Hongera sana Mtangazaji na mchambuzi Kibwana Dachi wa Channel Ten na redio Magic FM kwa kazi nzuri

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Kibwana Dachi ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari Mwandamizi kiukweli napenda sana kwanza anavyochambua taarifa na habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Kitu kikubwa ambacho anacho huyu mtangazaji na mchambuzi ni kumbukumbu ya matukio mengi ya nchi na kuyaelezea bila kuegemea upande wowote.

Ingawaje baba yake alikuwa Ofisa mwandamizi wa Jeshi la Magereza na CCM ndani lakini mara zote Kibwana Dachi amekuwa Neutral Katika kazi yake siku zote.

Kama ni kuisema Serikali mahali ilipokesea anasema na kama ni upinzani atasema tu.

Hi sifa ni watangazaji na waandishi wa habari ni wachache sana wenye nayo wengi wao wanaonyesha upande wazi wazi kabisa.

Hongera sana Kibwana Dachi kwa kazi nzuri hasa ktk kipindi cha Morning Magic cha Redio Magic kinachorushwa Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:30 asb hadi saa 4 asb anapokuwa anachambua habari mbalimbali.
 
Mkuu Tramadol huwa tunatofautiana kwenye issue ya CCM na Chadema,ila kwenye hii mada niko nawewe.Jamaa ni mwandishi kweli,yuko neutral sana na uchambuzi wake unavutia kuendelea kumsikiliza.
 
Mkuu Tramadol huwa tunatofautiana kwenye issue ya CCM na Chadema,ila kwenye hii mada niko nawewe.Jamaa ni mwandishi kweli,yuko neutral sana na uchambuzi wake unavutia kuendelea kumsikiliza.
Namshukuru ....lakini siko CCM wala Chadema wala chama kingine chochote.
 
Jamaa baada ya Ile Ban kipind cha morning magic ni hovyo

Sent From My Nokia Ya Tochi
Kibwana yuko vizuri sana.Kipindi kile walivuka mipaka ya maadili ya kazi zao ndiyo maana Nape Nnauye alikifungia.
 
Walikuwaga zamani hao ila baada ya kupigwa ban na TCRA sa iv wamekuwa kama TBC, huko channel 10 kila baada ya muda lazima waweke matangazo ya Makonda mara kuhusu barabara, mara ujenz wa nyumba za walim, na upimaji wa afyA buree..
Sasa cjui anawazamini au ni shobo zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom