Hongera sana NSSF kwa kutoa mikopo, lakini...

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Kwa sasa sihitaji tena kuzungumzia ugonjwa unaoitwa CORONA, kwasababu hapa nchini kwetu ugonjwa huo watu wengi badala ya kuuchukulia kwa umakini zaidi... Lakini wengi wanauchukulia ugonjwa huo kisiasa-siasa zaidi.

Leo wacha niwasifu kidogo NSSF kwa kujaribu kuwajali wateja wake kutokana na kutoa huduma ya mikopo kwa wanachama wake kupitia Benki ya AZANIA.

Siwasifu kwa asilimia %100 bali nawasifu kwa asilimia %50 tu. Hiyo ni kwasababu, huduma hiyo ya mkopo haiwezi kuwasaidia wanachama wengi nchini bali wanachama wachache tu.

Ni AZANIA Benki tu, kwa ushirikiano na NSSF ndio waliodhamiria kutoa mikopo kwa wanachama wa NSSF nchi nzima... Lakini kwa masharti magumu.

Ukienda AZANIA Benki kuomba mkopo kwa udhamini wa NSSF, utatakiwa kwanza upeleke barua au MKATABA wa kazi toka kwa mwajiri wako. Kwa wale waliostaafu kazi ambao bado hawajalipwa mafao yao, kwa upande wao hakuna masharti yoyote... Wao wanakopeshwa kwa haraka bila matatizo.

Je, ni wafanyakazi wangapi nchini ambao wameajiriwa kwa maandishi (mikataba)? Je, ni waajiri wangapi ambao wanaweza kuwadhamini wafanyakazi wao Benki kwaajili ya kuomba mikopo? Je, ni waajiri wangapi ambao wamekuwa wakiwasilisha kikamilifu michango ya wafanyakazi wao NSSF?

Hapa ndipo ninapoona tatizo kubwa la wanachama wengi wa NSSF nchini, kutoweza kupata mikopo kupitia Benki ya AZANIA. Hivyo, ni vyema NSSF ijipange upya kwaajili kuboresha huduma hiyo ya mkopo kwa wanachama wake.
 
Mkuu dadavua kidogo nataka nikachukue hela,mkopo kwa mda gani na limit Ni kiasi gani
 
Kwanini NSSF wenyewe wasitoe mikopo na baadala yake wakudirect ukakope Azania ambako utapigiwa hesabu ya riba za benki??
Nilichoelewa hapa NSSF ni kama mdhamini tu kwasababu tayari una hela zako kule na mwajiri anatumika ili kujua capacity yako ya kulipa kwa mwezi..

NSSF acheni janja janja, jengeni nyumba nzuri zenye mandhari yaliyo bora na kwa gharama zenye uhalisia halafu mkopeshe wanachama wenu kwa malipo ya kuanzia miaka 10 kwa riba ndogo..
 
Back
Top Bottom