Hongera sana waziri wa afya kumng'oa mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera sana waziri wa afya kumng'oa mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maluluma, Mar 17, 2012.

 1. m

  maluluma Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatimaye jibu la kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi wa taasisi ya chakula na lishe Tanzania limepatikana. Ilikuwa ijumaa siku ambayo wengi wao hawakutegemea kuwa hayawi hayawi YAMEKUWA. Taasisi kwa kipindi kirefu ilikumbwa na dhoruba kubwa sana ambapo wafanyakazi wengi walitamani siku moja kushuhudia mabadiliko ya uongozi wa katika yao unabadilika kufuatia kero kubwa zilizo sababishwa na mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Ndosi. Katika kipindi akiwa kama bosi taasisi hii imekumbwa na kero nyingi sana. Baadhi ya kero hizo wafanyakazi wengi kunyanyaswa, kuonewa, kutotedewa haki na upendeleo katika mishahara, kutopandishwa vyeo kwa baadhi ya wafanyakazi, kutokuwa wazi ktk utendaji wa masuala mengi ya fedha na nyaraka mbalimbali. mambo mengine ni tuhuma za ufisadi, lugha mbaya kwa wafanyakazi na maendeleo ya taasisi kudidimia kabisa ukilinganisha na kipindi chochote kile ktk uongozi wa taasisi. Taasisi ina majengo chakavu, magari yamechakaa na msululu wa mambo mengi ya kusikitisha.

  Katika kipindi chake tumeshuhudia tume nyingi za uchunguzi zikija kuchunguza tuhuma mbalimbali alizokuwa nazo, lakini aliweza kuzima na mpaka sasa hakuna hatua iliyochukuliwa. Hivyo wengi tulikuwa tukisubiri siku ya kustaafu kwake. Kibaya zaidi huyu bwana alikuwa hataki kustaafu licha ya kufikia umri wa kustaafu. Lakini kumbe akawa ameomba mkataba wa kuendelea. Mungu mkubwa, kigogo (Nyoni) aliyekuwa anataka kumpa mkataba akaondolewa wizarani kupitia mgomo wa madaktari.

  Hakukataa tamaa. Akatupa kete nyingine. Mara hii ya pili akaomba mkataba kwa mkataba wa kuendelea kubaki kwa waziri wa afya na baadaye akatangaza mbele ya menejimenti ya tarehe 9/3 kuwa ataendelea kwa maana hatastaafu kwasababu hakukuwa na mtu wa kumwachia taasisi. Hatua hiyo iliwasikitisha sana wafanyakazi. Lakini ilipofika ijumaa tarehe 16/3 tukashuhudia anaitisha kikao cha wafanyakazi na kuaga. Hii ilisababishwa na barua toka wizara ya afya kumshinikiza astaafu. Hivyo wafanyakazi tuna pongeza uamuzi wa busara kubwa wa waziri wa afya watendaji wa sasa wa wizara ya afya. Wafanyakazi wengi wamepokea kwa furaha uamuzi huo na pili umeepusha rabusha ambazo zingetokea kwa bwana huyu kuendelea kung'ang'ania madaraka wakati taasisi iko mahtuti sana (ICU). Wafanyakazi wanasherekea gogo kung'oka.
   
Loading...