hawatamheshimu!!
Athari zake zitakuwa kwenye familia na jamii inayonufaika na jasho la Mgunda.
Bado wa Tanzania tunaishi maisha ya kumtemea mjomba, shangazi aliyepo Daithalamu.
 
Mshahara ni makubaliano ya pande mbili, hakuna habari ya kusema mimi nataka kulipwa kama yule.unalipwa kutokana na ulivyojiuza na madini uliyo nayo
Tatizo ni kuwa unachokiita wewe kuwa ni mshahara mzuri unajilinganisha na kipato chako cha m1 au m2. Kwa hiyo ukiona kapewa m5 wewe utasema ni mshahara mzuri!! Hiyo HAPANA. Apewe mshahara kulingana na jinsi walivyokuwa wanawalipa makocha wa kigeni!! Huwezi kutegemea kocha wa kigeni apewe m5!! Lakini wabongo hawana aibu!! wanaweza kumwiliza kwani coastal union walikuwa wanakupa shilingi ngapi? Kwa hiyo sisi tunakupa mara mbili yao!! Hapo keshapigwa tayari!!
 
Yasije yakawa kama ya azam na yule kocha msomali baada ya kusain mkataba wa miaka mitatu
 
Back
Top Bottom