Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,285
Hatimaye serikali imesikia kilio cha wadau wa elimu waliokuwa wakishauri kuitaka serikali iruhusu watoto wanaopata ujauzito wangali mashuleni waendelee na masomo, binafsi naipongeza serikali kwa kuona kuwa ni vyema na haki kuwaandalia utaratibu watoto hao kuendelea na masomo, Na sababu zangu ni hizi zifuatazo:
1. Kwanza sheria zetu nchini zinasema kuwa kufanya mapenzi na mtoto chini ya miaka 18 unakuwa umebaka hata kama karidhia, Sasa inakuwaje aliyebakwa umhukumu kwa kumfukuza shule, Yaani ni sheria gani hiyo mbaya kabisa ya kuadhibu victim?, Mwanafunzi alipaswa afanyiwe counselling, na kumpa msaada wa kisaikoojia baada ya kubeba mimba kwa sababu kakosewa yeye na siyo kumuadhibu zaidi.
2. Pili Akili hazikai tumboni, bali ziko kichwani, hakuna ushahidi kuwa mwanafunzi akiwa na mimba hawezi kusoma, akaelewa, kisha elimu hiyo ikaja kuwa na manufaa kwake, kwa familia yake na Taifa kiujumla.
3. Tatu kumfukuza mwanafunzi shule ni kumuadhibu kwa kumnyima elimu yaani ni kumhukumia Ujinga, Sasa kufanya hivyo ni kukwamisha juhudi za Taifa za kupambana na umasikini, Ujinga na maradhi, maana elimu ni silaha ya kupambana na hivyo vitu vitatu. Sasa Taifa lingepata faida gani wakati linawanyima elimu baadhi ya watu wake makusudi eti hiyo iwe ni adhabu kwao?
4. Nne mimba siyo kosa la kisheria nchini, bali kile kitendo kinacholeta mimba ndiyo kosa la kikanuni katika mashule yetu, Sasa kumfukuza mwanafunzi shule si tu kuwa unakuwa unaharibu future yake peke yake bali unaharibu future hata ya mtoto aliye tumboni mwake pia, maana future ya mtoto iko linked na mama yake. Sasa Taifa gani hilo katili linaadhibu hadi mimba!
5. Sasa imagine tayari umemfunga baba mtu miaka 30 kwa kosa la "kubaka" , kisha ukamfukuza mama yake shule, huyo mtoto atakayezaliwa atakuwa na hali gani?, baba hayupo yuko jela, mama ndo hivyo mmeamua kumuadhibu kwa kumnyima elimu, huyu mtoto akiwa mkubwa atalipenda kwel hili Taifa?, Yaani Taifa limfukuze mama yake shule kisha mtoto huyo ukubwani eti aje kuwa mzalendo wa kulipenda Taifa hilohilo lililomuona yeye ni mzigo na kosa kubwa tangu akiwa mimba?
6. Kuna wale wanaosema eti kumuacha mwanafunzi darasani ni sawa na kupigia chapuo tabia mbaya kwa watoto wengine, hiyo hoja ni muflisi kwa sababu hawa watoto huko nyumbani watokapo mama zao, dada zao, shangazi zao, majirani zao bado wanabeba mimba, kwa nini tusiseme kuwa watajifunzia huko tudhani eti watajifunzia shuleni kwa wenzao wenye mimba?.
7. Kuna wale wanaoleta hoja za dini katika suala hili, kuwa uasherati na uzinifu ni dhambi, ni kweli vitendo hivyo ni dhambi, lakini siyo kazi ya serikali hii ya kisecular kutangaza dini au kuadhibu madhambi ya kidini, Lakini pia wale wanaotaka watoto wafukuzwe shule kwa sababu wametenda "dhambi", Je adhabu ya mtenda dhambi wa makosa hayo huwa ni kumfukuza shule?, Je na wale wanaozini mtaani nao mnataka serikali iwafanyeje?
Kwa hiyo basi kwa hoja za kimantiki, kiuchumi, kihaki na umuhimu wa elimu kwa kila mtu, naipongeza sana serikali kwa uamuzi huu wa busara, huu ni uamuzi tuliousubiri kwa muda mrefu.
KUMNYIMA ELIMU MTOTO WA KIKE ni kukwamisha juhudi za Taifa kwenye kupambana na Umasikini, Ujinga na Maradhi