Hongera sana Mkuu wa Mkoa wa Geita

SAIZI YANGU

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
381
83
Kwa kipidi kirefu Mkoa mpya wa Geita ulikuwa haujapata Mkuu wa Mkoa ambaye ni makini kama aliyepo sasa Jenerali Kyunga.

Kamanda huyu amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi hasa kwa kuwaambia ukweli wamiliki wa Migodi mingi iliyopo hapa Geita.

Kwa sasa hali nzuri inaanza kuonekana ambapo wamiliki hawa wanatakiwa kutoa mchango wa maendeleo na si kuamua kusaidia.

Tunashukuru sana Rais Magufuli kwa kutuletea kamanda huyu. Najua atapigwa vita lakini kwakuwa ni mwanajeshi bila shaka hayo hayatampa shida.
 
Sijui umetumia vigezo gani kumsifia lakini kinachofanywa na RC huyu ni kilekile kilichokuwa kinafanywa na RC aliyepita lakini pia Migodi mingi inachangia huduma za jamii tatizo watendaji wa serikali walikuwa wanaihamishia kwenye matumbo yao na vilevile ilikuwa haitangazwi vya kutosha ndo maana GGM wameamua kuanzisha vipindi vya TV kuielezea jamii mambo waloyosaidia.
 
Kwa kipidi kirefu Mkoa mpya wa Geita ulikuwa haujapata Mkuu wa Mkoa ambaye ni makini kama aliyepo sasa Jenerali Kyunga. Kamanda huyu amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi hasa kwa kuwaambia ukweli wamiliki wa Migodi mingi iliyopo hapa Geita. Kwa sasa hali nzuri inaanza kuonekana ambapo wamiliki hawa wanatakiwa kutoa mchango wa maendeleo na si kuamua kusaidia. Tunashukuru sana Rais Magufuli kwa kutuletea kamanda huyu. Najua atapigwa vita lakini kwakuwa ni mwanajeshi bila shaka hayo hayatampa shida.
Katika Uzi wa hovyo tangu Mwaka huu uanze,huu unaweza kuongoza,kilifanya umpongeze hakijulikani,alichotetea hakijulikani,unaomba migodi ichangie maendeleo wakati wanachangia kupitia kodi serikali kuu na halmashauri,hivi mtu akishakuwa Ccm anakuwaje?
 
Awali ilikuwa MGODI ndo unaamua nini wafanye bila kufuata priority za community. Kwasasa community ndo watatoa priority zao ambazo ndizo zinapaswa kutekelezwa na migodi.
 
Sijui umetumia vigezo gani kumsifia lakini kinachofanywa na RC huyu ni kilekile kilichokuwa kinafanywa na RC aliyepita lakini pia Migodi mingi inachangia huduma za jamii tatizo watendaji wa serikali walikuwa wanaihamishia kwenye matumbo yao na vilevile ilikuwa haitangazwi vya kutosha ndo maana GGM wameamua kuanzisha vipindi vya TV kuielezea jamii mambo waloyosaidia.

Haina haja ya kuchangia jamii kwa lolote...mchango wa kampuni ni kodi na tozo walipazo serikalini,kwa hiyo mgodi ukishalipa kodi serikali haiirejeshi kwa wananchi kwa mfumo wa maendeleo ya barabara ,maji,elimu ,Kilimo?

Serikali inaipeleka wapi kodi hiyo sasa mpaka wananchi wanageuka ombaomba kwa mgodi?

Na huo uombaomba wanataka kuuchukulia kama haki yao wanadai wanadai,wanadai, wanadai kama vile huo mgodi ndio waliupigia kura....waliipigia kura serikali wakadai huko.
 
H
Awali ilikuwa MGODI ndo unaamua nini wafanye bila kufuata priority za community. Kwasasa community ndo watatoa priority zao ambazo ndizo zinapaswa kutekelezwa na migodi.
Hao msiwasikilize kama wanataka kusaidiwa msaada zaidi ya shule......wajengeeni shule tu wakasome wapate akili ya kutafuta vya kwao,vinginevyo watawaomba Jana ,Leo,kesho,keshokutwa,keshokutwa na milele wataendelea kulaumu,kulia, watanzania
 
Haina haja ya kuchangia jamii kwa lolote...mchango wa kampuni ni kodi na tozo walipazo serikalini,kwa hiyo mgodi ukishalipa kodi serikali haiirejeshi kwa wananchi kwa mfumo wa maendeleo ya barabara ,maji,elimu ,Kilimo? Serikali inaipeleka wapi kodi hiyo sasa mpaka wananchi wanageuka ombaomba kwa mgodi?
Na huo uombaomba wanataka kuuchukulia kama haki yao wanadai wanadai,wanadai, wanadai kama vile huo mgodi ndio waliupigia kura....waliipigia kura serikali wakadai huko.

Kuna kodi za aina mbili, Cooperate Social Responsibility (CSR) na Service Levy. Sasa hiyo CSR ilikuwa inapangwa na Mgodi badala ya wananchi. Wao wana shida ya barabara, mgodi unawapa msaada wa maji...utofauti huu wa perceptions na priorities umekuja kumalizwa na RC huyu. Anastahili pongezi kwakweli.
 
Na siku mungu anitupie BAHATI ya kuwa bosi halo GGM sitaki vikao visivyoeleweka na viongozi wa serikali isipokuwa TRA,polisi,wizara ya madini,kwa wenye shida ya maji sijui na nini,ntaboresha ofisi ya mbunge kwa kuipa hotline....na kuajiri Msaidizi atakayekaa hapo muda wote asikilize kero ziende serikalini
 
Kuna kodi za aina mbili, Cooperate Social Responsibility (CSR) na Service Levy. Sasa hiyo CSR ilikuwa inapangwa na Mgodi badala ya wananchi. Wao wana shida ya barabara, mgodi unawapa msaada wa maji...utofauti huu wa perceptions na priorities umekuja kumalizwa na RC huyu. Anastahili pongezi kwakweli.
CSR nayo ni kodi? Tangu lini mtu anajipangia kodi?
 
CSR nayo ni kodi? Tangu lini mtu anajipangia kodi?

Kama hujui jambo afadhali ukae kimya. CSR ni moja kati ya mambo yaliyopo katika mikataba ya uanzishaji wa Migodi. Ni lazima na siyo kujiamlia. Kutokujua sheria kwako ndo kumekuwa kunatuumiza kila siku.
 
Kuna kodi za aina mbili, Cooperate Social Responsibility (CSR) na Service Levy. Sasa hiyo CSR ilikuwa inapangwa na Mgodi badala ya wananchi. Wao wana shida ya barabara, mgodi unawapa msaada wa maji...utofauti huu wa perceptions na priorities umekuja kumalizwa na RC huyu. Anastahili pongezi kwakweli.
Kwa kawaida makampuni huweka bajeti za CSR kutegemeana na mipango na malengo yao kwa kipindi fulani. Wakati mwingine wanaoomba kupata msaada kupitia CSR ndio wanapaswa kuwasiliasha andiko (proposal) kuomba huo msaada wakionyesha pia kampuni husika itafaidikaje ikitoa huo msaada.

Kwa kesi ya migodi ya huko Geita kusaidia miradi ya kijamii kwenye maeneo yanayoizunguka, nadhani tatizo litakuwa kwa watendaji na halmashauri zenyewe kutokuwa na umakini wa kuwasilisha maombi kwa ajili ya miradi inayohitajika zaidi na wananchi, na hivyo migodi kuamua yenyewe miradi ya kutekeleza. Na ninadhani katika hili ndipo hufanyika "ulaji"!
 
Wana Geita na wa kanda nzima ya Ziwa! Tusisahau kutokomeza umasikini wa vipato kwa wananchi wetu! Naona tumetekwa zaidi na siasa....! Tufanyeje ili tujikomboe? Hali ni mbaya sana! Mikoa 5 ya mwisho ni kanda moja tu ya Ziwa! Aibu!!
 
Back
Top Bottom