Hongera Sanctus Mtsimbe: apanda ngazi katika kazi mpya! Bosi nchi 11

Hongera sana kaka umetutoa kimasomaso!!!

Tatizo la wasomi wengi wa TZ ni waoga mno wa changamoto. Ndo maana wamekalia kulialia tu na kuwaona wengine kama wa-Kenya kuwa wako juu yetu. Afadhali Bw. Mtsimbe umewaonesha njia wasomi wengine!! Naamini humo kulikuwa na wa-Kenya, waganda, n.k lakini umewabwaga. Wasomi wengine igeni huo mfano msiogope kuomba kazi kubwa kubwa kwa kujishusha utafikri hamjaenda shule!!

Always it pays to have a trained person!!

Hongera sana bro. kachape kazi na uache porojo za wa-TZ.

Asante sana Job K.

Nasaha zako nitazizingatia Mkuu.
 
hahah hahha...sasa mshkaji vip kale kamimba ulikonipa?ulikokatelekeza...UTANIHUDUMIA?(joke)



misss u ma dia..just congratsssssssssss ma supaman.....hongeraaaaaaaaaaaaa sana..

lin utakuja ..pande ile ya brazil?

hongera mshikaj

MUNGU AKUJALIE BUSARA NA HEKIMA KTK KAZ ZAKO

Duh! JF is Amazing . . . . Nitunzie, nitahudumia tu . . . LOL (Joke)

Brazil nauli shida tena. Msalimie Dos Santos . . .

Asante sana kwa pongezi.
 
Inafurahisha sana kusoma habari kama hii. Hongera sana Mkuu maana nakumbuka sana juhudi zako na wadau wengine kwenye kuchangia Wahanga wa mafuriko. Kila la kheri huko unakoenda na ukawe balozi mzuri kwa familia yako, ndugu zako, Marafiki, Watanzania na Waafrica kwa ujumla na mwisho, kama binadamu.

Kuna haja ile kampeni ya kuchangia isiishie hapo. Itakuwa vema siku moja kiwepo kitu kama hicho walau mara moja kwa mwaka kwani wenye kuhitaji hapa Tanzania wapo wengi na kama alivyosema Mzee Mwanakijiji, inaonekana kuwa sisi Watanzania pia tunaweza sasa swali linakuja "kwanini kwenye misaada tusiweze?" Kuna Watanzania wanaishi vizuri sana kuzidi hao wa nchi tajiri zinazotoa msaada ila wai wanaamini kuwa kutoa ni moyo.

Kila la kheri katika kazi yako mpya na HONGERA SANA.

Kaka Sikonge asante na nashukuru sana kwa kumbukumbu zako hai.

Bila ya shaka nakumbuka nawe ulikuwa kati ya wachangiaji wakuu na nina uhakika Mungu anaendelea kukubariki sawa sawa na ahadi zake.

Asante sana kwa pongezi zako na yote uliyoongea.

Ubarikiwe sana Mkuu.
 
Congrats brother Sanctus. I remember you those days a serious A-level guy who commanded much respect from us O-levels at a certain school in the coast region! I will still look up on you brother as you conquer the global with your hardwork and dedication. Congratulations.

Asante sana kwa kunikumbusha habari za Kibaha High School . . . . . Ila umesahau kuwa tulifukuzwa shule kwa ule mgomo? Good luck kuvunjika kwa korea sio mwisho wa uhunzi. Tuwasiliane kwa PM . . . .

Asante sana kwa pongezi.
 
Big up,ex- Kibo Sec school,Moshi tena pale stend ya basi hii inaonesha shule siyo lazima ya hadhi kubwa au pesa nyingi juhudi yako tu,kwani hata form vi nadhani ilikataa.

Asante sana HS na pia kunikumbusha habari za Kibo Sec.

Ila weka kumbukumbu vema, form IV ilikubali vema kwa daraja la juu kabisa. Refer vema kumbukumbu. Pia tuwasiliane kwa PM.

Asante sana kwa pongezi zako.
 
Congratulations On Your New Job
I want to say my heartfelt "Congratulations"
How glad I am for you, God has answered every prayer for all you seek to do.
~*Congratulations*~
May God bless and keep you in all ways
always..................................
 
Heshima mbele sana mkuu Mtsimble,

Karibu katika mtandao mpana na wa kimataifa, Hongera sana kwa kupanda ngazi mkuu, hii inaonesha kweli kujifunza, kushirikiana, kujiamini, na kuwa na juhudi katika unachofanya basi nafasi ya kupanda ngazi ni kitu kinachowezekana sana.

Kupitia mtandao wa TPN jaribu kuwakumbusha vijana wa Tanzania wawe na ujasili wa kufanya uliyoyafanya na waache uvivu uliozungukwa na fikra za siasa zenye kaulimbiu ya "maandamano ndiyo mkombozi", waambie hata wao pia kama sisi kaka zao wanaweza kuwa na kazi kubwa za kimataifa, maisha mazuri kumiliki nyumba maeneo kama Georgetown na kufanya bbq party kila weekend huku wakiisaidia serikali yao kwa mawazo yanayojenga ili kujenga mstakabali mzuri wa taifa letu changa, maslahi ya Taifa Mbele.

Respect

Mkuu GJ;

Asante sana kwa nasaha zako. Nitazifanyia kazi.

Asante sana kwa pongezi.
 
Mzee Mwanakijiji, kwanza naungana nanyi kumpongeza Mzalendo Sanctus Mtsimbe.

Pili sio kweli Watanzania waliosoma vizuri tuu, wanaonekana kuwa hawawezi hizi kazi za kimataifa, ukweli ni kuwa Watanzania hawaziombi!.

Sanctus ni mpiganaji ndio maana ameweza. Wengi wa Watanzania, they don't dare apply!.

Naomba nitolee mfano wa fani ya tasnia ya habari na utangazaji. Tanzania ndio nchi ya kwanza ulimwenguni kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha yake ya taifa. Wakati wa cold war, mataifa mengi yaliwachukua Watanzania kuwa watangazaji wake wa idhaa za Kiswahili, ukianzia BBC, VOA, Deutche Welle, NHK, Radio Mosco, All India Radio, RSA etc. Baada ya kuisha vita baridi, baadhi walizifunga lakini waliobaki wote haikuwa kuchukua Watanzania, bali sasa watu waliapply, angalia kilichotokea, Wakenya na Waganda walitake upper hand kwa kuwa na idadi kubwa ya watangazaji kuliko sisi Watanzania. BBC walipoamua kuanzisha regional centre, Nairobi ndio the choice not Dar es Salaam, kisa Watanzania hatuko aggresive sana kuomba kazi za kimataifa.

Niliumia sana nilipofika UN na kukuta ile Quota ya ajira ya East and The Horn of Africa pale UN imejazwa na Wakenya, Waganda, Wasomali na Wa Ethiopia, Watanzania were almost nill, nilipouliza nikajibiwa, hawaombi!. Nikamuuliza Mkenya mmoja, iweje wao wanapata, ndipo nikaujua ukweli. Kwanza MFA zao huzitangaza hizo posts kwa publics za nyumbani kwao, MFA yetu haina mpango huo. Pili, Wakenya na Waganda wakisikia openings tuu, huwatumia wenzao huku wameisha find out what does it take to get such jobs, sio sisi, ukishafanikiwa, hujiuona umeukata na ikitokea ukasikia Mtanzania mwingine yuko on your way to join you ndio kwanza unamkimbia au kumdidimiza kabisa!.

UDSM ndio ilianza kutoa wahitimu wa fani ya Kiswahili, leo vyuo vikuu vingi vinafundisha Kiswahili, ila huwezi amini, idadi kubwa ya ma lectures ni Wakenya!.

Wako Watanzania wengi kwenye top jobs mahala kwingi Ulimwenguni, kuna lecture mmoja mmbongo pale BU (Boston Univesity), kuna kabinti kamoja ka Zanzibari kameshika top job fulani IMF, dada mwingine mmoja yuko WB. Head of Corporate Communication wa Africa Region ya Stan Chart Bank pale London ni dada wa Kitanzania, hawa na wengine wengi, hata tuu kujichanganya kwenye events za Watanzania wao ni no, wameshajiona wazungu!, find out kama wanafanya efforts zozote kuwavuta Watanzania wenzao angalau wawakaribie..hakuna!. Kuna wakati nimehudhuria party ya wabongo hapo DC, mtu mnafahamiana, hata tuu kukuambia anafanya nini au anaishi wapi ni issue, itakuwa kusaidiana!.

Mimi naamini wale wenye kujiamini type ya Mtsimbe wako wengi, na wenye uwezo pia ni wengi, ila ambao wa dare trying ni wachache na ndio hawa wanaotutoa kimasomaso.

Hongera Santus!.

Pasco.

Asante sana Mkuu Pasco. Tuko pamoja sana na changamoto zote ulizozielezea ni za kweli na naamini wa TZ wengi wanao uwezo mkubwa tu.
 
Ndugu Sactus,mimi napenda kukushukuru wewe kwa kuonyesha mfano kwa vijana rika lako wanaosema haiwezekani na kukata tamaa,wewe ni mfano wa kuigwa.Umetuonyesha mwanga wa kuthubutu na kuweza.

Ndugu Sactus,Napenda kumshukuru Mwanakijiji kwa kutuwekea taarifa hii,sikujua kama wewe mwanachama mwenzetu.Namshukuru kwa kupenda kutushirikisha taarifa hii njema kama angeamua asingetuambia ila kwa kujua umuhimu wake na kutupa changamoto sisi vijana wa kiTanzania kaamua kutuweka hapa.
Namshukuru sana saana Mwanakijiji,ubarikiwe sana

Ndugu Sactus,Napenda pia kuwashukuru hata wale ambao hujawashukuru,Mkeo,watoto,na ndugu zako ambao kwa namna moja au nyingine wamechagia kupata nafasi hii adimu.Nawashukuru sana.

Ndugu Sactus,pia si vibaya kuwapa shukrani wale washindani wako kwenye interview ambao kwa namna moja au nyingine nao walithubutu ila Mwenyezi Mungu alikuchagua wewe sanjali na vigezo vyako vya elimu na uzoefu wako kazini.

Ufudu; nakushukuru sana na pia kwa yote uliyoyaandika. Ni mema tu. Stay blessed.
 
Hongera Sanctus!!
Unakumbuka 1985 JKT Ruvu (Operation Okoa) tukiwa kombania ya mapokezi kwa mzee Massanja? kale ka-group ka kupiga story kabla ya kulala kutafakari siku inayofuata? baada ya u service na ma-bog sijakuona tena hadi leo kwenye hii picha ya mzee Mwanakijiji!! hongera sana and kanyaga hapo hapo usiondoe mguu!!

Haaaa haaaa Nyantella umenikumbusha mbali sana. Kuna siku afande Lucas alinipigia kelele kuwa "Atanitemea mate yake yenye sumu ya nyoka nikatibiwe Afrika kusini" kisha akamalizia "sijui utaendaje wakati mipaka yote imefungwa" enzi hizo bado mapambano na makaburu yalikuwa yanaendelea.

Asante sana Mkuu. Tutafutane kwa PM.
 
Congratulations On Your New Job
I want to say my heartfelt "Congratulations"
How glad I am for you, God has answered every prayer for all you seek to do.
~*Congratulations*~
May God bless and keep you in all ways
always..................................

Hello FL1, thank you for your nice words.

God bless you too Mama wa Kwanza - 1.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom