Hongera Sana John Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Sana John Mnyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amanikwenu, Jan 5, 2011.

 1. A

  Amanikwenu Senior Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwangu mimi moja ya sasabu kuu ya kumfanya Kikwete akubali suala la kuwa na katiba mpya ni fedheha ya kusubiri kupewa maelekezo na Bunge nini Serikali inapasa kufanya kuhusu suala la kuwa na katiba mpya. Kitendo cha John Mnyika kupeleka hoja binafsi katika ofisi za Bunge kutaka Bunge litoe muongozo kuhusu uundaji wa katiba Mpya naamini kimechangia sana kumfanya Kikwete akubali suala la kuwa na Katiba Mpya japo kwa shingo upande vinginevyo angebaki peke yake. Kwa hili nampongeza sana Mbunge John Mnyika kwa kile alichokifanya kwa faida ya Watanzania.
   
 2. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  JK anatekeleza exactly alichokuwa anakihubiri Dr Slaa wakati wa kampeni kuhusu mchakato wa katiba kuanza ndani ya siku 100. JK kaanza siku ya 61!
  CCM na vibaraka wake kama kina Mbatia walimbeza Dr lakini ebu angalia kinachoendelea sasa!
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  labda na sisi tubadilike kidogo tuwe wa kweli na sio kusifia wachadema tuu kila mara ;;nafikiri kila jambo lina wakati wake na huu ni wakati wa katiba mpya upepo huo hauzuiliki hata kama mnyika angekaa kimya,mbona haya mapambano yapo muda lakini sasa yamewashinda na wameamua kusaliti amri mimi naamini huu ndio wakati wake hata kusingekuwa na chadema wala mnyika
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi hypothetically speaking kesho JK au hilo bunge likipewa nafasi ya kutunga hiyo katiba mpya tunataka iweje tofauti na ya sasa mpaka tunadai mpya kabisa ukitoa matatizo ya nguvu za raisi na mkono wake mrefu kupunguzwa labda na mambo ya muungano. Kingine ni kipi kinachotufanya tudai katiba mpya kabisa? au tunataka iweje tofauti na ya sasa?

  Trust me sehemu kubwa ya matatizo yetu ni viongozi wetu lelema pia wanachangia. Lakini katiba yetu aina matatizo ya hivyo mpaka kudai mpya kabisa, kwanza mnaposema mpya ina maana mnataka kuamia kwenye federal constitution ni aina ya katiba mbili tu zilizopo duniani. Na azija andikwa kumridhisha kila mtu bali kuongoza na kuunganisha jamii, mara kwa mara huwa zinarekebishwa kutokana na muono mpya kijamii lakini si kutunga mpya.

  Naona wenzetu mmekazana na katiba mpya mnataka iweje sasa embu tuelekezeni kabla hatujatupa hela kukusanya information ambazo already zina exist on the current one, only to discover we have poor politicians in the first place who dont have enough political qualities to challenge the opposition.
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  KATIBA YENYEWE INAITWA "KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA"" Wakati haitumiki Zanzibar huoni kama tuna taka katiba mpya amka ndugu
   
 6. A

  Amanikwenu Senior Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lazima tukubali kuwa bila ya Pressure na umakini wa CHADEMA Kikwete asingekubali. Maji yamezidi unga.
   
 7. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  tena inaitwa ya mwaka 1977,haufikirii kama tunataka mpya tuu,imesainiwa na AG Andrew Chenge heee huyu si fisadi papa?huoni bado tunataka mabadiliko mkuu amka;;
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  usilazimishe chadema kwani MKpa ni CHADEMA,Joseph Warioba na Jaji mkuu mstaafu ni CHADEMA??Sumaye na Pinda ni CHADEMA?
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  msajili wa vyam JOHN TENDWA NI CHADEMA?? MTIKILA NA MTATIRO NI CHADEMA?DONT FORCE supiriority it has to come itself hili ni jambo la watanzania tena ulkiangalia vizuri CHADEMA tumelidandia kwa mbele tuuu,au hujui nini??
   
 10. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe son of Pinda naona una tatizo walikuwa wapi kuidai kabla ya uchaguzi? mbona mpaka CHADEMA waliposusia hotuba na kuwasha moto sasa kila mtu anataka naye alikuwepo. Huu ni unafiki kama wa CUF tu.

  CHADEMA wanaplay role kubwa kuleta mabadiliko kwa umma na serikali iliyolala pono.
   
 11. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mimi nipo macho, hila nipo realistic vilevile najuwa kuna matatizo mengi ya msingi particularly nguvu za juu kwetu ni tatizo ambazo zinafanya independent bodies to play under the strings of the few. Lakini aina maana ya kusema tunataka katiba mpya kabisa, na kama kuna ulazima wa hivyo iandikwe tunataka iweje tofauti na ya sasa? au tunadai mpya bila ya kujua mwisho tunataka iweje?

  katiba ya Tanzania ni Tanzania na Zanzibar as union state inaweza ikawa na ya kwao, Mfano Scotland wana bunge lao, Wales wanabunge lao for devolution purposes hili waweze kuwa na autonomy katika local decisions lakini mwisho wa siku wote wapo chini ya imaya ya katiba ya GB.
   
 12. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0  ""WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliondoka bungeni mara Rais Jakaya Kikwete alipoanza kuhutubia Bunge mjini Dodoma. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema waliondoka kutilia mkazo wao kutotambua mchakato uliompa Kikwete urais"".

  soma vitu uelewe acha uzushi na sanaa
   
 13. A

  Amanikwenu Senior Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tzjamani, umenena.
   
 14. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  GB Hawana katiba wewe umesoma wapi?? wana unwritten agreement ambazo zaweza kuwa unwritten articles of association.Rudi shule;;
   
 15. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pumba zingine athee, sasa hizi 'acts' zao ni nini au zinabadilishwa kwa misingi hipi? wanayo constitution hila hipo in the form of uncodified kwa lugha yako ni kwamba rules zipo na zinabadilishwa kila siku hila azipo kwenye kitabu kimoja ndio maana wanasema hawana written constitution sijui mwenzetu shule gani umeenda wewe hiwapo hata hujui katiba ni nini.
   
 16. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Kwa nini hutaki CDM wasifiwe. Ukweli unabakia hapo, kuwa Katiba mpya haiko ktk ilani ya CCM na bila shinikizo la CDM labda usingemsikia kikwete akianza kutekeleza (Japo ni kazi ya bunge) ilani ya CDM ndani ya siku 100. Mh. Mnyika amefanya iliyo haki yake kwa manufaa ya wananchi! Kwa nini asisifiwe? Acha wivu!
   
 17. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu,

  Tuache kuzunguka mibuyu na vichaka,
  Katiba ya JMT ina mapungufu makubwa ya msingi na madogo mengi sana,
  Inahitaji mabadiliko makubwa sana,
  Hii sio katiba ya watu kwa ajili ya watu,

  Kwa ufupi kuna maeneo mengi sana ya kuchambuliwa na kuwekwa sawa:

  >Tume ya uchaguzi na mamalaka yake
  >Mamlaka yasiyo na kikomo ya raisi (udikteta) hasa uteuzi wa nafasi vyeti
  >Muundo wa serikali ya muungano (katiba ya JMT in waziri kiongozi, ya SMZ haina - :embarrassed:)
  >nk
   
 18. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Wivu wa nini?kama swala hili limeznzia CHADEMA basi mimi ndio mwanzilishi wake ,lakini najua sio sisi tulioanza jambo hili na ukweli lazima tuuseme msiwe vigeu geu sisi ni chama tuu na tunaongoza mawazo ya watu issue ya katiba haijaanzishwa na CHADEMA kubali au kataa sisi ndio tuliopo hapa na ndio tunaojua nini tunatakla CHADEMA usilete porojo
   
 19. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Haya bwana wacha nikupe hii kama unajua kidhungu kidogo unaweza kupata kitu

  A constitution is a set of fundamental principles or established precedents according to which a state or other organization is governed.These rules together make up, i.e. constitute, what the entity is. When these principles are written down into a single or set of legal documents, those documents may be said to comprise a constitution
   
 20. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  umekaa kimya nimekugusa eeeeeeeeeeeeh;;au ulikuwa cyber cafeeeeeee na chapaaa amekwenda zake au bosi wako muhindi yuko around utajibu badae

  usilolijua usilizungumziae utaumbuka;;parachichi wee
   
Loading...